Papa hospitalini ni mapumziko na maji kama chakula na utaratibu kawaida baada ya upasuaji
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi 8 Juni 2023 siku moja baada ya kupata operesheni, alitumia siku ya kupumzika na kula chakula cha maji. Viungo ‘haemodynamic ‘na mfumo wa kupumua ni imara. Hatua zote baada ya upasuaji ni za kawaida” kwa mujibu wa madaktari wamesema. Ikumbukwe kuwa Timu ya madaktari wa matibabu walikuwa wamethibitisha juu ya hali ya kiafya ya Papa kwamba, mapema alasiri tarehe 7 Juni, alifanyiwa upasuaji wa laparotomy na plastiki ya ukuta wa tumbo kwa kutumia viungo bandia katika hospitali ya Gemelli. Na walifafanua jinsi gani waliweza kufanya operesheni hiyo na sababu za kufanya hivyo hasa maumivu makali kutokana na makovu ya ndani baada ya upasuaji alio wahi kuupata Papa siku za nyumba katika maisha yake.
Na katika maelezo yaliyotolewa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican jioni pia tunasoma kwamba: “Mchana wa leo, tarehe 8 Juni, katika fursa ya Maadhimisho ya (Corpus Domini) Mwili na Damu ya Yesu Papa alipokea Ekaristi.” Kama walivyokuwa wametaarifa mapema asubuhi, vilevile ilikuwa mara kwa mara timu ya matibabu karibu saa sita mchana ambao waliripoti maelezo juu ya hali ya afya ya Papa katika siku yake ya kwanza baada ya upasuaji. Taarifa kwa vyombo vya habari ilizungumza juu ya usiku wa kwanza ulivyotumiwa kulala kwa amani, kwa hali nzuri kwa ujumla ya Papa Francisko kupumua kwa uangalifu na kwa hiari. “Vipimo vya udhibiti wa kawaida ni vizuri,” madaktari walisema, na kuwa “kwa siku nzima atazingatia mapumziko muhimu baada ya upasuaji”. Na ndivyo ilivyokuwa, ripoti kama ilivyothibitishwa na taarifa ya pili kwa vyombo vya habari jioni.
Kwa siku nzima kama ilivyokuwa alasiri ya tarehe 7 Juni 2023, kulikuwa na utiririshaji wa ujumbe uliotoka sehemu mbali mbali za dunia: watoto wagonjwa wa Hospitali ya Kipapa ya Gesu Bambino, ambao walichora picha na kumtumia kupitia Tweeter, Jimbo la Roma na Mabaraza ya Maaskofu duniani, vyama na harakati za kikanisa wamemwahakikishia sala, upendo na mshikamano na pia Rais Sergio Mattarella, Italia.
Baba Mtakatifu Francisko alipendelea kumpigia simu mwanamke mmoja, ambaye alikutana naye tarehe 31 Machi 2023 wakati wa kulazwa hospitalini kwa ugonjwa wa bronchitis, katika wodi ya Saratani ya watoto. Katika tukio hilo, Papa alikuwa amembatiza mtoto mdogo wa siku chache, aliyelazwa hospitalini kufuatia kuanguka vibaya kutoka kiti cha juu. Hata hivyo Moto Miguel Angel hakuwa na ugonjwa mbaya ni sababu yya kuanguka tu na kupoteza fahamu. Mama huyo kijana kwa hiyo alhamisi tarehe 8 Juni 2023 amemtumia salamu Papa za matashi mema ili aweze kupona haraka kutoka kwa familia yake. Mchana walizungumza kwenye simu: utani kidogo, salamu, maneno ya upendo kwa mtoto ambaye amepita mtihani mkubwa.
Mpangilio ni sawa kila wakati, huko Hospitali ya Gemelli, ambapo Papa amelazwa hospitalini tangu tarehe 7 kwa upasuaji wa laparotomy na upasuaji wa plastiki wa ukuta wa tumbo kwa kutumia viungo bandia. Akiwa katika ghorofa ya kumi, Papa Francisko alijua kwamba wakati wa mchana mama wa mtoto aliyekutana naye katika idara ya Saratani kwa watoto na idara ya upasuaji wa neva za watoto wachanga alipokuwa amekuja hospitalini mwishoni mwa Machi iliyopita,wakati Papa alipolazwa hospitalini kwa ugonjwa wa bronchitis ya kuambukiza. Kisha Papa alimpigia simu mwanamke huyo, kwa mujibu wa ripoti Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, kwa sababu “alishangazwa na upendo uliooneshwa na mwanamke wa Peru, ambaye tayari alikuwa Italia kwa miaka kadhaa na sehemu ya familia yake, ambaye alimpatia Bango la salamu za kupona haraka”.
Bango la salamu
Mwanamke huyo alilitengeneza. Leo, kama ilivyoelezwa alimeelezea shukrani zake kwa Papa Francisko kupitia bango la salamu ambalo aliambatanisha na picha zote za familia yake ya ‘hermosa’, watoto wake Massimo Antonio na José Miguel na wengine wa familia nchini Peru. Pamoja na haya pia matashi mema ya kupona na kutoa shukrani kwa Papa kwamba: “Tunaweza tu kukushukuru kwa kumbariki ndugu yetu na tunakutakia kwa moyo wa dhati ili uweze kuwa bora zaidi, tungependa kukutana nawe ana kwa ana na kukaa alasiri pamoja ili kukufanya utambue familia yetu vizuri zaidi, familia yako, kwa sababu sasa wewe ni sehemu ya maisha yetu.”