Tafuta

MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA

Ni nini Vatican News?

Vatican News ni mtandao mpya unaotoa habari za Baba Mtakatifu, Vatican na Kanisa la Kiulimwengu kwa upana zaidi bila kusahau habari za kimataifa. Vatican News inapatikana hata kwenye mitandao ya kijamii kama vile: Facebook, Twitter, YouTube na Instagram.

Kwa matatizo ya kiufundi unaweza kuwasiliana nasi kwa anuani ifuatayo:

 kiswahili@vaticannews.va  au webmaster@vaticannews.va.

Je, ninaweza kutumia habari zilizochapishwa kwenye Vatican News?

Kuhusu masharti na vigezo, tunakushauri uangalie ukurasa unaohusiana na masuala ya haki miliki na sheria kwa anuani ifuatayo.

Je, Ninaweza kupata wapi hotuba rasmi ya Baba Mtakatifu Francisko?

Tembelea tovuti rasmi ya Vatican kwa anuani ifuatayo.

Je, ninawezaje kufahamu tarehe za matukio muhimu ya shughuli za Baba Mtakatifu Francisko?

Tembelea tovuti ya Vatican inayoonesha Kalenda ya Maadhimisho ya Liturujia ya Baba Mtakatifu kwa anuani ifuatayo.

Je, ninawezaje kupata baraka za kipapa?

Tembelea tovuti ya Mtunza Sadaka wa Papa kwa anuani ifuatayo.

Je, ninawezaje kushiriki katika Katekesi ya Baba Mtakatifu siku ya Jumatano?

Tiketi kwa ajili ya kuhudhuria Katekesi ya Baba Mtakatifu kwa Siku ya Jumatano zinatolewa bure. Ili kupata tiketi yako, tunakushauri kutembelea tovuti ya Nyumba ya Kipapa kwa anuani ifuatayo.

Je, ninaweza kutumia anuani gani kuwasiliana moja kwa moja na Baba Mtakatifu Francisko?

Ukitaka kumwandikia Baba Mtakatifu Francisko barua, unaweza kutumia anuani ifuatayo: Baba Mtakatifu Francisko. Casa Santa Marta. 00120 Città del Vaticano”.

Je, ninawezaje kuchangia Injili ya upendo wa Baba Mtakatifu kwa maskini?

Injili ya upendo wa Baba Mtakatifu imedhaminishwa kwa Mfuko wa Mtakatifu Petro. Mfuko huu ni msaada mkubwa kwa ajili ya utekelezaji wa huduma mbali mbali zinazotolewa na Kanisa la Kiulimwengu. Kwa ushiriki wako katika mshikamano na maskini unaweza kutembelea tovuti ifuatayo kwa habari zaidi.

Je, ninaweza kupata wapi maelezo kuhusu Makumbusho na Bustani za Vatican?

Kwa habari zaidi kuhusu tiketi, kuomba nafasi ya kutembelea kama mtu binafsi au kwa kusindikizwa kwenye: Makumbusho ya Vatican, Bustani za Vatican, Ikulu Ndogo ya Castel Gandolfo, tunakushauri utembelee ukurasa maalum uliotengwa kwa ajili ya huduma hizi.

Je, ni muda gani Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican linafunguliwa kwa huduma?

Ukitaka kufahamu ratiba ya Ibada ya Misa Takatifu na Sakramenti ya Upatanisho katika Makanisa Makuu ya Kipapa yaani (Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo nje ya Kuta, Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane wa Laterano na Kanisa kuu la Bikira Maria Mkuu) unaweza kutembelea tovuti rasmi kwa anuani ifuatayo.

Je, ninaweza kununua wapi fedha za kumbu kumbu na stampu za Vatican?

Ili kuweza kupata habari muhimu kuhusiana na ununuzi wa stamp za Vatican unashauriwa kutembelea ukurasa wa tovuti ya Serikali ya Mji wa Vatican, maalum kwa ajili ya huduma hii kwa anuani ifuatayo.

Je, ninawezaje kununua picha niliyopiga na Baba Mtakatifu Francisko?

Ili kununua au kuagiza picha ya matukio ya hadhara na Baba Mtakatifu Francisko, tunakushauri kutembelea tovuti ya Huduma ya Picha ya Vatican na Vyombo vya Mawasiliano vya Vatican kwa anuani ifuatayo.

Je, kuna huduma ya webcam huko Vatican?

Ndiyo! Ukiwa unataka kufuatilia matukio yanayotendeka katika maeneo muhimu zaidi mjini Vatican unaweza kwa kutembelea ukurasa wa Webcam wa Serikali ya Vatican kwa anuani ifuatayo.