Tafuta

Papa amelala salama: Tuzidi kumuombea!

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari Vatican kupitia Telegram ya saa 2.38 , Alhamisi tarehe 8 Juni 2023 zinahabarisha kuwa " Usiku umepita vizuri na habari zaidi zitajulishwa kwa wakati.”

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Alhamisi asubuhi tarehe 8 Juni 2023, kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari Vatican kupitia Telegram ya saa 2.38 kuhusiana na afya ya baba Mtakatifu na kulazwa na kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Gemelli, Roma siku ya Jumatano 7 Juni 2023, inabainisha kuwa: “Usiku umepita vizuri na habari zaidi zitajulishwa kwa wakati.”

Wakati wa kuwasilisha hali halisi ya Papa baada ya upasuaji
Wakati wa kuwasilisha hali halisi ya Papa baada ya upasuaji

Hata hivyo Msemaji wa vyombo vya habari Vtican, Dk. Matteo Bruni, jioni sana  tarehe 7 Juni 2023 alisema kuwa: Baba Mtakatifu, aliyelazwa katika hospitali ya A. Gemelli alifanyiwa upasuaji ulioratibiwa na kufanywa mapema alasiri na Profesa Sergio Alfieri, Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Tiba na Upasuaji ya Metaboliki ya Tumbo na Endocrine, akisaidiwa na Dk. Valerio, Dk. Roberta Menghi, Dk. Antonio Tortorelli na Dk. Joseph Quero; upasuaji ulifanyika chini ya anesthesia (dawa ya usingizi) ya jumla na Professa Massimo Antonelli, Mkurugenzi wa Idara ya Dharura, ‘Anaesthesiological’ na mazoezi ya kusaidia kuamka,  akisaidiwa na Dk Teresa Sacco, Dk. Paola Aceto, Dk. Maurizio Soave na Dk. Giuseppina Annetta kwa uwekaji wa dawa ya usingizi hadi ufikiaji wa mishipa ya kati. Pia waliokuwepo katika Chumba cha Upasuaji Profesa.Giovanni Battista Doglietto, Mkurugenzi wa Mfuko wa Usaidizi wa Afya, na Dk. Luigi Carbone, Daktari wa Kurugenzi ya Afya na Usafi wa mji wa Vatican.

Taarifa zilizotolewa moja kwa moja na Profesa Alfieri, ambaye alifuatilia operesheni alisema: “Leo mchana, katika hospitali ya Gemelli Baba Mtakatifu alifanyiwa upasuaji uliopangwa kwa hernia ya ndani kwenye eneo la kovu la upasuaji wa laparotomy (yaani ukuta wa tumbo katika eneo maalumu ili kufikia viungo vya ndani vilivyomo) wa  awali uliofanyika miaka iliyopita. Herinia hii ya mkato ilimsababishia Baba Mtakatifu, kwa muda wa miezi kadhaa, ugonjwa wa uchungu na mbaya zaidi wa tumbo. Wakati wa uingiliaji wa upasuaji, mshikamano thabiti ulipatikana kati ya mizunguko ya sehemu ya katikati ya utumbo mwembamba na ‘peritoneum ya parietali.’ Yaani safu ya nje, inayoweka uso wa ndani kabisa ya kuta za tumbo;  ambayo ilisababisha dalili zilizotajwa hapo juu. Kwa hiyo tuliendelea na kutolewa kwa adhesions yaani (makovu ya ndani) na uharibifu kamili wa makovu yenye unene kidogo. Kisha kasoro ya hernia zilirekebishwa kwa upasuaji wa plastiki ya ukuta wa tumbo kwa msaada wa kiungo bandia. Upasuaji na anesthesia (dawa ya usingizi) ya jumla ilikwenda bila matatizo. Baba Mtakatifu aliitikia vyema upasuaji huo.” Papa Francisko yuko macho na anaufahamu na anashukuru kwa ujumbe mwingi wa ukaribu na sala ambazo zilimfikia mara moja.”, alihitimisha Dk. Alfieri.

Ujumbe wa salamu na matashi mema

Ujumbe mwingi kutoka sehemu mbalimbali wa kumtakia heri na ukaribu kwa Papa Francisko kwa ajili ya kupona haraka umeendelea kufika kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Italia Mattarella, hadi Ikulu, kutoka Mabaraza ya Maaskofu hadi wawakilishi wa kisiasa na kiutamaduni, kwa waamini rahisi, hadi vijana na watoto wadogo wagonjwa wa Hospitali ya kipapa ya  Watoto Bambino Gesù ambao wamechora michoro mfululizo  kwa ajili ya Papa.

Imesasishwa saa 6.35

Taarifa za Papa Francisko kwa afya yake
08 June 2023, 09:56