Upasuaji wa Papa huko Gemelli ni bila matatizo&umechukua masaa matatu!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Upasuaji umekwenda vizuri. Huu ni upasuaji wa kile kinachoitwa "laparotomy" ambayo ni mbinu ya upasuaji inayohusisha kufungua ukuta wa tumbo katika eneo maalum ili kuweza kufikia viungo vilivyomo, kwa maana hiyo upasuaji wa ukuta wa tumbo na kuweka kiungo bandia" ambao Papa Francisko amefanyiwa mapema alasiri tarehe, 7 Juni 2023, katika Hospitali ya Agostino Gemelli kwamba ulifanyika "bila matatizo na ulidumu kwa masaa matatu". Hayo yalitangazwa na Msemaji wa vyombo vya habari Vatican, Dk. Matteo Bruni, akiwasilisha taarifa kuhusu operesheni ya Papa ambayo kulingana na taarifa za awali zilizotolewa asubuhi ni kwamba "imeandaliwa katika siku za hivi karibuni na timu ya matibabu inayomsaidia Baba Mtakatifu na ilikuwa imefanywa kuwa muhimu kwa sababu ya hernia iliyofungwa ya mkato ambayo husababisha kujirudia, kuumiza na kuzorota kwa dalili za maumivu makali." Kwa hiyo: "Kutahitajika kukaa katika kituo cha afya ambako kutachukua siku kadhaa ili kuruhusu mwendo wa kawaida wa baada ya upasuaji na kupona kamili," alikuwa amesema Dk. Bruni asubuhi 7 Juni 2023.
Maombi kwa Mtakatifu Teresa
Papa Francisko aliwasili katika Hospitali ya Gemelli kabla ya saa 5.30, asubuhi akiwa ndani ya gari lake aina ya Fiat 500 L, akilakiwa na waandishi wa habari na watu waliomkaribisha kwa nderemo. Hapo awali, baada ya mikutano miwili ya faragha katika Jumba la Kitume, na mara baada ya katekesi yake Jumatano, alisimama kama kawaida mwishoni ili kuwasalimu waamini na mahujaji waliokuwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Mwanzoni alikuwa ametoa heshima kwa masalio ya Mtakatifu Tereza wa Mtoto Yesu, katika fursa ya kumbukumbu ya miaka 150 ya kuzaliwa kwa mtakatifu. Papa aliweka waridi nyeupe mbele ya Sanduku la Masalio.
Papa pia alitoa ujumbe wake katika Twitter kutoka katika akaunti yake ya @Pontifex kwa Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu katika lugha tisa, akitoa mwaliko wa kumwomba: "Mtakatifu mlinzi na msimamizi wa utume wa kimisionari kwa neema ya kumpenda Yesu kama alivyompenda, kumpa majaribu na huzuni zetu, kama alivyofanya, ili ajulikane na kupendwa na watu wote."