Papa amepokea ujumbe wa matashi mema akiwa hospitali
Na Angella Rwezaula, Vatican.
Katika mchoro inaonesha andiko: “Usiogope, tuko pamoja nawe”. Ni andiko la kutia moyo kutoka kwa watoto waliolazwa hospitalini kama yeye lakini katika hospitali ya watoto Bambino Gesù Roma ambayo Papa anaifahamu vizuri, na ni Hospitali ya Kipapa, kwa hiyo imemfikia Baba Mtakatifu Francisko kupitia ujumbe wa Twitter na mchoro huo. Baba Mtakatifu Francisko kwa maana hiyo amepokea ujumbe mbali mbali kutoka ulimwenguni kote kumtakia matashi mema na ili aweze kupna kwa haraka. Hiyo ilitokea mata tu baada ya kutoa taarifa tarehe 7 Juni 2023 katika vyombo vya habari Vatican, utiririshaji wa ujumbe ulitoka Baraza la Maaskofu wa Italia waliomwakikishia sala na upendo wa makanisa yote ya Italia “katika wakati huu zaidi wa majaribu” wakimtakia ahueni ya haraka, Mabaraza mengine ya Maaskofu yametuma salamu zao kwa Papa Francisko kama vile Maaskofu wa Ufaransa waliandika: “Mungu amsaidie katika majaribu yake na amtie nguvu katika utume wake”.
Rais wa Baraza la Maaskofu wa Marekani, Askofu Mkuu Timothy P. Broglio, aliwaeleza waamini kwamba: “Papa Francisko anapopata nafuu baada ya upasuaji, anaimarishwa kwa imani katika nguvu ya uponyaji ya Mungu wetu mwenye huruma. Baba Mtakatifu Francisko na wote walio hospitalini muwaweka katika maombi yenu leo na kila siku. Yesu daima anatembea nasi na yuko karibu zaidi tunapohitaji uponyaji na faraja”. Ujumbe wa kumtakia uponyaji wa haraka pia ulitumwa na Askofu Mkuu Sviatoslav Shevchuck, wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraine.
Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Amerika Kusini (Celam), kwa njia ya ujumbe mfupi uliotolewa na Askofu Spengler, Rais wa Baraza hilo na Askofu Lizardo Estrada Herrera, katibu Mkuu, walitoa mwaliko wa kusali kwa ajili ya uponyaji wa Papa ambao walionesha ukaribu na upendo katika mchakato wa uponyaji. “Tunamshukuru Mungu kwamba (uingiliaji kati) umekwenda bila matatizo”. Maaskofu wa CELAM waliandika na kuwaalika watu wote wa Amerika ya Kusini na visiwa vya Karibiani kuungana katika sala kwa ajili ya uponyaji wa haraka na kamili wa mpendwa wao Papa Francisko. “Kwa Bikira Maria mama wa huruma na faraja kwa wagonjwa” waliomba “kumlinda na kumtia nguvu Papa ili aweze kuendelea kuwaongoza kama mchungaji wa ulimwengu wote na kuimarisha umoja wao”. Kwa namna ya pekee Maaskofu wa Peru kupitia kwa rais wao Askofu Mkuu Miguel Cabrejos Vidarte wanawaomba waamini kusali ili Baba Mtakatifu Francisko aweze kupona haraka. “Sala ya kibinafsi na ya jumuiya ya Watu wa Mungu ndiyo nguvu yetu kuu katika kukabiliana na matatizo ya afya ya Baba yetu Mtakatifu Francisko”.
Mshikamano wa Rais Mattarella wa Italia: Ujumbe wa salamu za heri kwa Papa Francisko ulifikatarehe 7 Juni 2023 , hata kabla habari kutoka Gemelli ambapo alimtakia matokeo chanya, Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella: “Watu wote wa Italia wako karibu na hisia za upendo na mshikamano, ambazo ninazipata kikamilifu. Kwa wakati huu, na pia juu ya sala za waamini wa Kikatoliki, unaweza kutegemea mawazo ya huruma ya watu wengi, waamini na wasioamini. Ninapyaisha matashi dhati zaidi ya kupona kwa amani, na kupona haraka na kamilifu”, alihitimisha.
Kanisa la Roma: Baada ya taarifa za kulazwa hospitalini, Kanisa zima la Roma, Jimbo kuu la Papa, lilimzungukia Baba Mtakatifu wakiomba baraka za Bwana kwa ajili ya kufanikisha operesheni hiyo na kupata nafuu ya haraka. Katika ujumbe waom walitoa mwaliko kwa waamini kuendelea kumuunga mkono Baba Mtakatifu kwa upendo mkuu, kushukuru kwa huduma yake kwa Kanisa leao na Kanisa la kiulimwengu na kutamani kumuona tena haraka iwezekanavyo.
Vyama na harakati: Jumbe nyingi pia zilitumwa mara moja na harakati na vyama vya kitume : ambapo wanamtakia Papa matashi mema na kumhakikishia maombi kwa Bwana ili kwa msaada wa neema yake aweze kumuunga mkono na kumfariji mpendwa wetu Papa Fransisko wakati wa uponyaji wake na ili aweze kurudi katika afya yake mapema iwezekanavyo katika kutekeleza huduma yake kikamilifu kama baba na mchungaji. “Tuna uhakika kwamba kwamba katika tukio hilo pia Papa Francis atatufundisha jinsi ya kukabiliana na mateso yanayoungwa mkono na imani ya Kikristo na matumaini. “Tunamngoja hivi karibuni katika utekelezaji kamili wa huduma yake kama mchungaji, aonesha kumbukumbu ya thamani kwa wengi”, waliandika Jumuiya ya Mtakatifu Egidio. Kwa upande Harataka ya Wafokolari nao wanamtakia Papa “heri ili Mwenyezi Mungu aweze kumhakikishia huruma, ukaribu katika majaribio haya zaidi ya maisha yake.”