Tafuta

Vatican News
2020.06.25 Mwongozo Mpya wa Katesi 2020.06.25 Mwongozo Mpya wa Katesi  

Martinez:Mwongozo wa Katekesi ni ufupisho wa huduma ya Papa!

Mwenyekiti wa Chama cha Wakarismatiki katoliki na mshauri wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Uinjilishaji Mpya anafafanua kuwa Hati ni ‘magna charta’kwa ajili ya changamoto za Milenia ya Tatu.Ni ufunuo unaofaa katika mafundisho kwa mahitaji ya wakati wetu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Bwana Salvatore Martinez, rais wa Chama cha Wakarismatiki Katoliki na mshauri wa Baraza la Uhamasishaji wa Uinjilisha Mpya, katika mahojiano na Vatican News ametumia kilelezo kuwa Hati ni ‘magna charta’kwa ajili ya changamoto za Milenia ya Tatu katika ufafanuzi wake kuhusu   Mwongozo mpya wa katekesi uliochapishwa na kutangazwa hivi karibuni tarehe  25 Juni 2020. Bwana Martinez amesema,  Mwongozo mpya  wa Katekesi ni kielelezo waziwazi cha mafundisho ya Papa Francisko. Hati hiyo ambayo pia inasisitiza hata dharura ya kujitoa kwa kila mtu aliyebatizwa ili kueneza Injili kwa kutumia kanuni tatu msingi:huruma, mazungumzo na ushuhuda kwa mujibu wa Martinez amethibitisha  huo “ ni  utaratibu wa mawazo ya Papa na utayari wake katika kutoa   huduma huku akishuhudia. Na hii ni kwa sababu changamoto kubwa za uinjilishaji mpya wa Milenia ya Tatu zinaoneshwa kwa wakati huu unaofaa na kuwa nguvu na ukweli. Mwongozo huo wa katekesi  pia ni aina ya kitaalimungu, na kikanisa hasa katika  msamiati wa Papa Francisko. Vile vile unadhihirisha njia inayofaa kwa mahitaji ya wakati wetu, katika changamoto zilizo na dalili nyingi,  kiasili,  na kutoa mwelekezo,  wa kufanya utume kimwendokasi na kwa  imani.

Katika ufafanuzi  wa Bwana Martinez anasema  Hati hiyo  inaonesha wazi  mada kuu ya kuwa na imani thabiti.  Imani ni maisha na inatakiwa  hasa katika karne hii, mwanzoni mwa milenia mpya  na kuongeza kusema, baadaye kuna uenezaji wa imani, yaani mazungumzo na tamaduni mbalimbali, mielekeo ya sasa ya mawazo. Tatu, kuna mada ya utamaduni wa mazungumzo, ya kukutana, ambayo ni nyeti kwa upande wa Papa Francisko. Yote hayo hii yamewekwa vizuri na lugha inayoeleweka na kujikitana ndani ya  muhtasari wa huduma ya kipapa  kuanzia na Wosia wake wa Kitume  ‘Evangelii Gaudium’, yaani Injili ya Furaha.

Hati ambayo inakumbusha kuwa kila mbatizwa ni mwajibikaji wa kueneza Injili kwa njia rahisi za mawasiliano, Bwana Martinez anasema kuna muktadha wa jumla ambao labda hadi jana tumeelezea hali halisi, kama vile ulimwengu wa digitali au utandawazi. Huduma ya kichungaji kwa sasa inataka kutoa umakini kwa wale ambao wako katika mantiki hii muhimu na ambayo kila kitu hufanyika na kutumiwa katika maisha yao, kwa maana ya kwamba  ni mahali ambapo wanaume na wanawake wanahitaji Injili ya Kristo. Mwongozo wa katekesi aidha unatukumbusha kwamba uinjilishaji haujafanyiki  kwa  ajili ya kupokea sakramenti tu. Ni katekesi ya kweli na siyo kuwa inapendekeza kukutana na Yesu peke yake lakini pia inayotuwezesha kuzaa matunda, kuongea na kumpeleka Kristo kwa watu wote. Ni uhusiano mkubwa uliopo kati ya malezi na uinjilishaji. Amesisitiza Bwana Martinez.

Mwongozo wa Katekesi pia unaweka wazi kutazam  familia kuwa chombo msingi kuanzia hasa katika mazungumzo ya katekesi ya kwanza. Unakumbusha wazi kuwa  familia ni fursa ya uinjilishaji ulio hai.  Familia siyo  mada ya katekesi tu,  lakini  ni mahali ambapo imani inarithishwa  na kuishi na kujiandaa kuishuhudia. Injili inazaliwa katika familia. Mwongozo wa Katekesi unapendekeza hata mada ya uhusiano wa kizazi na kizazi cha kibinadamu na kwamba  katekesi iwe   kichocheo kinachounda ili kwamba kuna shughuli mpya ambayo inaanzia kutoka kwa watoto hadi  kufikia hadi wazee, na sehemu muingine kama vile kwa wafungwa, wagonjwa , kazini , kila eneo lolote ni sehemu muafaka wa kueneza na kutangaza Injili ya Bwana.

Katika mwongozo wa Katekesi kuna sehemu ambayo inatazama maparokia, harakati na vyama vya kitume, mashule katoliki.  Harakati na vyama vya kitume vinahitaji kupokea msukumo mpya. Katika changamoto ya uinjilishaji mpya hakuna shaka kuwa wana jukumu la kusisimua. Ni muhimu kwamba Mwongozo huu chini ya  mtazamo wa kitaalimungu -kichungaji, unathibitisha tena mahali pa harakati za kanisa katika makanisa maalum na baadaye  kushiriki mazungumzo na ulimwengu. Harakati hizo zinafanywa na watu walei na katika umwengu unawasubiri wao kushuhudia Injili hata kwa njia ya mafunzo ya kielimu  ya kupyaisha yanayohusishwa na karama nyingi zilizowekwa na Roho Mtakatifu.

29 June 2020, 10:53