Tafuta

Vatican News
2020.06.25 Mkutano wa vyombo vya habari kuwasilisha Mwongozo mpya wa Katekesi 2020.06.25 Mkutano wa vyombo vya habari kuwasilisha Mwongozo mpya wa Katekesi  

Ask.Mkuu Fisichella:Katekesi ni tangazo la kwanza la Kristo kwa watu wote na hali zao!

Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya uhamasishaji wa Unjilishaji Mpya Askofu Mkuu Rino Fisichella,katika uwasilishaji kuhusu Mwongozo Mpya wa Katekesi anasema lengo siyo la kisakramenti bali ni kuingiza maisha kwa ujula katika jumuiya ya kikristo.Hii ni kwamba katekesi inafanyika hata katika magereza,wahamiaji na watu walemavu.Katekesi inaingia katika ulimwengu wa kidigitali na hata katika ulimwengu wa utandawazi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni hatua muhimu katika mwendelezo wa safari ya Katekesi mara baada ya Mtaguso ili kuweza kujibu changamoto za utamaduni wa kidigitali na utandawazi wa utumaduni. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Rino Fisichella, ambaye amewakilisha kwa vyombo vya habari kuhusu Mwongozo mpya wa Katekesi uliokubaliwa na Papa Francisko amethibitishwa kwamba mwendelezo huo unataka kusisitiza kuwa katekesi inakumbatia maisha yote ya kila mbatizwa pamoja na kukutano na Bwana na kushiriki fumbo lake katika maisha yetu yote. Mambo mapya yaliyomo katika hati hiyo, mpya ni kusititizia kwamba katekesi haifanyiki kwa sababu ya kupokea sakramenti tu, bali ni kuingizwa hatua kwa hatua kwenye  mchakato wa maisha ya jumuiya ya kikristo na kuweza kutoa ushuhuda wetu wa dhati leo hii. Zaidi ya hayo, Askofu Mkuu Fisichella amebainisha katika kuonodoa ile hali ya  katekesi kutoka kila mtindo na njia za kishule, kama ilivyo kuwa kwamba  kuna vyumba vya madarasa na vitabu vya shule, kuna vyumba vya madarasa na maandishi ya katekisimu, kumbe  si hivyo. Kwa maana hii ndiyo sababu katekesi hii inakwenda hata katika magereza, inakutana na wahamiaji, inakumbatia watu wenye ulemavu na wadhaifu zaidi ili pasiwepo mtu yoyote anayebaki peke yake katika safari yake ya imani,

Hata hvyo kwa maelezo zaidi Askofu Mkuu Fisichella amesema kwa kuzingatia mambo mawili pamoja ya uinjilishaji na katekesi ni kwamba katika hatua  msingi ambayo inastahili katika Mwongozo Mpya ni ile hatua ya kina inayounganisha Katekesi na uinjilishaji, mambo mawili ambayo yanakuwa tangazo la kwanza la Kristo kuwa nguvu ya katekesi iliyopyaishwa. Mwongozo wa mwisho ulikuwa umetangazwa kunako mwaka 1997. Kwa maana hiyo miaka zaidi ya ishirini sasa Askofu Mkuu Fisichella amesema wanawakilisha Mwongozo mpya kwa ajili ya katekesi  kama  jaribio la kuweka zaidi awamu mpya ambayo ina utamaduni wa ulimwengu tunaoishi. Katika utamaduni wa kidijitali mahali ambamo nafasi na wakati hupita kwa haraka sana,  kwa maana hiyo hitaji pia la kuwa na mawasiliano ya  mara moja na tamaduni ya vijana wa  na wale ambao kwa sasa ni wazaliwa wa kidigitali na kwa  upande wao wamekuwa na hitaji la vitendo vya ufundishaji na mafunzo ambavyo vinaendana na hali hiyo amesisistiza Askofu Mkuu Fisichella. Aidha Askofu Fischella amebainisha kwamba katika Mwongozo mpya umeweka mwanga kwa kile ambacho Papa Francisko alipendelea kukiacha kwenye Wosia wa “Evangelii gaudium”, yaani Injili ya furaha ‘kuhusu suala la katekesi. Utambuzi wake ulikuwa ni wa kupenda katekesi ya tangazo (kerygmatic) liwe hitaji la kuweka pamoja Unjilishaji na katekesi. Katekesi ni hatua ya uinjilishaji na siyo njia mbadala ya uinjilishaji. Lakini ndani ya mchakato huo mkubwa unakua kwa pande kadhaa, kuanzia liturujia, hadi  ushuhuda wa upendo, kutoka katika  sala binafsi kufikia katika ukuaji wa kimaadili  kwa maana hiyo katekesi inakusudia kufanya tangazo la kwanza la Yesu Kristo  katika nguvu yake.

Swali kwa Askofu Mkuu kuhusu alivyoandika utangulizi wake kwamba, Mwongozo ni zana ya upendeleo ambayo haina madai ya ukamilifu na inategemea mchango wa wengi amethibitisha,  awali ya yote mwongozo  mpya unawasilishwa kwa njia ya kimfumo sana. Kuna sehemu kadhaa ambazo zinajaribu kuonyesha maendeleo ya utaratibu wa katekesi. Kuna sehemu ya kwanza inayowasilisha msingi wa kitaalimungu. Katekesi ni mchakato wa uinjilishaji na Kanisa ni sehemu ya mchakato huo wa kurirhisha kutoka kizazi hadi kizazi. Kwa njia hii katekesi inaturudisha katika wakati ule muhimu wa maisha ya Kanisa pia iliyokumbukwa hata mwanzoni mwa  Injili ya Luka, wakati anasema kwamba anakusudia kuwasilisha kwa Theophilo, ambaye alikuwa  tayari  amebatizwa, msaada wa nguvu ya kihistoria ya utafiti alioufanya juu ya Yesu na anatumia kitenzi cha katechein, yaani kufanya katekesi. Injili kwa maana hiyo inakuwa, pamoja na tangazo lake, katekesi kwa waliobatizwa. Pia kuna sehemu ambazo zinawasilisha, kidogo kidogo, kuelewa zaidi na zaidi jukumu la katekesi. Katika nafasi ya kwanza, asili ya katekesi na jukumu la katekista, malezi ambayo anapaswa kuwa nayo katekista, bila kusahau kwamba Askofu ndiye katekista wa kwanza. Baadaye ni kuongezea ili  kufikia familia zetu na hali zote hizo ambazo zinajumuisha ufahamu wa fumbo la Yesu Kristo.

Hatupaswi kusahau, kwa namna ya pekee kuwa maaskofu, ambao ndiyo watu wa kwanza wanaolekezwa Mwongozo ili kujua kazi yao ni nini. Kutoka katika katekesi ya Cyril wa Alexandria hadi kufikia katekesi ya Ambrosio; kutoka ile ya Agostino hadi ile ya Ruffino wa Aquileia, ketekesi zilikuwa ni kazi maalum ambayo maaskofu daima waliielewa kuwa ni kwa ajili yao. Katika mwanga huu, Mwongozo unakabidhi hata sura nyingine muhimu kuhusu ufundishaji, juu ya mwelekeo  mafunzo hasa  juu ya utambuzi wa hali nyingi ambazo ni mpya katika utamaduni huu wa ulimwenguwa wa leo ambazo zinawajibisha daima Kanisa kuwa karibu.

Aidha amesema kwamba kutoka Mtaguso hadi leo hii kwa maana ya miaka 50 iliyopita  hawajasahahu hata Wosia wa Kitume wa  “Catechesi tradendae wa Yohane Paulo II kwa maaskofu, wacleri na waamini wote wa Mungu (16 Oktoba 1979) na Miongozo mingine miwili  iliyotangulia, ni mwendelezo, ni nguvu, ni jaribio la kufanya hali hii ichukue hatua zaidi. Kuna melekezo mengi katika Mwongozo ambayo yanatakiwa kufuatwa. Awali ya yote ile ya kufanya kila iwezekanavyo ili katekesi isifikiriwe kama ni hali halisi inayowahusu watoto au vijana tu. Katekesi inakumbatia maisha yote ya kila mbatizwa na kila mwaamini , na kwa kuwa katekesi ni kama mkutano na Bwana na ushiriki wa fumbo lake katika maisha yetu binafsi, inahitaji hata jitihada za utamaduni wa kina ambao sisi tunakiri na tunaamini. Baada ya mkutano na Bwana na kukutana na katekesi kunakuwa na shauku ya kutaka kujua zaidi na zaidi na kwa maana hiyo inahusu watu wote na kama njia nyingi za maisha binafsi.

Hata  hivyo amaebainisha kwamba suala la katekesi ndiyo lipo  kwa watoto na vijana, watoto na watu wazima, kwa ajili ya familia, wahamiaji na wale ambao wako katika magereza na pia kwa wazee. Kutokana na hili hakuna lolote linaweza kuondolewa katika shauku ya kumjua vema Bwana. Baadaye kuna jaribio la kufanya katekesi iweze kutoka  nje kwenye ufinyu wa mazoea ya kupokea sakramenti.  Haifanyiki katekesi kwa ajili ya kupokea sakramenti, lakini ni katika kuelewa vizuri mafumbo ya maisha yetu yaliyoingizwa katika fumbo la Kristo na, kwa hivyo, jinsi ya kuweka kila mmoja wetu na zawadi zake katika huduma ya Jumuiya ya Wakristo, ya Kanisa, ili Bwana aweze kutangazwa na kujulikana kwa watu wote. Na hatimaye kuondoa tabia ya katekesi katika kioto cha ukawaida wa shule kwa kufanya unjilishaji ulio fungamani kwa kila mmoja.

25 June 2020, 14:45