Tafuta

Vatican News
Kanisa la Afrika Kanisa la Afrika  (Vatican Media)

Mwongozo mpya kwa ajili ya katekesi ili Injili iweze kuwa hai!

Baada ya Mwongozo wa Katekisimu kuu ya 1971 na Mwongozo wa Katekesi kuu ya 1997,leo umetangazwa Mwongozo mpya wa Katekesi,ulioandikwa na Baraza la Kipapa la Uhamaishaji wa Uinjilishaji mpya.Hati imekubaliwa na Papa Francisko tarehe 23 Machi 2020 katika kumbu kumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Turibio wa Mogrovejo ambaye katika karne ya XVI alitoa msukumo wa unjilishaji na katekesi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Umetolewa Mwongozo mpya wa ufafanuzi kwa ajili ya Katekesi ili kuifanya Injili iweze kuwa hai  daima na utamaduni wa makutano, ulioandikwa na Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Uinjilishi mpya na ambao una uhusiano mkubwa kati ya uinjilishaji na Katekesi. Ni chombo makini kati ya tangazo la kwanza na ukomavu wa imani, katika mwanga wa utamaduni wa kukutana. Uhusiano huu ni muhimu sana mbele ya changamoto mbili za Kanisa katika enzi ya kisasa na ambazo ni utamaduni wa kidijitali na utandawazi wa utamaduni. Mara baada ya Mwongozo wa ufundishaji kwa ujumla  wa Ketekisimu wa  1971 na Mwongozo mkuu wa katekesi  ya 1997 sasa tarehe 25 Juni 2020 unatolewa Mwongozo mpya ambao ulikubaliwa na Papa Francisko kunako tarehe 23 Machi 2020 katika kumbukumbu kiliturujia ya Mtakatifu Turibio wa Mogrovejo ambaye katika karne ya XVI alitoa msukumo mkubwa wa uinjilishaji na katekesi. Zaidi ya kurasa 3000 zilizogawanyika katika sehemu tatu na makala 12, maandishi yanakumbusha kuwa kila mbatizwa ni mtume mmisionari na anayetakiwa kujitahidi na kuwajibika ili kupata lugha mpya za kuweza kuwasilisha imani. Misingi mitatu ambayo inaweza kusaidia kufanya hivyo  ni ushuhuda, kwa sababu Kanisa halikui kwa upropaganda, bali kwa kuvutia; huruma, katekesi ya dhati ambayo inafanya kuaminika kwa tangazo la imani; mazungumzo, ambayo yana uhuru na ya bure yasiyo lazimisha lakini yanaanzia na upendo, katika kuchangia ujenzi wa amani. Kwa njia hiyp mwongozo unaeleza kwamba katekesi inasaidia wakristo kutoa maana kamili ya kuishi kwao.

Katekesi katika utume wa uinjilishaji wa Kanisa

Katika sehemu yake ya kwanza yenye mada ya  “ Katekesi katika utume wa uinjilishaji wa Kanisa, maandiko yanajkita  kwa namna ya pekee juuy a mafundisho ya makatekisita. Na ili waweze kuwa mashuhuda waaminifu wa imani lazima “wawe katekisimu kabla ya kuwa katekista”. Kwa njia hii watatakiwa watenda bure, kujitoe, bure kuwa na uthabiti kwa mujibu wa roho ya kimisionari ambayo inazingatia kuwa mbali na uchungaji tasa usio zaa matunda, na ubinafsi. Walimu, wafundishaji, viongozi wasimamizi, mashuhuda, makatekista lazima  wasindikize kwa unyenyekevu na heshima ya uhuru wa mwingine. Na wakati huo huo, lazima kuzingatia kwa uamuzi kwa sababu kila mtu ahakikishiwe kwa namna ya pekee wadogo na watu wathirika, ulinzi wa dhati  na kila aina ya manyanyaso. Makatekista aidha wamealikwa kuwa na mtindo wa umoja na wawe wabunifu katika matumizi ya zana na lugha.

Mchakato wa katekesi:umuhimu wa familia

Sehemu ya pili ya mwongozo yenye mada ya “mchakato wa katekesi” kinyume chake inajikita katika kufafanua zaidi juu ya umuhimu wa familia. Familia ni kitu hai kinachofaa unjilishaji na mahali asili  ya kuishi imani kwa namna rahisi ambamo kwayo inatoa elimu ya kikristo. Familia inatoa ushuhuda zaidi wa kufundisha kwa njia ya mtindo wa unyenyekevu na ufahamu. Mbele ya hali halisi zisizo za kawaida ya majanga ya kifamilia yaliyopo katika jamii ya sasa, Kanisa linaitwa kusindikiza familia katika imani kwa ukaribu, kusikiliza na kuelewa ili kuwarudishia wote imani na matumaini.  Ujumuishwaji, kukaribisha na utumbuzi ni ufunguo wa maneno ya katekesi hata mbele ya walemavu. Mashuhuda wa kweli wa maisha ya binadamu, wanapaswa wakaribishwe kama zawadi kubwa, wakati  hu huo familia zao zinastahili kuheshimiwa na  kushangaza.

Jambo jingine kwa namna ya pekee ambalo linajionesha katika mwongozo huu ni la wahamiaji ambao wakiwa mbali na nchi zao, wanaweza kukumbana na mgogoro wa imani. Hata kwa ajili yao, katekesi inapaswa izingatie juu ya kukarimu, imani na mshikamano ili watu hao waweze kusaidiwa katika mapambano dhidi ya hukumu na hatari mbaya ambazo wanaweza kukutana nazo, kama vile biashara mbaya ya binadamu. Mwongozo huu pia unatazama magereza kama “eneo la kweli la utume. Kwa ajili ya wafungwa Katekesi itatakiwa kutangaza wokovu wa Kristo na kusikiliza kwa huruma na kuonyesha uso wa mama Kanisa. Chaguo la upendeleo kwa maskini pia ni la msingi. Katika muktadha huu, katekesi italazimika kuelimisha juu ya umaskini wa kiinjili, kuhamasisha utamaduni wa udugu na kukuza uelewa zaidi kwa waamini ile hali halisi ya shida na ukosefu wa haki

Katekesi katika makanisa mahalia: kutoka nje kuelekea uzoefu wa watu

Katika sehemu ya tatu ya Hati Mwongozo huo inajikita kwenye mada ya “Katekesi katika Makanisa maalum,ambapo  inaonesha bayana nafasi ya maparokia, kwa kutajwa kuwa ni mfano wa utume wa kijumuiya na wenye uwezo wa katekesi bunifu inayotoka nje kuelekea kwenye uzoefu wa watu. Na kwa upande wa mashule katoliki, Mwongozo unashauri kutoka katika mfumo wa shule kitaasisi kwenda katika mfumo wa shule ya jumuiya ya imani inayojikita katika mafundisho ya dini ambayo yanatofautisha, lakini inakilishwa na katekesi yenyewe. Muktadha wa kidini ni mwelekeo wa uwepo na ambao haupaswi kupuuzwa kwa mujibu wa  Mwongozo na kwa njia hiyo ni hali ya mzazi na wanafunzi kupokea mafunzo kamili ambayo yanazingatia hata mafundisho ya dini. Sekta maalum  kwa ajili ya katekesi pia ni ile ya uekumene na mazungumzo ya kidini na ulimwengu wa kiyahudi na kiislam. Kwa mtazamo wa kwanza, Mwongozo unasisitiza jinsi ya katekesi inavyopaswa kuchochea shauku ya umoja kati ya wakristo kuwa chombo aminifu cha uinjilishaji. Kwa upande wa Wayahudi, wanaalikwa katika mazungumzo ambayo yanapingana na chuki dhidi ya  wayahudi na kuhamasisha amani na haki. Na wakati wanakabiliwa na misingi ya vurugu ambayo wakati mwingine inaweza kupatikana hata katika dini ya Uislam, Kanisa linashuri kuzuia kizazi cha kijuu juu, ili kukuza ufahamu na kukutana na waislamu.

Mantiki ya dini nyingi na ulimwengu wa kidijitali

Kwa upande mwingine, katika mantiki ya wingi wa dini, katekesi inapaswa ijikite kwa kina na kuongeza nguvu ya utambulisho kwa waamini  katika kuwahamasisha kuwa na mwamko wa kimisionari kwa njia ya ushuhuda na mazungumzo aminifu na maelewano. Takafakari ya mwongozo aidha inaelekeza juu ya utamaduni wa kidijitali ambao leo hii  unajulikana kama “asili”, kiasi kwamba umebadilisha lugha na mfumo wa maadili kwa ngazi ya ya ulimwengu. Utajiri kwa mantiki chanya (kwa mfano, unatajirisha uwezo wa kuelewa na kukuza mawasiliano hasa habari inayojitegemea ili kuwalinda watu walio hatarini zaidi) na wakati huo huo ulimwengu wa kidigitali una “unayo sehemu nyeusi”.  Inawezekana kupelekea upweke, udanganyifu, vurugu, chochezi, upekuzi, hukumu na chuki. Bila kusahau tabia karibu za kutoaminiana ambazo kwa mfano katika mantiki ya injini ya utatifi. Katika sekta hii, katekesi lazima ielimishe kupinga utamaduni wa kitambo, usiokuwa na herakia ya maadili, na kukosa kutofautisha ukweli na ubora. Vijana hasa watatakiwa kusindikizwa katika utafiti wa uhuru wa ndani ambao utawasaidia kujitofautisha kutoka katika zizi la mtandao wa kijamii. Changamoto ya uinjilishaji inapelekea ile ya utamadunisho katika bara la kidigitali, kwa mujibu wa mwongozo na kwamba kuna umuhimu wa kutoa nafasi ya kufanya uzoefu wa imani ya dhati, ili  iweze kutoa mwelekezo wa kutafsiri mada zenye nguvu, kama vile za upendo, haki na amani.

Sayansi na teknolojia kwa ajili ya huduma ya mtu

Hati hiyo pia inazingatia sayansi na teknolojia. Mwongozo huu unathibitisha kuwa hayo yapo katika huduma ya mtu na yanapaswa yaelekezwe kwa ajili ya kuboresha hali za maisha ya familia ya binadamu. Hati hiyo ya mwingozo inatoa ushauri wa kuona migogoro iliyowazi kati ya sayansi na imani na kuthamanisha ushuhuda wa sayansi ya kikristo, kwa mfano wa maelewano na muundo kati ya hizo mbili. Tafakari tofauti, hata hivyo, vinapaswa kufanywa katika sehemu ya elimu vya viumbe na wanyama kuanzia kwa dhana kwamba “sio kila kitu kinachowezekana kitaalam kinakubalika kimaadili. Kwa maana hiyo  itakuwa muhimu kutofautisha kati ya uingiliaji wa matibabu na ujanja na  kuwa makini juu ya hilo na ubaguzi unaotoka ndani mwake.  Aidha  kuhusu suala la kile kiitwacho “jinsia” Hati ya mwongozo  huo inakumbusha kuwa Kanisa linasindikiza kila wakati kila hali yoyote, bila kuhukumu, watu ambao wanaish hali ngumu na ambayo wakati mwingine ni yenye utata. Licha ya hayo katika matarajio ya imani, suala  la ujinsia siyo suala la kimwili tu, lakini ni dhamana iliyokabidhiwa jukumu la mtu kutoa jibu la wito wa asili.

Heshima ya hadhi ya mtu katika maadili

Katika mantiki ya uchunguzi maalum wa matatizo ya kiadili na maadili katika uwanja wa matibabu na kibaiolojia kuhusiana na maisha ya mwanadamu au ya wanyama(bioethical), Mwongozo unabaini kuwa itahitaji makatekista kufanya mafunzo maalum ambayo yaanzie mwanzo wa utakatifu na kutokiukwa maisha ya mwanadamu na kupinga utamaduni wa kifo. Kutokana na pendekezo hilo Mwongozo unalaani adhabu ya kifo kwa kutaja ni” kipimo kisicho cha kibinadamu ambacho kinadharau hadhi ya mtu”. Katika ya mada nyingine zilizo kabiliwa katika hati hiyo, ni mwaliko wa uongofu wa kina wa kiekolojia, wa kuhamasisha kwa njia ya katekesi umakini juu ya utunzaji wa kazi ya uumbaji na msukumo wa maisha ya fadhila  mbali na juu ya  matumizi ya hovyo.  Vile vile jitihada za kijamii zilizo hai katoliki zimetiwa moyo mkuu ili ziweze kuendelea kutenda zaidi kwa ajili ya wema wa pamoja.  Katika mtazamo  wa kazi, wanashuri Unjilishaji kwa mujibu wa Mafundisho Jamii ya Kanisa na kwa namna ya pekee umakini zaidi katika kutetea haki za walio wadhaifu zaidi. Hatimaye Sura mbili za mwisho wa Mwongozo zinajikita juu ya Katekisimu mahalia, kuhusiana  na maelekezo kwa ajili ya kukubaliwa na Makao Makuu ya Kitume na juu ya mihimili ya huduma ya katekesi, kati ya hizo ni Sinodi ya Maaskofu na Mabaraza ya Maaskofu.

25 June 2020, 11:30