Tafuta

Mgogoro kati ya Israel na Palestina unaendelea. Mgogoro kati ya Israel na Palestina unaendelea.  (AFP or licensors) Tahariri

Hapana vita bali kuwa na ukaribu kwa waathirika wote

Kwa zaidi ya karne moja Mapapa wameeleza kukataa kwao vita.Na katika uso wa migogoro,Vatican haijawahi kuegemea upande wowote wala usawa.Badala yake Vatican daima imejaribu kuwa karibu na waathirika wasio na hatia,kwa wale wanaoteseka na kulipa matokeo ya vurugu katika pande zote mbili.

ANDREA TORNIELLI 

Kwa zaidi ya karne moja Vatican ikiwa na msururu wa matamko yaliyoamuliwa na kuongezeka kwa vitisho vya vita na matumizi ya silaha zinazozidi kuwa za kisasa na haribifu, imekuwa ikitangaza kwa nguvu zote "hapana" yake kwa vita. Tangu mwito wa kinabii wa Papa Benedikto XV, dhidhi ya mauaji yasiyostahili ya Vita kubwa hadi maneno yaliyosema kwa kila fursa na Papa Francisko kuhusu vita kama kushindwa kwa ubinadamu, mafundisho ya Maaskofu wa Roma yameweka bayana na kwa kina kwamba hakuna "vita vya haki" na kwamba haki ya kujilinda lazima pia iwe sawa, kama Katekisimu ya Kanisa Katoliki inavyofundisha... Tangu mwanzo wa vita vya uchokozi vilivyofanywa na Urussi dhidi ya Ukraine na tena katika majuma machache yaliyopita baada ya shambulio lisilo la kibinadamu la Hamas, kwa ukatili waliofanyiwa raia wa Israel na kisha uvamizi wa jeshi la Israel lililobomoa nyumba nyingi huko Gaza na kuua maelfu ya watu, kwa Wapalestina wasio na hatia, ukosoaji umekuzwa dhidi ya mtazamo wa Papa na Kiti kitakatifu. Ni mtazamo ambao kwa muda mrefu sasa umekosoa na kwa wengine kuwa kama"usio na upande wowote", kana kwamba karibu huku Vatican, kwa sababu ya kupitia kiasi kikubwa kwa njia ya diplomasia, haikuweza kutathmini haki na makosa ya pande zinazozozana.

https://www.vaticannews.va/sw/pope/news/2023-11/papa-atoa-wito-kwa-ajili-ya-myanmar-palestina-israel-na-ukraine.html

Kwa hivyo inafaa kukumbuka,  kwa mara nyingine tena,  kwamba Vatican haijawahi "kuegemea upande wowote" au kuwa "sawa" katika uso wa vita. Kinyume chake, imejaribu kila wakati kutokuwa na upendeleo, ambapo ni kutohusika au kuonekana kuhusika katika mzozo huo na wakati huo huo "kwa usawa", ambao na sio karibu na wale wanaosababisha vita, badala yake kuwa karibu kwa wale wanaoteseka, kwa  wale wanaolipa matokeo ya migogoro, kwa raia waliouawa, waliojeruhiwa, mama na baba wa askari waliokufa, waathiriwa wasio na hatia wa ugaidi na kulipiza kisasi. Vyombo vya habari vya Vatican haviwezi kujizuia kufuata mstari huu wa uhariri, vikikataa ubaguzi huo ambao unaonekana kuwa kipengele cha kutilia maanani,  si tu cha vita vinavyoendelea bali pia kwa ujumla zaidi katika ulimwengu ambao tunajikuta tunaishi leo hii.https://www.vaticannews.va/sw/pope/news/2019-11/mkataba-kimataifa-geneva-1949-haki-wafungwa-kivita-kimataifa.html,

Kuweka njia za mazungumzo wazi na kila mtu, kamwe isifunge milango kwa matumaini ya kufikia usitishaji mapigano na kisha mazungumzo ya amani ya haki, wasiwasi juu ya waathiriwa wasio na hatia kwa upande wowote ule walioko, ni tafakari juu ya sababu za mbali au kidogo za migogoro, kuepuka kutumia lugha za chuki na uzushi, haimaanishi kabisa kupuuza ukweli kwamba kuna mchokozi na mtu kushambuliwa, wala hata kupuuza uhalali wa kujilinda. Kinyume chake, ina maana ya kuwa na hatima ya watu wasio na hatia moyoni, kutozima nuru kamwe  inayobubujika tumaini la amani, na kushika kila ishara ndogo ya uwazi popote inapotokea, kuamini diplomasia na juu ya yote kuhangaikia hatima ya waathiriwa, vilema na waliohamishwa. Pia ina maana ya kuondoka kutoka katika mantiki ya ubaguzi na kufikiri ushirikishwaji pamoja. https://www.vaticannews.va/it/papa/news/2023-11/papa-francesco-post-x-bambini-giornata-diritti-infanzia.html

Je, inawezekana kulaani shambulio la kigaidi lisilo la kibinadamu la Hamas dhidi ya raia wa Israel na wakati huo huo kuibua shaka na maswali kuhusu jibu la silaha za Jeshi la Tel Aviv kwa idadi kubwa ya wahanga wa raia waliosababishwa na maafa ya kibinadamu huko Gaza? Kuna migogoro ambayo ushangiliaji haufai kabisa na ule unaoendelea Mashariki ya Kati kwa hakika ni miongoni mwake, unaotokana na hali ngumu sana ambapo majukumu ya wengine yanaongeza yale ya wengine na hayawahalalishi. https://www.vaticannews.va/sw/vatican-city/news/2023-11/neema-ya-ubatizo-utamaduni-na-desturi-za-mipaka-ya-kikasisi.html

Katika kujaribu kuzungumza juu ya vita vinavyoendelea na kutoa tafakari ya  mawazo, taa yetu inawakilishwa na maneno ya kinabii ya Mrithi wa sasa wa Mtakatifu Petro, ambaye anaendelea kuwaonya wanadamu wote dhidi ya hatari ya vita vya kimataifa na uharibifu wa kibinafsi. Tunajaribu kufanya uandishi wa habari kwa kutenganisha ukweli kutoka katika maoni, na maoni yetu kutoka kwa wengine. Mwisho wake, kuripoti na  kutoa sauti kwa watu ambao wanaonekana kuvutia kwetu, haimaanishi kuwashirikisha. Badala yake, inamaanisha kujaribu kuelewa kwa kuthamini sauti muhimu zaidi na zisizo za kiitikadi. https://www.vaticannews.va/it/chiesa/news/2023-10/editoriale-andrea-tornielli-sinodo-sinodalita.html

20 November 2023, 18:08