Tafuta

Ubatizo wa Watoto katika Kikanisa cha Sistina, Vatican. Ubatizo wa Watoto katika Kikanisa cha Sistina, Vatican.  Tahariri

Neema ya ubatizo,utamaduni na desturi za mipaka ya kikasisi

Tunachapisha tahariri ya Mwariri wetu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican,Dk.Andrea Tornielli kuhusu tafakari ya jibu la Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa,kuhusiana na maadhimisho ya Sakramenti ya Ubatizo kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na watu wa jinsia moja.

ANDREA TORNIELLI

Mtakatifu Cyprian, Askofu wa Carthage aliyeuawa mnamo mwaka 258, akishiriki katika sinodi ya maaskofu wa Kiafrika, alisema: "Huwezi kukatalia  huruma na neema ya Mungu kwa mtu yeyote anayekuja kuwepo kwake". Na Mtakatifu Agostino aliandika: "Watoto wanawasilishwa ili kupokea neema ya kiroho, sio sana kutoka kwa wale wanaowabeba mikononi mwao (ingawa pia kutoka kwao, ikiwa ni waamini wazuri), lakini kutoka kwa jamii ya ulimwengu ya watakatifu na waaminifu ... Ni Kanisa zima la Watakatifu linalofanya kazi, kwa kuwa katika ukamilifu wake huzalisha kila mmoja.” Hizi ni kauli mbili kutoka kwa Mababa wa Kanisa ambazo zinathibitisha kabisa  ubatizo wa bure, pia zinahusiana kwa namna fulani jukumu la wazazi na wasimamizi wao ("ikiwa ni waamini wazuri") wanaoomba sakramenti na kuwasilisha mtoto.

Haya ni maneno ambayo ni bora kuliko mengine yanayoakisi majibu ya hivi karibuni ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kwa maswali kutoka kwa  Askofu wa Brazil kuhusu ubatizo. Barua iliyotiwa saini na Kadinali Victor Manuel Fernandéz na kuidhinishwa na Papa Francisko inaonesha maelewano wazi na mafundisho ya hivi karibuni ya Papa. Kwa hakika, Papa Fransisko alisisitiza mara kadhaa juu ya ukweli kwamba mlango wa sakramenti, na hasa ule wa ubatizo, haupaswi kubaki umefungwa, na kwamba Kanisa lisijibadilishe na kuwa nyumba ya forodha, badala yake linapaswa kuwakaribisha na kuwasindikiza  kila mtu katika mchakato wa safari zao ngumu za maisha. Majibu ya Baraza la  Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, katika mazingira yenye mgawanyiko mkubwa sana  na ambayo  leo hii yanagandisha Kanisa , yamechochea hisia tofauti, na kati ya hizo tunapaswa kukumbuka ile ya wale wanaoogopa kwamba, kwa kukubali sakramenti ya ubatizo wa watoto wa wapenzi wa jinsia moja (adopted childrenyaani watoto wa kuasili au watoto wa mmoja wa wenzi wawili labda waliozaliwa kupitia uzazi mbadala), hufanywa kuwa halali wote wanaoitwa kutoka "ndoa za mashoga" na mazoezi ya kinachojulikana kama "tumbo la kukodi."

Kwa maana hii, wakosoaji wanapaswa pia kusoma kupunguzwa umarufuku wa kuwa Wasimamizi wakati wa ubatizo, ambapo Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa linawasilisha kwa mtindo wa shida. Inastaajabisha kwanza kabisa kutambua kifungu katika barua, mahali ambapo kinatukumbusha kwamba majibu yaliyochapishwa katika siku za hivi karibuni "yanapendekeza, kwa upya kimsingi, yaliyomo ya msingi ya yale ambayo tayari yalisemwa hapo awali juu ya mada hii na Baraza." Kwa kurejea ni matamko ya awali ambayo yalibaki kuwa siri (moja ya hayo pia ilitajwa katika maandishi) ambayo yanaanzia wakati huu wa papa na kwa watangulizi wake. Zaidi ya hayo, nukuu za mwanzo kabisa kutoka kwa Mababa wawili wa Kanisa waliopendekeza mwanzoni mwa makala hii zimo, pamoja na nyingine nyingi, katika hati ya umma ya wakati ule wa Baraza la Kipapa la Mafundisho ya imani, wakati huo likiongozwa na Kardinali Franjo Šeper wa Kroatia na Askofu Mkuu Jérôme Hamer wa Dominika.


Haya ni maagizo yaliyoidhinishwa mnamo Oktoba 1980 na Mtakatifu Yohane Paulo II ambapo yanajibu mfululizo wa pingamizi dhidi ya kuadhimisha ubatizo wa watoto wadogo, akisisitiza umuhimu wa "mazoea ya kale" ya asili ya kitume ambayo hayajaachwa. Kwa wale ambao leo hii wangependa kukataa ubatizo kwa watoto wa wapenzi wa jinsia moja kwa sababu kwa kuwabatiza Kanisa lingefanya muungano wa mashoga au mazoezi ya kukodisha matumbo ya uzazi  kuwa halali kiadili, hati ya 1980 ilikuwa tayari imejibu kwa njia isiyo ya moja kwa moja, ikisema kwamba " hatua za zoea la ubatizo wa watoto ni wa kweli wa kiinjili, kwa kuwa una thamani ya ushuhuda; kwa hakika, unadhihirisha mpango wa Mungu kwetu na  wa upendo wake unaozunguka maisha yetu yote: “Si sisi tuliompenda Mungu, bali yeye ndiye aliyetupenda... Sisi twampenda, kwa sababu yeye alitupenda sisi kwanza” (1Yh 4, 10. 19.)" Na pia “kwa watu wazima, mahitaji yanayohusiana na kupokea ubatizo hayapaswi kutufanya tusahau kwamba Mungu "alituokoa si kwa matendo ya haki tuliyofanya, bali kwa huruma yake kwa kuoshwa ili kuzaliwa upya na kufanywa upya katika Roho Mtakatifu”(Tt. 3, 5.)”

Maagizo yaliyoidhinishwa na Papa Wojtyla miaka arobaini na mitatu iliyopita bila shaka yalizingatia mabadiliko ya muktadha wa kijamii na ya kutokuwa na dini: "Inaweza kutokea kwamba wazazi ambao hawaamini imani na kutenda mara kwa mara, au hata wasio Wakristo, wanageukia mapadre wa parokia , ambao kwa sababu zinazostahili kufikiriwa huomba ubatizo kwa ajili ya mtoto wao.” Je ni jinsi gani ya kutenda katika kesi hizi? Ingawa kigezo - cha jana na leo - kinabakia kuwa halali kwamba ubatizo wa watoto unaadhimishwa ikiwa kuna ahadi ya kuwaelimisha katika njia ya Kikristo, waraka wa 1980 ulibainisha katika suala hili kuwa: "Kuhusiana na dhamana, lazima izingatiwe kwamba dhamana yoyote inayotoa tumaini lenye msingi mzuri kuhusu elimu ya Kikristo ya watoto inastahili kuhukumiwa vya kutosha." Mazoezi yanayotumika maparokiani yanathibitisha kwamba, kwa kufuata mfano wa Mnazareti, bila kuchoka katika kutafuta kila kondoo aliyepotea, inatosha kuwepo ndugu ambaye anaaapa mbele ya Kanisa kutofunga mlango.

Je, kusingekuwa na haja leo hii ya kuamini zaidi tendo la neema linalotenda kazi kupitia sakramenti ambazo si thawabu kwa walio kamili bali ni dawa kwa wenye dhambi? Je! hatupaswi pengine kutazama zaidi kurasa za kiinjili ambamo Yesu anatoka ambaye anapenda kwanza, anayesamehe kwanza, anakumbatia huruma kwanza na ni ndani ya kumbatio hilo ambapo mioyo ya watu inasonga kuelekea uwongofu? Na tena, je watoto wana kosa gani? Kwa vyovyote vile walivyokuja ulimwenguni, wao daima ni viumbe waliopendelewa na kupendwa na Mungu. Kwa hiyo haingefaa kukazia zaidi ukweli chanya, yaani ukweli kwamba ubatizo unaoombwa katika mazingira ya baada ya Ukristo, ambapo unazidi kuwa nadra, kwani haya yanatokea kwa desturi tu?

Inafariji kusoma tena maneno ambayo Askofu mkuu wa karne ya ishirini alitamka katika mahojiano mnamo Julai 1978 kuhusu Luise Brown, mtoto wa kwanza aliyezaliwa kwa majaribu ya bomba. Alishutumu hatari kwamba "viwanda vya watoto" vinaweza kutokea tofauti na muktadha wa familia na akaelezea juu ya kukubali kwa upande tu,  wa  shauku ya jaribio hilo. Lakini mwishowe alielezea kuwa "matakwa ya joto zaidi kwa mtoto mdogo yanastahili" na wazo la upendo kwa wazazi, akisema: "Sina haki ya kuwahukumu: kibinafsi, ikiwa walifanya kazi kwa nia sahihi na kwa nia njema, wao wanaweza hata kuwa na sifa kubwa mbele ya Mungu kwa kile walichoamua na kuwataka madaktari kutekeleza." Askofu huyo aliitwa Albino Luciani, alikuwa Patriaki wa Venezia, mwezi mmoja baadaye akawa  Yohane Paulo I na leo hii ni mwenyeheri.

Kwa maelezo zaidi fungua Hati iliyotolewa na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kuhusu kile ambacho kimefafanuliwa katika tahariri hii:https://www.vatican.va/roman_curia/congregations/cfaith/doc_doc_index_it.htm

Nota
11 November 2023, 11:26