Tafuta

Tukio kuu la Jukwaa la Chakula Duniani (WFF)  linalofanyika kuaniza 16-20 Oktoba 2023 jijini Roma lina washiriki hata vijana kutoka Tanzania. Tukio kuu la Jukwaa la Chakula Duniani (WFF) linalofanyika kuaniza 16-20 Oktoba 2023 jijini Roma lina washiriki hata vijana kutoka Tanzania. 

Vijana watanzania washiriki Jukwaa la Kimataifa la Chakula(WFF)jijini Roma

Vijana wajasiliamali kutoka Tanzania wanashiriki Jukwaa la Chakula duniani(WFF)kuanzia Oktoba 16-20.Vatican News inakuletea mahojiano maalum Mkami Yusuph Tetere-Mbeya,Ray Peter Mark-Dodoma,Geophrey Tenganamba Dar Es Salama-Iringa hatimaye kijana Emmanuel Lucian Kisinda.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Tukio kuu la Jukwaa la Chakula Duniani (WFF) linajumuisha Jukwaa la Vijana Ulimwenguni la WFF, Jukwaa la Sayansi na Ubunifu la FAO na Jukwaa la Uwekezaji wa Kuunga Mikono na FAO. Majumuisho haya matatu yaliyounganishwa yanaleta pamoja suluhisho za kijasiri na zinazoweza kutekelezeka ili kuchochea mabadiliko ya mifumo yetu ya kilimo kulingana na changamoto na majanga ya sasa, zikimulika hasa  umuhimu wa ushirikiano kati ya kizazi cha sasa na kijacho na ujanja wao wa pamoja na ubunifu katika sayansi, teknolojia na uvumbuzi na uwekezaji katika maeneo muhimu ya kilimo na chakula.  Ni katika Muktadha huo, idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican inakuletea mahojiano maalum baada ya kutembelewa ndani ya Studio zetu Vatican News, na  vijana 4 kutoka Tanzania ambao wanashiriki kwa hakika Jukwaa la Chakula Duniani, wakiungana na wengine kutoka pembe za dunia ambalo lilifunguliwa mnamo tarehe 16 Oktoba na litahitimishwa tarehe 20 Oktoba 2023.

Vijana wetu wajasiriamali wakiwa ndani ya Studio za Vatican News
Vijana wetu wajasiriamali wakiwa ndani ya Studio za Vatican News

Vijana hawa  wajasiriamali wanne kutoka Tanzania ni Mkami Yusuph Tetere kutoka Mbeya ambaye ni kijana msichana mjasiriamali anayejikita na kampuni inayoitwa, ‘MKAMI T LIMITED,’ na  ambaye anasambaza bidhaa za viungo vya chakula; kijana Ray Peter Mark kutoka Dodoma MKULIMA na Shirika linaloitwa ‘THE YOUNGER WORD FEEDERS’, mkulima wa mboga mboga na ufugani wa wa samaki katika mabawa na mengine; Geophrey Tenganamba ambaye anaendesha ujasiriamali Dar Es - Salam na Iringa kwa kampuni inayoitwa ‘MAZAO HUB.’ Shirika la kitekonolojia ambalo kwa kiasi fulani ni muhimu sana kuingiza mifumo ya kidijitali katika maishamba na hatimaye kijana Emmanuel Lucian Kisinda, anayejishughulisha na kampuni inayoitwa ‘KIKOMBO AVOCADO FARM’, ambalo linajieleza lenyewe.

Vijana wa rika zote wanashiriki Jukwaa la Chakula duniani,Roma

Kwa njia hiyo kwa mwaka  2023, tukio kuu la Jukwa hii la Chakula duniani  WFF ambalo lilizinduliwa tangu  tarehe  16 katika Makao Makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) jijini Roma, Italia, ni la juma zima, ambalo linaendelea kuhamasisha mijadala na makongamano  miongoni mwa wadau husika, kuanzia barubaru  na vijana, wakulima, wazalishaji wadogo, watu wa Asili, watunga sera, wawekezaji wa kilimo na wanasayansi, kutoka pembe nne za dunia, wote wakiwa na lengo moja  la kuhamisha kutoka ufinyu kabisa kama wa sindano wa  uhakika wa chakula ili kufikia mustakabali bora  na mpana wa chakula kwa wote, bila kumwacha mtu  yeyote nyuma. Yafuatayo ni mahojiano ya vijana hawa:Mkami Yusuph Tetere, Ray Peter Mark, Geophrey Teganamba na Emmanuel Lucian Kisinda.

Mahojiano na Mkami Y.Tetere, Ray P.Mark,Geophrey Teganamba na Emmanuel L.Kisinda

 

19 October 2023, 16:32