Vijana watanzania washiriki Jukwaa la Kimataifa la Chakula(WFF)jijini Roma
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Tukio kuu la Jukwaa la Chakula Duniani (WFF) linajumuisha Jukwaa la Vijana Ulimwenguni la WFF, Jukwaa la Sayansi na Ubunifu la FAO na Jukwaa la Uwekezaji wa Kuunga Mikono na FAO. Majumuisho haya matatu yaliyounganishwa yanaleta pamoja suluhisho za kijasiri na zinazoweza kutekelezeka ili kuchochea mabadiliko ya mifumo yetu ya kilimo kulingana na changamoto na majanga ya sasa, zikimulika hasa umuhimu wa ushirikiano kati ya kizazi cha sasa na kijacho na ujanja wao wa pamoja na ubunifu katika sayansi, teknolojia na uvumbuzi na uwekezaji katika maeneo muhimu ya kilimo na chakula. Ni katika Muktadha huo, idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican inakuletea mahojiano maalum baada ya kutembelewa ndani ya Studio zetu Vatican News, na vijana 4 kutoka Tanzania ambao wanashiriki kwa hakika Jukwaa la Chakula Duniani, wakiungana na wengine kutoka pembe za dunia ambalo lilifunguliwa mnamo tarehe 16 Oktoba na litahitimishwa tarehe 20 Oktoba 2023.
Vijana hawa wajasiriamali wanne kutoka Tanzania ni Mkami Yusuph Tetere kutoka Mbeya ambaye ni kijana msichana mjasiriamali anayejikita na kampuni inayoitwa, ‘MKAMI T LIMITED,’ na ambaye anasambaza bidhaa za viungo vya chakula; kijana Ray Peter Mark kutoka Dodoma MKULIMA na Shirika linaloitwa ‘THE YOUNGER WORD FEEDERS’, mkulima wa mboga mboga na ufugani wa wa samaki katika mabawa na mengine; Geophrey Tenganamba ambaye anaendesha ujasiriamali Dar Es - Salam na Iringa kwa kampuni inayoitwa ‘MAZAO HUB.’ Shirika la kitekonolojia ambalo kwa kiasi fulani ni muhimu sana kuingiza mifumo ya kidijitali katika maishamba na hatimaye kijana Emmanuel Lucian Kisinda, anayejishughulisha na kampuni inayoitwa ‘KIKOMBO AVOCADO FARM’, ambalo linajieleza lenyewe.
Vijana wa rika zote wanashiriki Jukwaa la Chakula duniani,Roma
Kwa njia hiyo kwa mwaka 2023, tukio kuu la Jukwa hii la Chakula duniani WFF ambalo lilizinduliwa tangu tarehe 16 katika Makao Makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) jijini Roma, Italia, ni la juma zima, ambalo linaendelea kuhamasisha mijadala na makongamano miongoni mwa wadau husika, kuanzia barubaru na vijana, wakulima, wazalishaji wadogo, watu wa Asili, watunga sera, wawekezaji wa kilimo na wanasayansi, kutoka pembe nne za dunia, wote wakiwa na lengo moja la kuhamisha kutoka ufinyu kabisa kama wa sindano wa uhakika wa chakula ili kufikia mustakabali bora na mpana wa chakula kwa wote, bila kumwacha mtu yeyote nyuma. Yafuatayo ni mahojiano ya vijana hawa:Mkami Yusuph Tetere, Ray Peter Mark, Geophrey Teganamba na Emmanuel Lucian Kisinda.