Tafuta

Vatican News
2021.03.07 Ziara ya Papa Francisko:maombi kwa waathirika wa vita huko Mosul 2021.03.07 Ziara ya Papa Francisko:maombi kwa waathirika wa vita huko Mosul  (AFP or licensors)

Ziara ya Papa Francisko nchini Iraq ni ishara ya matumaini,unesco

Ziara ya Papa Francisko nchi Iraq kwa siku tatu tangu tarehe 5 Machi kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni(UNESCO)limabinisha kuwa ni ishara ya matumaini na fursa ya kuimarisha jitihada za amani na umoja nchini humo.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Tangu Papa Francisko kuanza ziara yake ya kitume nchini Iraq kwa siku tatu hadi tarehe 8 Machi, imepata maoni mengi na mitazamo mbali mbali kutoka sekta mbali mbali, wakuu wa mataifa na mashirika. Kwa mfano Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO  kufuatia na ziara hiyo linasema ni ishara ya matumaini na fursa ya kuimarisha jitihada za amani, na umoja nchini humo.

PAPA AKIWA ANELEKEA KUSALI KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA VITA HUKO MOSUL
PAPA AKIWA ANELEKEA KUSALI KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA VITA HUKO MOSUL

UNESCO kupitia taarifa yake imesisitiza “ziara ya Papa Francisko inakuja na ujumbe wa amani na umoja ikiungwa mkono na utofauti wa wairaq. Ujumbe huu uko katika mamlaka yetu kuu ya kuelewana, kuheshimiana na hatimaye kuwa na dunia yenye amani na haki.” Papa Francisko aliwasili Iraq siku ya Ijumaa tarehe 5 Machi ambapo  Jumamozi alikwenda mji wa kaskazini huko Mosul na mabpo siku ya Jumapili tarehe 7 Machi amesali  na waathirika wa mzozo unaliosababishwa na magaidi wa ISIL na uliosababaisha maelfu na maelfu ya watu. Kwa mujibu wa UNESCO inasema “Ziara ya Mosul inabeba ujumbe muhimu, mji ambao ni wa kale zaidi duniani na kituo cha kitamaduni na kidini, mji ambao umekumbwa na uharibifu mkubwa tangu magaidi wa ISIL wadhibiti mji huo kati yam waka 2014 hadi 2017”.

MAGOFU HUKO MOSUL YANAJIELEZA
MAGOFU HUKO MOSUL YANAJIELEZA

Jumuiya za Kikristo Iraq zimetambua mateso na ushahidi: Kwa wastani jumuiya za Kikristo za Iraq zimetambua na kujua  miaka ya kuuawa kishahidi kwa sababu ya vita na mateso, ambayo yamesukuma mamia ya maelfu ya Wairaq kuondoka katika nchi yao. Sasa, inaonekana ni nafasi ya kugeweza kugeuza ukurasa na kuchangia ujenzi wa jamii nzima. Ni mwanzo ambao siyo rahisi ambao unahitahi nguvu na umakini  wa kimataifa  Jitihada na msaada uliotolewa na mashirika ya Kanisa ya kimisaada kwa mujibu wa Bwana Alessandro Monteduro, mkurugenzi wa tawi shirika la Misaada la Italia kwa upande wa Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji ansema zimekuwa msingi wa kuruhusu jamii za Kikristo kuishi, hasa kaskazini mwa Iraq.

WASICHANA WAKIWA NA NGUO ZA KIUTAMADUNI HUKO MOSUL
WASICHANA WAKIWA NA NGUO ZA KIUTAMADUNI HUKO MOSUL

Jitihada za kifedha na shirika ambalo linatpekea kwenye kambi za mapokezi limepelekea familia zote za Kikristo zilizobaki kurudi kwenye nyumba za kweli. Bwana Monteduro ameongeza kusema kuwa: “Leo tunaweza kuwasalimia kwa furaha ukweli kwamba asilimia 45% ya Wakristo  ya wale elfu 120,000 ambao walilazimika kukimbia mnamo 2014 wamerudi katika vijiji vya Bonde la Ninawi, kwa namna hiyo sehemu pendwa ya utuamaduni wetu”.

PAPA AMEHUTUBIA KATIKA MJI WA ZAMANI HUKO MOSUL
PAPA AMEHUTUBIA KATIKA MJI WA ZAMANI HUKO MOSUL
07 March 2021, 13:12