Tafuta

Vatican News
2021.03.19 BI SAMIA SULUHU RAIS WA KWANZA MWANAMKE TANZANIA BAADA YA KIFO CHA MTANGUZLI WAKE DK MAGUFULI 2021.03.19 BI SAMIA SULUHU RAIS WA KWANZA MWANAMKE TANZANIA BAADA YA KIFO CHA MTANGUZLI WAKE DK MAGUFULI 

Bi Samia Suluhu ni mwanamke wa kwanza kuwa rais Tanzania

Bi Samia Suluhu Hassan aliyekuwa makamu wa rais wa Tanzania ameapishwa rasmi Ijumaa tarehe 19 Machi kuwa rais wa Tanzania, na mwanamke wa kwanza kushika hatamu hiyo

Na Sr. Angela Rwezala- Vatican.

Pamoja na majonzi makubwa, na mshangao nchini Tanzania kufuatia na kifo cha aliyekuwa  mpendwa wa nchi rais John Pombe Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi, jijini Dar Es Salaam, leo hii tarehe 19 Machi 2021, Bi Samia Suluhu Hassan mwenye umri wa miaka 61 na aliyekuwa ni makamu wake, ameapishwa katika ikulu ya jijini Dar es Salaam kuchukua wadhifa huo. Anawakuwa  mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini Tanzania , lakini pia kwa kanda ya Afrika Mashariki na wa pili kwa Afrika maana wa kwanza ni nchini Ethiopia.

BI SAMIA SULUHU AKILA KIAPO KUWA RAIS WA TANZANIA
BI SAMIA SULUHU AKILA KIAPO KUWA RAIS WA TANZANIA

Mara  baada ya kula kiapo na kukagua gwaride lililoambatana na mizinga ikiwa ni utaratibu wa kawaida kama amri jeshi mkuu, Bi Samia amehutubia taifa kwa kuanza kutoa taratibu za mazishi ya hayati Rais Magufuli, ambapo maombolezo yatakuwa ni siku 21 na kuelekeza kuwa, marehemu ataagwa  kuanzia  Dar es Salaam na kufuatiwa na mkoa Dodoma na Mwanza kuwakilisha mikoa yote kabla ya kuzikwa nyumbani kwao kufuatia Chato kuafuatia na uamuzi wake. Aidha Bi  Suluhu amelitangazia taifa lake siku mbili za mapumziko ya kitaifa ikiwemo siku ya kuaga wananchi wa dodoma na siku ya maziko ambayo ni tarehe 25 Machi. Wakati huo huo amewaomba raia wote kushirikiana na kuwa na utulivu wakati wa mazishi ambao unakuwa ni tofauti.

BI SAMIA AKIHUTUBIA TAIFA
BI SAMIA AKIHUTUBIA TAIFA

Katika hotuba yake hata hivyo ameonesha na kudhihirisha kwa taifa kuwa lina viongozi na katiba mambo ambayo ni muhimu kuliongoza nchi na kuwataka kila mmoja kuwa na matumaini na serikali iliyopo kwani amethibtisha wazi jinsi alivyo andaliwa vema na mtangulizi wake hayati Rais John Magufuli wakati akiwa ni makamu wake. Kwa maana hiyo Bi Suluhu amethibitisha kuendelea kuenzi yale yote ambayo mtangulizi wake amefanya na kwa kufanya hivyo ameomba kuwa ushirikiano na maombi kwa watanzania.

KIKAO CHA  KWANZA CHA RAIS WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN
KIKAO CHA KWANZA CHA RAIS WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN

Katika hafla hiyo ya kuapishwa kwa rais viongozi mbalimbali wamehudhuria wakiwemo Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliobaki na Zanzibar, Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi, spika wa Jamhuri wa muungano, Job Ndugai, jaji mkuu Profesa Ibrahim Juma pamoja na mawaziri mbalimbali na viongozi wa Kanisa. Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan atatoa huduma yake kama rais kwa kipindi cha muhula wa urais hadi pale uchaguzi mwingine wa urais utakapofanyika.

19 March 2021, 14:10