Tafuta

2024.01.29 Papa amakutana na Rais Umaro SIssoco Embalo, wa Jamhuri ya  Guinea Bissau 2024.01.29 Papa amakutana na Rais Umaro SIssoco Embalo, wa Jamhuri ya Guinea Bissau  (Vatican Media)

Papa amekutana na rais wa Guinea Bissau

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican:Jumatatu 29 Januari 2024,Papa amekutana na Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau,Bwana Umaro Sissoco Embaló,ambaye baadaye alikutana na Kardinali Parolin,Katibu wa Vatican,akifuatana na Askofu Mkuu Paul Gallagher,Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatatu tarehe 29 Januari 2024 kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican, inataarifa kuwa: “Baba Mtakatifu Francisko amempokea, katika Jumba la Kitume mjini  Vatican, Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau, Bwana Umaro Sissoco Embaló, ambaye  mara baada ya mazungumzo alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akifuatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.”

Papa Francisko na Rais wa Guinea Bissau  pamoja na uwakilishi wake
Papa Francisko na Rais wa Guinea Bissau pamoja na uwakilishi wake

Katika taarifa hiyo tunasoma kuwa: “Wakati wa mazungumzo yao ya ukarimu katika Sekretarieti ya Vatican, uhusiano mzuri kati ya Vatican na Guinea Bissau ulisisitizwa, na baadhi ya mambo ya hali ya kijamii ya nchi yaliakisiwa na mchango wa Kanisa kwa ajili ya manufaa ya wote ukasisitizwa, hasa katika nyanja za elimu na afya.

Rais wa Guinea Bissau akizungumza na Katibu wa Vatican.
Rais wa Guinea Bissau akizungumza na Katibu wa Vatican.

Katika kubadilishana zawadi za kiutamaduni, Papa Francisko amempatia rais Sanamu ya shaba, Idadi za hati za kipapa na vile vile Ujumbe wa Amani wa mwaka 2024.

Wakati wa kubadilishana zawadi
Wakati wa kubadilishana zawadi
Papa alikutana na Rais wa Guinea Bissau
29 January 2024, 16:18