Tafuta

2023.12.23 Balozi  Marek Zalewski 2023.12.23 Balozi Marek Zalewski  (Vatican Media)

Balozi Zalewski aliteuliwa kuwa mwakilishi mkazi wa Papa nchini Vietnam

Askofu mkuu Marek Zalewski,mwenye umri wa miaka 60,Balozi wa Vatican wa Singapore ameteuliwa kuwa tena mwakilishi wa makazi huko Vietinam.Julai iliyopita wakati wa ziara yake Rais Vo Van Thuong,wa Vietnam,mjini Vatican waliafikiana Mkataba wa kuwa na Mwakilishi Mkazi wa Papa nchini humo.

Vatican News

BabaMtakatifu Francisko  Jumamosi tarehe 23 Desemba 2023 amemteua Balozi wa kitume nchini Singapore,Monsinyo Marek Zalewski, mwenye umri wa miaka 60, Askofu mkuu wa Afrika, kuwa mwakilishi Mkazi  wa Papa huko Vietnam. Mnamo Julai 27 iliyopita, Vatican na serikali ya Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam ilikuwa imeafikiana(Accordo sullo Statuto del rappresentante pontificio residente)Makubaliano ya Mkataba wa kuwa na Mwakilishi Mkazi wa Kipapa huko Vietnam. Makubaliano hayo yalitiwa saini wakati wa ziara ya Rais Vo Van Thuong, mjini Vatican kwa msingi wa kikao cha kumi cha Kikundi kazi cha pamoja kati ya Vietnam-na Vatican  kilichofanyika tarehe 31 Machi 2023 mjini Vatican, kwa nia ya kuendelea kusongesha mbele mahusiano baina ya nchi hizi  mbili. Wakati wa mazungumzo kati ya rais wa Vietnam na Papa Francisko na baadaye na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin kwa mujibu wa  taarifa iliyoripotiwa(comunicato congiunto )kuwa: “Pande hizo mbili zilishukuru sana kwa maendeleo makubwa katika mahusiano baina ya nchi hizo mbili na kwa michango chanya iliyotolewa hadi sasa na jumuiya ya Kikatoliki ya nchi hiyo.”

Barua ya Papa kwa Kanisa la Asia

Katika (Lettera alla Chiesa della nazione asiatica)Barua kwa Kanisa la Taifa la Asia mnamo Septemba iliyopita, Papa Francisko aliwaalika waamini wa Kikatoliki kuishi kama “Wakristo wema na raia wema, wakishuhudia upendo wa Mungu bila ubaguzi wa dini, rangi na utamaduni.” Hata hivyo kuhusiana na mahusiano hayo yalikuwa yamekatizwa mnamo mwaka wa 1975, lakini yalikuwa yameona maendeleo ya kutia moyo tangu 1990. Na mnamo 2011 Papa Benedikto XVI alitemteua Mwakilishi wa Papa asiye mkaazi.

Askofu Mkuu Zalewski

Askofu Mkuu Zalewski alizaliwa mnamo mwaka 1963 huko Augustow, Poland, alipewa daraja la Upadre mwaka 1989. Ana shahada ya udaktari katika sheria ya kanuni kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana  Roma. Baada ya kuingia katika huduma ya kidiplomasia ya Vatican  mwaka 1995, amehudumu katika Tume mbali mbali za Vatican katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Umoja wa Mataifa, Uingereza, Ujerumani, Thailand, Singapore na Malaysia. Baba Mtakatifu Francisko pia alimteua kuwa Balozi wa Kitume nchini Zimbabwe mwezi Machi 2014. Licha ya lugha yake ya asili, pia anazungumza Kiitaliano, Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani na Kihispania.

Papa amteua Balozi mpya wa Vietnam
23 December 2023, 17:45