Tafuta

2023.07.07 Huko Lisbon utafanyika mkutano wa kwanza wa Utume wa kidihitalo katika Kiwanja cha Cristonautas wakati wa Tukio la WYD 2023.07.07 Huko Lisbon utafanyika mkutano wa kwanza wa Utume wa kidihitalo katika Kiwanja cha Cristonautas wakati wa Tukio la WYD  

Mkutano wa kwanza kimataifa wa wamisionari wa kidijitali huko Lisbon katika WYD

Katika mji mkuu wa Ureno,mnamo tarehe 4 Agosti 2023,toleo la kwanza la Tamasha la washawishi wa Kikatoliki,kupitia mtandao wa kidijitali litafanyika mbele ya Kadinali Oscar Rodriguez Maradiaga na Monsinyo Lucio Adrián Ruiz,katibu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ambalo ni moja ya wafadhili wa tukio hilo.

Vatican News.

Litakuwa tukio la kimataifa la kushukuru “kazi kubwa” ambayo watu wenye ushawishi wa kidijitali na wamisionari kutoka mabara matano hufanya kila siku, wakisambaza Injili kupitia mitandao yao ya kijamii. Uteuzi wa siku itakuwa  Ijumaa tarehe 4 Agosti, 2023 kuanzia saa 3.00 hadi 4.30,  usiku huko huko Lisbon, katika Eno la  Cristonautas, kwenye kiwanja cha  Martim Moniz, ambapo mkutano wa kwanza wa ulimwengu wa wainjilishaji wa kidijitali na wamisionari utafanyika “Tamasha la washawishi wa Kikatoliki.” Hayo yalikuwa yametangazwa na waandaji wa 'Kanisa linasikiliza' (The Church is Listening), mpango ulioanzishwa na wamisionari wa kidijitali ili kuitikia wito wa Papa Francisko kwa Kanisa zima kwa ajili ya Sinodi la Kisinodi, kwa nia ya kulifikisha katika mazingira ya kidijitali pia.

Kushiriki, shuhuda, maombi na muziki

Tamasha la Washawishi Wakatoliki kama tuonavyo "Enendeni Ulimwenguni kote" (Mk 16,15), litakuwa wakati wa kusherehekea pamoja, kushiriki shuhuda na uzoefu, kusali  na kuimba. Watu kutoka mabara yote watashiriki muziki na uzoefu wao, pia kwa kusindikizwa na  na Kadinali Oscar Rodriguez Maradiaga na Monsinyo Lucio Adrián Ruiz, katibu wa Baraza la Kipa la Mawasiliano.

Wimbo rasmi

Kwa ajili ya hafla hiyo, wimbo rasmi wa tamasha utawasilishwa, unaoitwa “Vamos por todo el Mundo”, ambao bi muziki na maneno yake yalitungwa na wasanii mbalimbali kutoka nchi mbalimbali: Aldana Canale (Argentina), Tomas Romero (Colombia) , Padre José Pablo (Chile), Pablo Martínez (Argentina) na Felipe Contreras (Marekani). Ufafanuzi wa lugha nyingi wa wimbo huu ulifanywa, vile vile na mmoja wa waandishi (Pablo Martínez kwa Kihispania) na waimbaji wa Kikatoliki: Pitter Di Laura (Kireno), Gen Verde (Kiitaliano), Juan Delgado (Kiingereza) na DJ. Halver ( Kifaransa).

Jinsi ya kufuatilia Tamasha

Wimbo na klipu ya video vitapatikana kwenye majukwaa yote ya kidijitali, yakijumuisha Spotify na YouTube, na kwenye tovuti ya Sinodi ya Dijitali: https://www.sinododigital.com/. Kwa hiyo  Tamasha hilo, ambalo linaweza kufuatiliwa mtandaoni kupitia tovuti rasmi, linaungwa mkono na kufadhiliwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano na pia kufadhiliwa na Chama cha Kikatoliki cha Wanapropaganda (ACdP) na Mfuko Cristonautas.

26 July 2023, 16:55