Mkutano wa kwanza kimataifa wa wamisionari wa kidijitali huko Lisbon katika WYD
Vatican News.
Litakuwa tukio la kimataifa la kushukuru “kazi kubwa” ambayo watu wenye ushawishi wa kidijitali na wamisionari kutoka mabara matano hufanya kila siku, wakisambaza Injili kupitia mitandao yao ya kijamii. Uteuzi wa siku itakuwa Ijumaa tarehe 4 Agosti, 2023 kuanzia saa 3.00 hadi 4.30, usiku huko huko Lisbon, katika Eno la Cristonautas, kwenye kiwanja cha Martim Moniz, ambapo mkutano wa kwanza wa ulimwengu wa wainjilishaji wa kidijitali na wamisionari utafanyika “Tamasha la washawishi wa Kikatoliki.” Hayo yalikuwa yametangazwa na waandaji wa 'Kanisa linasikiliza' (The Church is Listening), mpango ulioanzishwa na wamisionari wa kidijitali ili kuitikia wito wa Papa Francisko kwa Kanisa zima kwa ajili ya Sinodi la Kisinodi, kwa nia ya kulifikisha katika mazingira ya kidijitali pia.
Kushiriki, shuhuda, maombi na muziki
Tamasha la Washawishi Wakatoliki kama tuonavyo "Enendeni Ulimwenguni kote" (Mk 16,15), litakuwa wakati wa kusherehekea pamoja, kushiriki shuhuda na uzoefu, kusali na kuimba. Watu kutoka mabara yote watashiriki muziki na uzoefu wao, pia kwa kusindikizwa na na Kadinali Oscar Rodriguez Maradiaga na Monsinyo Lucio Adrián Ruiz, katibu wa Baraza la Kipa la Mawasiliano.
Wimbo rasmi
Kwa ajili ya hafla hiyo, wimbo rasmi wa tamasha utawasilishwa, unaoitwa “Vamos por todo el Mundo”, ambao bi muziki na maneno yake yalitungwa na wasanii mbalimbali kutoka nchi mbalimbali: Aldana Canale (Argentina), Tomas Romero (Colombia) , Padre José Pablo (Chile), Pablo Martínez (Argentina) na Felipe Contreras (Marekani). Ufafanuzi wa lugha nyingi wa wimbo huu ulifanywa, vile vile na mmoja wa waandishi (Pablo Martínez kwa Kihispania) na waimbaji wa Kikatoliki: Pitter Di Laura (Kireno), Gen Verde (Kiitaliano), Juan Delgado (Kiingereza) na DJ. Halver ( Kifaransa).
Jinsi ya kufuatilia Tamasha
Wimbo na klipu ya video vitapatikana kwenye majukwaa yote ya kidijitali, yakijumuisha Spotify na YouTube, na kwenye tovuti ya Sinodi ya Dijitali: https://www.sinododigital.com/. Kwa hiyo Tamasha hilo, ambalo linaweza kufuatiliwa mtandaoni kupitia tovuti rasmi, linaungwa mkono na kufadhiliwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano na pia kufadhiliwa na Chama cha Kikatoliki cha Wanapropaganda (ACdP) na Mfuko Cristonautas.