Ukatili wa kinyama na muujiza wa msamaha
ANDREA TORNIELLI
Tangu hotuba yake ya kwanza mjini Kinshasa, Papa Francisko aliutaka ulimwengu kutofunga macho, masikio na midomo yake kwa kile kinachotokea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na bara lote la Afrika. Alasiri ya siku ya pili ya ziara yake, katika ukumbi wa Ubalozi wa Vatican, kulikuwa na makabiliano makubwa kuhusu ukatili wa kinyama wa migogoro na vurugu zinazoendelea mashariki mwa nchi hiyo inayokumbwa na mapambano ya kikabila na kimaeneo, katika migogoro ambayo inahusishwa na mali ya ardhi, chuki za kufuru za wale wanaoua kwa jina la mungu wa uongo. Nchi iliyokumbwa na vita “iliyochochewa na uroho usioshibishwa wa malighafi na pesa”.
Ukimya tu na machozi ndiyo yangeweza kusindikiza historia zilizowasilishwa kwa Papa, kama ile ya mkulima mdogo Ladislas, ambaye aliona wanaume waliovalia kama askari wakimuua na kumkatakata baba yake na kumteka nyara mama yake. Kama ile ya Bijoux, ambaye mnamo 2020 akiwa na umri wa miaka kumi na tano wakati anakwenda kuchota maji kutoka mtoni alitekwa nyara na kundi la waasi, na kubakwa kwa miezi 19 na kamanda wao. Alifanikiwa kutoroka akiwa mjamzito na sasa alikuwa pale mbele ya Mrithi wa Petro pamoja na watoto wake mapacha. Kama ile ya Emelda, ambaye aliishia kuwa mateka mikononi mwa waasi siku ya Ijumaa jioni mwaka 2005, akiwa na umri wa miaka kumi na sita, na kushikiliwa kama mtumwa wa ngono kwa miezi mitatu: wanaume watano hadi kumi walimnyanyasa kila siku. Alilazimishwa, ili asiishie vipande vipande pia, na kula nyama za wale watu waliouawa…
Ni kimya tu na na machozi. Papa Francisko alikuwa alipigwa na butwaa na hisia kali. Katika hotuba yake alirudia kwa jina la Yesu, kwa sababu “pamoja naye uovu hauna tena neno la mwisho juu ya maisha ... Pamoja Naye kila kaburi linaweza kubadilishwa kuwa kitanda cha mtoto, kila jaribio kuwa bustani ya Pasaka”. Pamoja naye matumaini yanaweza kuzaliwa upya kwa wale ambao wameteseka mabaya na hata kwa wale ambao wameyatenda”. Waathirika, wakijishughulisha katika mchakato wa msamaha na upatanisho, waliweka baadhi ya alama za mateso yao kama vile panga, mkeka, baadhi ya misumari, chini ya Msalaba mkubwa uliosimama karibu na Papa. Ni vigumu hata kufikiria uwezekano wa msamaha huo baada ya kusikia maneno yao na bahari ya vurugu, mateso na fedheha ambazo wamestahimili. Ikiwa inatokea, ni kwa neema safi kabisa. Na ni muujiza tu unaweza kuruhusu. Katika muujiza huo, unaowezekana kwa wale wanaoishi kutoka kwa Yule aliyefanya uzoefu wa kaburi kuwa mwanzo wa historia mpya, na kuona wakati jua likizama Kinshasa!