Tafuta

Papa asikiliza shuhuda za wahanga wa ukatili wa Mashariki mwa DRC

Katika mkutano uliofanyika Februari Mosi katika Ubalozi wa Vatican,Kinshasa,ni shuhuda za ukatili usiofikirika dhidi ya wavulana na wasichana ambao kwa msaada wa Kanisa wameanza kuishi kwa upya.Walimwambia Papa wanahitaji amani tu na kuwasamehe watesi wao ili kuishi katika roho ya udugu,upatanisho na imstakabali wa nchi.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Papa Francisko Jumatano alasiri tarehe Mosi Februari 2023 mara tu baada ya Misa asubuhi na kufanya Mkutano wa kwanza katika Ubalozi wa Vatican jijini Kinshasa DRC na walemavu na vikundi vya matendo ya upendo  alikutana na wahanga wa ukatili mkubwa wa ubakaji, waliotekwa nyara na walemavu wa kila aina katika Mashariki mwa nchi hiyo. Kwa hakika ilikuwa ni kipindi kigumu hasa wakati wa kutoa shuhuda za kutisha sana. Ni vema ndugu msikilizaji na msomaji kuelewa ni mateso gani ya kimwili na kiroho na kitu gani kimetendeka na kinaendelea kutendeka kwa ndugu zetu jirani. Kila wakati baada ya ushuhuda walioomba kwa Mwenyezi Mumba wa Mbingu na nchi: “Bwana, Mungu wetu, ambaye kwake tumepokea uhai wetu na uzima wetu, leo tunaweka vyombo vya mateso yetu chini ya Msalaba wa Mwanao. Tumejitolea kusameheana na kuepuka njia yoyote ya vita na migogoro ili kutatua tofauti. Tunakuomba, Baba, kwa neema yako, kuifanya nchi yetu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa mahali pa amani na furaha, upendo na amani ambapo kila mtu anapenda na kuishi pamoja kidugu. Roho wako daima anatusindikiza na Baba Mtakatifu, aliyepo hapa, utuombee.

Papa akikutana na walemavu na makundi ya upendo nchini DRC

Shuhuda kutika Goma

Baadaye zilianza shuhuda za kugusa: "Ninaitwa Kissa Catarina na ninasomaushuhuda wa Bijoux Mkumbi Kamala  aliyekaribu nami kwa sababu hajuhi kusoma vizuri kifaransa". “Ninatoka Walikale. Nina miaka 17.  Kwa hiyo akiendelea kusoma alisema yeye alianza kalavari ya mateso mnamo 2020.  Ambapo siku moja alikuwa anakwenda kuteka maji kwenye mto. Huko Musenge, moja ya vijiji vya eneo la Walikale 2020. Wakati wako njia walikutana na waasi ambao waliwachukua mateka hadi kwenye msitu. Kila muasi alichagua anayetaka. Kamanda wa kikundi walimbaka kama mnyama. Ilikuwa ni mateso makali. Na alibaki hapo kama mke wake. Walikuwa wakimlaiti mara kadhaa kwa siku, jinsi walivyokuwa wakitaka kwa masaa mengi. Hali hiyo ilienda mbele hati miei mwaka mmoja na miezi saba. Ilikuwa bure kupiga kelele kwa sababu hakuna ambaye angeweza kumsikiliza au kumsaidia. Lakini alipata kutoroka kwa bahati nzuri na rafiki yake baada ya miei 19 ya mateso. Kutokana na uzoefu huo mbaya alibaki mjamzito.

Yeye baadaye alijifungua mapacha ambao amesema kwamba hawatamjua kamwe baba yao. Marafiki wenzake wa kike waliokuwa wametekwa nyara naye hawakurudi tena. Hawajuhi kama walikufa aubado wanaishi. Kwa njia hiyo akiendelea ameeleza kwa Papa kwamba uwepo wa makundi mengi ya sila0ha, mauaji yameongezeka zaidi kila mahali, familia zimekuwa zikirudikana mara nyingi, watoto ambao wamebaki bila wazazi wao, wamenyonywa katika machimbo ya madini au zidi kwenye vikosi vya waasi; wasichana na wanawake walianza kalvari ya nyanyaso za kijinsia za kila aina, na mateso yasiyo na jina.  Watu wengi wamerudindika na hawana mahali pa kukaa , wanakwenda hapa na pale. Aidha ameeleza Papa kwamba kwa yote hayo Kanisa linabaki kama moja ya kimbilio ambalo linatibu majeraha yao na kufariji mioyo yao kwa njia ya huduma nyingi za msaada na kuwatia nguvu: maparokia na huduma za caritas jimbo zinabaki kuwa maeneo yao ya kukimbilia na msaada. Uwepo wake Baba Mtakatifu umewahakikisha kuwa Kanisa linachukua wajibu wa kuwasaidia.Amemshukuru sana ujio wake.

Na hatimaye walitoa zawadi ya mkeka kama ishara ya umaskini wao wa kike ulioharibiwa. Ameuweka chini ya msalaba wa Kristo ili Msalaba. “Huu hapa mkeka, ishara ya mateso yangu kama mwanamke aliyebakwa. Ninaiweka chini ya msalaba wa Kristo, ili Kristo anisamehe kwa hukumu nilizotoa moyoni mwangu dhidi ya watu hawa. Msalaba wa Kristo unisamehe mimi na wabakaji wangu na uwaongoze kuacha kuwatesa watu bila sababu. Huu pia ni mkuki sawa na ule ambao ulichoma vifua vya  ndugu zetu wengi. Mungu atusamehe sote na atufundishe kuheshimu maisha ya mwanadamu.”

Mwathirika wa Bunia

Jina langu ni Don Guy-Robert Mandro Deholo na nimekatwa kwenye vidole vya mkono mmoja. Ninawasilisha ushuhuda ambao Désiré Dhetsina alikuwa ametayarisha, kabla ya kutoweka miezi michache iliyopita, bila kuacha habari. “Mimi ni manusura wa shambulio katika kambi ya IDP ya Bule katika kijiji cha Bahema Badjere, eneo la Djugu, Wilaya ya  Ituri. Kambi hiyo inajulikana kama "Plaine Savo". Shambulio hilo lilifanyika usiku wa kuamkia tarehe Mosi Februari 2022 na kundi lenye silaha, ambalo liliua watu 63, wakiwemo wanawake 24 na watoto 17. Niliona unyama huo: watu walikatwa vipande vipande kama nyama ya mchinjaji, wanawake waliovuliwa matumbo, wanaume waliokatwa vichwa. Tunaishi katika kambi za watu waliohamishwa bila matumaini ya kurudi nyumbani, kwa sababu mauaji, uharibifu, uporaji, ubakaji, uhamishaji wa watu, utekaji nyara, unyanyasaji, kwa kifupi, vinaonekana kama utekelezaji wa mpango wa kuangamiza, wa maangamizi ya kimwili, kiadili na kiroho, ambao unaendelea kila siku.

Baba Mtakatifu, tunahitaji Amani na hakuna  cha zaidi ila Amani, zawadi hii ya bure ya Yesu Kristo Mfufuka. Tunataka kurudi vijijini kwetu, tulime mashamba yetu, tujenge nyumba zetu, tusomeshe watoto wetu, tuishi pamoja na majirani zetu wa zamani, mbali na kelele za bunduki! Tunataka uovu unaotendwa Ituri ukome, uadhibiwe na urekebishwe! Tunataka kuishi kwa heshima kama wana na binti za Mungu. Kwa hilo tunaweka mapanga na nyundo hizi chini ya msalaba wa Kristo, ili atusamehe kwa damu iliyomwagika isivyo haki. Kristo atupe nyakati za amani na utulivu ambapo kila mtu awe na  hisia nzuri kwa mwenzake. Asante sana kwa kuja kutufariji, Baba Mtakatifu. Asante sana kwa kutuombea.”

Katika ushuhuda kutoka Bukavu na Uvira

Baba Mtakatifu Mimi ni Aimée na ninazungumza kwa niaba ya Emelda M'KARHUNGULU wa Bugobe, Groupement Cirunga, Parokia ya Kabare, katika Jimbo Kuu la Bukavu, kusini-magharibi mwa jiji hilo kubwa. Emelda yuko karibu nami lakini hazungumzi Kifaransa. Ninasoma tafsiri ya Kifaransa ya ushuhuda wake kwa lugha ya Kiswahili. “Waasi walikuwa wamevamia kijiji chetu cha Bugobe; ilikuwa Ijumaa jioni mnamo mwaka wa 2005. Waliingia kijijini, wakimchukua kila mtu ambaye wangeweza kumteka, na kuwafukuza kila mtu waliyemkuta, na kuwafanya wabebe vitu vilivyoporwa. Wakiwa njiani, waliwaua wanaume wengi kwa risasi au visu. Badala yake, wanawake waliwapeleka Mbuga ya Kahuzi-Biega. Wakati huo nilikuwa na miaka 16

Nilishikiliwa kama mtumwa wa ngono na kuteswa kwa muda wa miezi mitatu. Kila siku, wanaume watano hadi kumi walitunyanyasa kila mmoja wetu. Walitufanya tule mahindi na nyama ya watu waliouawa. Wakati fulani walichanganya vichwa vya watu na nyama ya wanyama. Hiki kilikuwa chakula chetu cha kila siku. Waliokataa kula walikatwa vipande vipande na wengine walilazimishwa kula. Tuliishi uchi ili tusikimbie. Nilikuwa mmoja wa wale waliotii, hadi siku ambayo, kwa neema, nilifanikiwa kutoroka walipotutuma kuchota maji mtoni. Niliporudi nyumbani, wazazi wangu walinipeleka kwenye hospitali ya Panzi, nikapitia kituo cha Olame, ambako nilipata matibabu ya kutosha. Kupitia uhuishaji wa Kanisa ilinibidi kudhani na kukubali hali yangu. Pia, watu walionidhihaki wamebadilika. Leo  hii ninaishi vizuri kama mwanamke aliyekamilika ambaye anakubali maisha yake ya zamani. Mkoa wetu ni mahali pa mateso na machozi.

Ninaweza kusema nini, Baba Mtakatifu, kuhusu wahanga wa maafa ya Mulongwe ambao wamepoteza kila kitu kwa mmomonyoko wa pori: nyumba na vitu vyote vilivyomo. Wengi wamekufa. Maafa ya mafuriko katika mito ya Mulongwe na Kavimvira, Jimbo  Uvira,  mnamo tarehe 17-20 Aprili 2020, yalisababisha watu 60 kuzikwa chini ya matope ya mafuriko, watu 45 kujeruhiwa, nyumba 3500 kuharibiwa, familia 7700 hazina makazi. Walionusurika wanaishi katika kambi za maafa ambapo wanashiriki katika  hema moja na familia 3 au 4, yaani watu kadhaa, katika hema moja, limejaa sana. Hakika ni makao ya uasherati. Ukahaba unashamiri katika mazingira haya ya kuishi. Hawana hata kiwango cha chini cha hali ya kibinadamu. Kutokana na vita baina ya makabila katika nyanda za juu, zaidi ya watu 346,000 wamekimbia makazi yao katika maeneo ya miinuko ya Fizi, Mwenga/Itombwe na Uvira tangu 2019, ikijumuisha 100,000 katika eneo la Uvira na 246,000 katika eneo la Fizi. Wengi wameacha kila kitu. Ukanda  mzima umeachwa kwa watu wenye silaha. Wengi walikufa, wengine walikimbia, bila hata kujua wapi mahali pa kupata wapendwa wao.

Baba Mtakatifu, ni kwa furaha kubwa kwamba sisi, wahanga wa ukatili na maafa mengine, tunachukua nafasi ya kuwasilisha kwako shukrani zetu za dhati na shukrani zetu kwa kututembelea licha ya majukumu yako mengi. Unatuachia urithi, zawadi ya upendo kupitia ukaribu huu, kupitia ukaribu wako. Kwa hiyo tunaweka chini ya msalaba wa Kristo nguo hizi za wanaume waliovaa silaha ambao bado wanatutisha, kwa kuwa wametufanyia vitendo vingi vya kikatili na vya kikatili  sana visivyoelezeka, ambavyo bado vinaendelea hadi leo hii. Tunataka mustakabali tofauti. Tunataka kuacha siku hii ya giza nyuma na tuweze kujenga mustakabali mzuri. Tunaomba haki na amani. Tuwasamehe wauaji wetu kwa yote waliyofanya na tumwombe Mungu  atujalie neema ya kuishi pamoja kwa amani, kibinadamu na kidugu. Asante Baba Mtakatifu kwa ufika kwako.”

Shuhuda nyingine zilitoka kwa waathirika wa Butembo Beni

Baba Mtakatifu ninaitwa Ladislas KAMBALE KOMBI. Nilizaliwa Eringeti tarehe 15 Julai 2006. Mimi ni mkulima kitaaluma. Mimi ni wa pili katika familia yangu. Kaka yangu mkubwa aliuawa katika mazingira ambayo bado hatuyajui hadi leo. Baba yangu aliuawa nikiwepo, kule Ingwe, kuelekea Kikungu, Wilaya ya Beni, na wanaume waliovalia suruali za mafunzo na mashati ya jeshi. Kutoka mahali nilipojificha, nilifuatilia jinsi walivyomkata, kisha kichwa chake kilichokatwa kikawekwa kwenye kikapu. Hatimaye, waliondoka na mama. Walimteka nyara. Tukabaki yatima, mimi na wadogo zangu wa kike wawili. Mama hakurudi tena hadi leo. Hatujui walifanya nini naye. Baba Mtakatifu, ni jambo la kutisha kuona tukio kama hilo. Haliniachi kamwe. Usiku siwezi kulala. Ni vigumu kuelewa uovu kama huo, ukatili huu wa karibu na  wanyama. Baba Mtakatifu, Tunakushukuru kwa kuja kutufariji. Kufuatia mfuatano wa kiroho na kisaikolojia wa Kanisa letu la mahalia, mimi na watoto wengine ambao tuko hapa tumewasamehe watekaji wetu. Ndiyo maana ninaweka mbele ya Msalaba wa Kristo mshindi panga sawa na lile lililomuua baba yangu.

Mimi pia (Léonie Matumaini kutoka shule ya msingi ya Mbau) ninamwekea mbele ya Msalaba wa Kristo mshindi kisu sawa na kile kilichoua watu wote wa familia yangu mbele yangu na ambacho nilipewa na wauaji, wakinitaka niwakabidhi askari wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Mimi pia (Kambale Kakombi Fiston, mwenye umri wa miaka 13, kutoka shule ya msingi Chamboko) ninawasamehe wauaji walioniteka nyara kwa miezi 9. Ninamwomba Kristo aliyeshinda msalabani aguse mioyo ya watesaji ili wawafungue watoto wengine ambao bado wako msituni. Baba Mtakatifu ninakuomba uwaombee watoto hawa ili hatimaye wapate kuungana  nasi shuleni na katika jamii. Asante.

Wakati wa ushuhuda uliimbwa wimbo wa kiswahili

R/ Natoa shukrani kwa Mungu, Mungu muumbaji wangu, Bwana wangu,
Natoa shukrani kwa Mungu, Mungu muumbaji wangu, amenitendea makuu.

1. Mungu wangu usifiwe daima, uliye nipa uzima, kwa neema yako ninaishi kwa kuwa nimependwa nawe. Jina lako ni kubwa sana Bwana wangu na unastahili sifa, na shukrani yangu ni kwako siku zote, kwako wewe Mungu mzima.
2. Mungu wangu utukuzwe daima uliye mchungaji wangu, kwa uwezo wako ninashinda maovu haukuniachilia, utukufu wako ni kubwa bwana wangu katika maisha yangu. Tangu utoto wangu umenipenda sana, Bwana wewe mkinga wangu.
Mungu wangu utukuzwe popote katika viumbe vyako, yote tunayo katika maisha yetu ni kwa neema yako. Moyo wangu wakuimbia siku zote, kwani wewe wastahili, bila wewe siwezi kitu mimi mkosefu, bali ninakubariki.

Ushuhuda wa wahanga wa Mashariki mwa DRC mbele ya Papa
02 February 2023, 10:27