Wanawake katika majadiliano ya kukuza mtandao wa kidini kimataifa!
Na Angella Rwezaula- Vatican.
Mkutano wa kimataifa wa “Wanawake wanaojenga utamaduni wa kukutana baina ya dini ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini kwa kushirikiana na Umoja wa Mashirika ya Wanawake Wakatoliki Duniani ulikuwa na lengo kuu sehemu mbili: Kusikiliza mipango baina ya dini za wanawake kutoka katika mazingira mbalimbali na kutoa uhai wa dhati kupitia mtandao wa kimataifa wa wanawake wa mila na desturi mbalimbali za kidini zinazopendelea kuhuisha hadhi ya jamii kwa njia ya urafiki, mazungumzo na ushirikiano. Hawa ni ni washiriki wa kimatifa waliokutana mjini Vatican kuanzia tarehe 25 - 27 Januari, 2023 katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, kwenye ukumbi wa Yohane Paulo II, ambapo walikuwa ni wanawake viongozi 30 kutoka nchi 23 tofauti, wakiwakilisha tamaduni 12 za kidini. Tarehe 26 Januari walikuwa na fursa ya kukutana na Papa ambapo aliwambia kuwa Kanisa Katoliki limejikita katika majadiliano ya kidini na katika kuhamasisha uelewa na ushirikiano kati ya waamini wa tamaduni nyingi za kidini. Kila mmoja wa tamaduni hizi na kila mmoja wao binafsi ana utajiri wa kutoa ulimwenguni, kwa kueneza roho moja ya makaribisho, ya kutunza na ya udugu.
Uzoefu wa wanawake katika familia na jumuiya
Sehemu kubwa ya waliokuwa kwenye mkutano huo imehusika kugundua mantiki ya kike katika tamaduni zao za kidini na kuonesha zenyewe jinsi zinavyochangia utamaduni mmoja wa kukutana. Kiukweli kukaa na kusikiliza mwingine, tabia ya kukutana kibinadamu ni mfano wa tabia ya kukaribisha, ya kushinda kujipendelea na kumpokea mwingine, kwa kumpatia umakini, kutengeneza nafasi katika mzunguko binafsi. Papa ametoa onyo kuwa Shughuli za makutano na ufunguzi unaohitajika, unaanza kupotea na wakati uzoefu wake ni moja ya zawadi kubwa ambazo wanaweza kutoa katika familia zao, jumuiya zao na jamii. Katikati ya siku zao za kulikuwa na majadiliano juu ya takwimu za wanawake katika Maandiko matakatifu na juu ya mafundisho ya kidini kwa ajili ya utamaduni wa kukutana, kubadilishana uzoefu na mchango wa watakatifu na watu wenye hekima. Kwa njia hiyo ripoti, majukwaa, majadiliano na nyakati za kushirikishana zilikuwa kwa umama yaani kwa waliokuwa ukumbini na kwa njia ya mtandaoni: www.vaticannews.va. Kwa kufungua siku ya kwanza ua kazi kulikuwa na kipindi cha ukimya wa sala ukisindikizwa na muziki wa ala.
Kujenga madaraja, kubomoa kuta, kufikiria juu ya mipango ya kawaida
Naye Monsinyo Indunil Kodithuwakku, katibu wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini akizungumza na Vatican News, alieleza juu ya dhana ya utamaduni wa kukutana ilivyo zaliwa wakati wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican ambao ulitia nguvu ya mazungumzo ya kidini na Waraka huo wa Nostra Aetate ambao kwa hakika uliotolewa na Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili kuhusiana na majadiliano ya kidini. Papa Francisko katika Waraka wake wa Kitume wa, Fratelli tutti (216) anasisitiza kuwa “Kuzunguzam juu ya utamaduni wa kukutana” maana yake ni kama watu walio na ari ya kupenda kukutana, kutafuta vipengele vya kuwasiliana, kujenga madaraja , kupanga jambo lolote ambalo linawajumuisha wote”. Kwa maana hiyo hiki ndicho kipengele cha kwanza cha kujenga utamaduni wa kukutana, kwa maelezi ya Monsinyo Kodithuwakku kwamba shauku ya kukutana na mwingine, shauku ambayo pia inatoka na Ukristo, kwa sababu Mungu ndiye wa kwanza kuingia ulimwenguni ili kukutana na ubinadamu. Zaidi ya hayo, imani ya Kikristo ni kukutana na Bwana Yesu Kristo. Mkutano huo kwa mujibu wa katibu wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini, unasaidia kushinda chuki, ujinga, woga, unasaidia kuponya majeraha ya wakati uliopita.
Katika majadiliano,muunganiko na tofauti hujitokeza
Zaidi ya hayo, katika makabiliano hayo, ni kujaribu kutafuta sehemu za kuwasiliana kwa sababu katika kukutana kuna mazungumzo na katika mazungumzo muunganiko na tofauti hujitokeza. Kwa hivyo, alibainisha Monsinyo Kodithuwakku, kwa kuanzia na dhana ya kwamba sisi sote hatufanani na kwamba hata dini, katika mazungumzo, kusikiliza mwingine husababisha kuheshimu utofauti, wakati huo huo maadili ya kawaida, maadili ya ulimwengu huibuka kama vile amani, haki, upendo na maelewano. Maadili haya yapo katika dini zote, na kwa kuzingatia maadili haya alisema inawezekana kufanya kazi pamoja. Na baadaye kujenga madaraja. Kwa hiyo, kukutana na kuzungumza husaidia kujenga madaraja, kubomoa kuta na kufikiria mipango ya kawaida kwa pamoja. Na hivyo ndivyo Baraza la kipapa la Majadiliano ya kidini yanalenga kukutana na wengine na kisha kuwa na mazungumzo, kutambua maeneo ya kuwasiliana, kujenga madaraja, na kupanga pamoja. Hiyo ndio maana hakika ya kujenga utamaduni wa kukutana.
Kuwapa wanawake sauti
Wazo la kutoa sauti kwa ulimwengu wa kike lilizaliwa ili kuhakikisha kwamba tofauti iliyopo kati ya yale ambayo dini tofauti na sheria za kiraia za fursa sawa kwa wanawake na ukweli zinafundisha, alisema Monsinyo Kodithuwakku. Tofauti ambayo Papa Francisko pia ameonesha wazi katika Waraka wa Fratelli tutti (23) akisema kwamba “shirika la jamii ulimwenguni kote bado liko mbali na kuonesha wazi kuwa wanawake wana hadhi sawa na haki sawa na wanaume. Maneno yanathibitisha mambo fulani, lakini maamuzi na ukweli hupaza sauti nyingine”. Je hapo ni kufanya nini? Katika hati kuhusu Ududgu wa Kibinadamu Documento sulla “Fratellanza umana” anapendekeza suluhisho la kupambana na ukosefu wa usawa na unyanyasaji dhidi ya wanawake ambapo kiukweli anafafanua 'umuhimu wa lazima wa kutambua haki ya wanawake ya elimu, kufanya kazi, kutekeleza haki zao hata kwa upande wa siasa na kwamba Papa anatoa mwaliko wa kufanya kazi ya kuikomboa hadhi hiyo kutokana na shinikizo za kihistoria na kijamii kinyume na kanuni za imani ya mtu na hadhi yake.
Mchango wa wanawake katika jamii
Mkutano waliouandaa kwa maana hiyo ulitaka kuwapatia nafasi wanawake katika muktadha wa mchakato wa mageuzi. Mnamo mwaka 2017, kiukweli, katika mkutano wao mkuu, alibanisha Monsinyo Kodithuwakku kwamba walitafakari juu ya jukumu la wanawake katika elimu, na hivyo basi mnamo 2019 walitaka majadilisno kati ya watawa wa Kibudha na watawa wa Kikatoliki katika monasteri ya Wabudha. Kwa ufupi, kila wakati kama Baraza la Kipapa la Muktahda hui wa majadiliano ya kidini wanajaribu kuwajumuisha wanawake kwenye meza ya mazungumzo, na katika furah hiyo ya mkutano jijini Roma walitaka kusikia tena sauti zao. Kwa sababu mchango wao ni muhimu. Zaidi ya hayo, kuna ukamilishano kati ya wanaume na wanawake. Na baadaye mwanamke na majukumu tofauti katika jamii, kama mama, mke, mahali pa kazi, kama mwalimu, na tena katika Kanisa, katika dini. Kwa hiyo ni lazima isemwe, tena kwamba wanawake wanahisi, zaidi ya mtu mwingine yeyote, kile kinachotokea katika jamii, alisisitiza Katibu wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini. Katibu hiyo aliendelea kueleza Monsinyo Kodithuwakku kwamba “Tunaishi katika ulimwengu wa majeraha mengi, na wanawake ndio wa kwanza kujeruhiwa, kwa sababu kuna ubaguzi katika jamii. Kwa hiyo, tunahitaji kusikia sauti zao. Wanawake pia hujibu, kwa kujaribu kubadilisha jamii, utamaduni, na kuna harakati za wanawake ambazo zimejaribu kuleta mabadiliko katika jamii kwa kushirikiana na kila mtu. Wanawake wana usikivu fulani ambapo wanaume hawana wana uwezo mkubwa wa kusikiliza hivyo. Matukio haya huwasaidia wanawake kutafakari, na kisha, katika mwanga wa dini yao, huleta mabadiliko, kwao wenyewe na kwa ajili ya familia nzima ya binadamu.”
Utamaduni wa kukutana katika mazingira magumu
Lakini kujenga utamaduni wa kukutana ni tatizo zaidi pale ambapo kuna mazingira magumu, mazingira ambayo mtu anakataa kukutana. Kwa hiyo Harakati za itikadi kali na misimamo mikali ya kidini kwa mjibu wa Katibu wa Baraza la Kipapa la Majadiliani ya kidini kwamba zina mambo ambayo yanapingana na utamaduni wa kukutana. Ikiwa utamaduni wa kukutana unamaanisha kukutana, kuzungumza juu ya maadili ya kawaida, kujenga madaraja, kuendeleza mipango pamoja, harakati hizi zina mwelekeo tofauti kabisa. Badala ya kukutana wanataka kujifungia, na badala ya kujenga madaraja wanainua kuta. Hatahivyo haipaswi kuweka kwa ujumla, kwa sababu ikiwa katika jamii, na katika dini, kuna makundi mbalimbali ya itikadi kali inayojifunga binafsi, pia kuna hata makundi mengine yaliyo wazi; harakati ambazo ni dhidi ya itikadi kali, dhidi ya misimamo mikali. Na baadaye ni lazima kushirikiana nao na pia na mashirika ya kiraia, na watendaji wa kisiasa ambao wana shauku sawa ya kujenga utamaduni wa kukutana. Ni dhamira ya kila mmoja basi, kujumuisha watu wengi zaidi, harakati zaidi kwa kuhamasisha utamaduni wa kukutana, licha ya kuwepo kwa vikwazo katika mazingira tofauti, ambayo yanatokana na mizizi ya kale, matatizo ya kisiasa na kijamii, matatizo ya makabila, mila, na dhuluma za kimataifa au kikanda. Haya ni masuala ambayo yanapaswa kushughulikiwa ili kupata ufumbuzi wa kudumu, alishauri Monsinyo Kodithuwakku.
Kazi ya Makanisa mahalia
Katika sehemu nyingi za dunia, leo hii harakati mbalimbali zinakwenda kinyume na utamaduni wa kukutana. Aidha, utandawazi umeibua harakati mbalimbali zinazojaribu kujifungia. Kwani kuna baadhi ya zilizo barani Asia, Afrika, Amerika ya Kusini, na pia Ulaya, ambapo, kwa mfano, kuna mvutano juu ya uhamiaji. Baadaye ni jambo muhimu, pia ushirikiano na Kanisa mahalia, ambalo tayari linafanya kazi katika mazingira haya magumu, na kuendeleza majadiliano na kujenga utamaduni wa kukutana. Hili ndilo tumaini la siku zijazo, amesisitiza Katibu huyo. Sauti za wanawake ni muhimu, na ziko katika mizunguko mingi. Katika mazingira ya familia, kwa mfano. Hatimaye sauti ya mwanamke inahesabiwa, inaleta familia nzima pamoja kwa mujibu wa maelezo hayo ya Monsinyo Kodithuwakku. Na tena, katika nyanja ya elimu, wanawake wameongezeka, katika mazingira mbalimbali si kama miaka 20 au 30 iliyopita. Leo hii wanawake wanasoma, wana majukumu ya uongozi. Lakini kuna maeneo ambayo yanahitaji kuboresha, kama vile katika uwanja wa siasa, ambapo wanawake bado hawana jukumu muhimu sana, na hivyo kunahitajika kujumuisha sauti zao. Hali inabadilika katika mazingira fulani, sio kwa wengine, kwa sababu kuna vikwazo vya kiutamaduni. Lazima kuwe na kazi kwa kila mtu, wanawake na wanaume, ili wanawake wasikilizwe. Kwa upande wa katibu wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini alisema mahali ambapo hakuna sauti ya wanawake, mambo yanahitaji kubadilishwa kabisa.
Mtandao wa dini kimataifa kati ya wanawake
Mkutano huo ambao uliwaona wanawake kama wahusika wakuu wa kuhamaisha utamaduni wa kukutana baina ya dini ulitaka kwa hakika kuendelea na mitandao. Lakini hizi sio habari kubwa, alibainisha Monsinyo Kodithuwakku. Kwa sababu kwa kuzungumzia juu ya mitandao ya wanawake, walibaini kuwa katika historia ya Kanisa kumekuwapo na makutaniko ya kike ambayo yalianza kazi zao katika nchi moja na kusambaa kwingine, huku yakitjikita, kulingana na karama zao, na kuleta mabadiliko katika utamaduni. Baadhi ya watawa wamefanya hivyo katika nyanja ya elimu, wengine katika hospitali, na wengine katika uwanja wa haki. Kwa miaka mingi, Kanisa limekuwa na mtandao huo na dini nyingine pia zimefanya hivyo. Lengo, basi, katika ulimwengu ambapo kuwasiliana kumekuwa rahisi leo hii, na pia kuzunguka, ni kuunda mtandao mpya. Kwanza kabisa katika matarajio yao, wanataka kuhimiza makundi katika mazingira ya ndani, ambayo yanaweza kuwa majimbo na ambayo yanaweza kuenea hadi ngazi ya kitaifa. Na baadaye kuunda mitandao ya kikanda na bado kufikia mtandao mpana zaidi, lakini pia kwa kutumia teknolojia ya kisasa, ili hatimaye kulenga mikutano ya mara kwa mara. Kwa sababu hiyo Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini yanapenda kujenga mtandao wa kidini. Ni mrpango kabambe, lakini wako kwenye njia sahihi kwa sababu baadhi ya wanawake walioshiriki katika mkutano wao tayari ni sehemu ya mitandao na pale ambapo hakuna wangependa kuwatangazia au kuwatia moyo ili basi waweza kujenga mtandao wa kimataifa.