Tafuta

26 .01.2023: Papa akutana na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu wanawake  wajenzi wa tamaduni za kukutana. 26 .01.2023: Papa akutana na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu wanawake wajenzi wa tamaduni za kukutana.  (Vatican Media)

Papa Francisko:dini zinachangia utamaduni wa kukutana

Kwa hakika kukaa na kusikiliza mwingine,tabia ya kukutana kibinadamu ni mfano wa tabia ya kukaribisha,ya kushinda kujipendelea na kumpokea mwingine,kwa kumpatia umakini,kutengeneza nafasi katika mzunguko binafsi.Ni ushauri wa Papa kwa washiriki wa Mkutano wa kimataifa kuhusu 'wanawake wajenzi wa tamaduni za kukutana kiimani'.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican tarehe 26 Januari 2023 na Wajumbe washauri wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu “Wanawake Kujenga Utamaduni wa Kukutana Kiiimani” ambapo amemshukuru Rais wa Umoja wa Mashirika ya Watawa wa kike katoliki duniani. Katika hotuba yake, Papa amewakaribisha kwa namna ya pekee watoa mada ya Mkutano huo uliongozwa na mada hiyo ya  wanawake ambao wanajenga utamaduni wa kukutana kidini. Amewapongeza kwa kuanzisha mpango huo.

Papa na washiriki wa Mkutano Kimataifa kuhusu wanawake wajenzi wa kukutana
Papa na washiriki wa Mkutano Kimataifa kuhusu wanawake wajenzi wa kukutana

Papa amesema sio tukio la kawaida kwa  waamini wa dini 12 duniani kote kuungana  na kujadiliana kuhusu masuala msingi yanayohusu  kukutana na kujadili kuhusiana na  kuhamasisha amani na uelewa katika Ulimwengu wetu uliojeruhiwa. Na wakati mkutano wao umejikita katika kusikiliza uzoefu na matarajio ya wanawake,  na kwamba una  maana kubwa tena. Kiukweli amani inapaswa kutafutwa kwa kuhusishwa pakubwa wanawake. Kwa sababu wanawake wanatoa utunzaji na maisha ulimwenguni. Ni njia kuelekea amani” (Hotuba ya Papa huko astana 15 Septemba 2022).

Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano wa kimataifa kuhusu wanawake wajenzi wa kukutana
Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano wa kimataifa kuhusu wanawake wajenzi wa kukutana

Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa Kanisa Katoliki limejikita katika majadiliano ya kidini na katika kuhamasisha uelewa na ushirikiano kati ya waamini wa tamaduni nyingi za kidini. Kila mmoja wa tamaduni hizi na kila mmoja wao binafsi ana utajiri wa kutoa ulimwenguni, kwa kueneza roho moja ya makaribisho, ya kutunza na ya udugu. Sehemu kubwa ya waliokuwa kwenye mkutano huo imehusika kugundua mantiki ya kike katika tamaduni zao za kidini na kuonesha zenyewe jinsi zinavyochangia utamaduni mmoja wa kukutana. Kiukweli kukaa na kusikiliza mwingine, tabia ya kukutana kibinadamu ni mfano wa tabia ya kukaribisha, ya kushinda kujipendelea na kumpokea mwingine, kwa kumpatia umakini, kutengeneza nafasi katika mzunguko binafsi.  Papa ametoa onyo kuwa Shughuli za makutano na ufunguzi unaohitajika, unaanza kupotea na  wakati uzoefu wake ni moja ya zawadi kubwa ambazo wanaweza kutoa katika familia zao, jumuiya za ona jamii.

Baba Mtakatifu Francisko amewatia moyo katika umuhimu huo wa kushirikiana  na kushikirishana dhamiri ya uzoefu wa matendo. Hayo yanatoa nguvu na ubunifu ikiwa katika miktadha yao, inafanya kazi kwa ajili ya kutoa msaada kwa watu wengi wanaotafuta nafuu katika mateso na zaidi  sana maana na mtindo katika maisha yao. Kutokana na hilo  Papapa Francisko ameapongeza kwa juhudi zao na nguvu zao wanazozitoa katika kuhamasisha hadhi ya wanawake kwa namna ya pekee wasichana.

Papa na washiriki wa mkutano wa kimataifa wa madhehubu ya kidini
26 January 2023, 15:53