Tafuta

2021.08.26 Jezi ya wanamichezo Vatican 2021.08.26 Jezi ya wanamichezo Vatican 

Vatican:Jezi za wawakilishi wa mchezo kwa wafanyakazi Vatican zinauzwa

Jezi za wawakilishi wa michezo kwa wafanyakazi wa Vatican zinauzwa na fedha itakayopatikana ni kwa ajili ya ufadhili wa wenye kuhitaji na kwa maana hiyo inaingia kwenye mfuko wa kitume wa kipapa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Inawezekana hatimaye kununua kupitia majumba ya makumbusho na duka la nguo katika katika  serikali ya mji wa Vatican,  jezi rasimi ya uwakilishi wa michezo kwa mpira wa miguu, kwa wafanyakazi wa Vatican. Yote hayo yamewezekana, shukrani kwa kazi kubwa ya Viongozi wa Chama ,lakini hasa kwa kuangazwa mmoja wa wakuu hao ambaye wakati wa janga la Uviko-19 alifikiria kuzindua changamoto hii nzuri!

Kardinali Comastri akipokea Jezi ya wanamichezo Vatican
Kardinali Comastri akipokea Jezi ya wanamichezo Vatican

Ni  seti nzima ikiwa na mfuko pia kofia rasimi, ambapo fedha zitakazopatikana zitakwenda kwenye Mfuko wa upendo wa kitume wa  Papa kwa ajili ya wenye kuhitaji zaidi.

Kofia ni sehemu ya jezi ya wanamichezo Vatican
Kofia ni sehemu ya jezi ya wanamichezo Vatican

Wazo hili hata hivyo limekutana na hamu kubwa ya wengi. Mtu wa kwanza kupokea zawadi hii ya jezi namba moja ni Papa Francisko ambaye aliipokea tangu tarehe 23 Juni 2021 wakati wa kumaliza katekesi yake. Ukabidhishwaji wa jezi hizi rasimi kama zawadi kwa makardinali, maaskofu na wakurugenzi mbali mbali wa Mabaraza ya kipapa umeendelea na bado unaendeleoa kama ishara ya kuonesha shukrani kubwa kwa ajili ya msaada uliopokelewa katika mchakato wa miaka hii na kuonesha hasa utashi wa kuendeleza katika shughuli za michezo, kwa ajili ya ufadhili, urafiki na utumaduni wa mazungumzo na kukutana.

Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican Dk Ruffini akipokea jezi
Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican Dk Ruffini akipokea jezi
Mfuko ni sehemu ya jezi ya wanamichezo Vatican
Mfuko ni sehemu ya jezi ya wanamichezo Vatican

Shughuli za michezo zitaanza mwezi Septemba ujao kwa ushiriki wa Michezo ya karafiki na goli kwa ajili ya Hospitali ya watoto katika hukusanyai wa fedha kwa ajili ya kitengo cha hospitali ya watoto katika mfuko wa Mtakatifu Matayo na mfuko wa Mondini huko Pavia Italia. Itafuata baadye michuano ya mashirika mwengine ya mpira wa mikuu kwa wanaume na wanakea wa  Bambino Gesù, kwa  kuwania kikombe cha Vatican na kikombe bora cha Vatican, na mwishowe katika  Siku ya Familia.

T-shirt na kofia ya wanamichezo Vatican
T-shirt na kofia ya wanamichezo Vatican
27 August 2021, 16:29