Tafuta

2021.08.13 Ibada ya Mazishi ya Kardinali Edoardo Martinez Somalo 2021.08.13 Ibada ya Mazishi ya Kardinali Edoardo Martinez Somalo 

Kard.Martínez Somalo alipenda Kanisa kwa akili na wema

Kardinali Battista Re,Dekano wa makardinali ameongoza misa ya mazishi ya Kardinali Eduardo Martinez Somalo(94)aliyefariki tarehe 9 Agosti mjini Vatican.Katika mahubiri yake amesema alikuwa ni mtu wa amani,mkarimu,mwenye akili sana na uwezo mkuu wa kutathimini mambo na alijitoa kwa Kanisa na kushirikiana na mapapa ambao aliwapenda kwa moyo wote na kuwapa ushirikiano wa kina.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Misa ya Maziko ya Kardinali Edoardo Martìnez iliyofanyika Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Peto Vatican tarehe 13 agosti 2021) imeongozwa na Kardinali Re, Decano wa Makardinali. Akianza tafakari yake katika masomo yaliyosomwa amesema, “somo lakwanza kutoka kitabu cha Hekima linakumbusha hatma baada ya kifo kinachowasubiri wenye haki na kuhakikisha kuwa hayo ni maisha ya milele na yenye furaha ambayo wanatunikiwa kwa kadiri ya matendo na majaribu yaliyokabiliwa wakati wa maisha yote. “Roho za wenye haki ziko katika mikono ya Mungu (Hekima 3,1). Kwa maana hiyo roho ya Kardinali Eduardo Martìnez Somalo sasa ipo mikononi mwa Mungu. Anapumzika kwa amnai. Matumaini yake ni timilifu katika uzima”. Sura ya Injili ambayo imesoma, imekumbusha kuwa Bwana wa historia na mioyo ambayo ipo katika ardhi hii ni kwa sababu isije potea kwa kile ambacho Baba alimkabidhi, na hata mwisho wa hija ya maisha yetu hapa duniani, tunasubiri uso wa huruma ya Mungu. “Haya ndiyo mapenzi ya Baba yangu, kila amwonaye Mwana na kuamini Yeye awe na uzima wa Milele na mi nitamfufua siku ya mwisho (Yh 6, 37-40). Ahadi hii ya Kristo inafungua moyo mkuu wa matumaini, kwa waamini katika hali halisi ya kifo; ni mapito kutoka katika dunia hii na kwenda katika nyumba ya Baba; ni kuingia katika upendo wa kina wa Mungu.

Kwa uhakika na  kwa matumaini aliishi na amezimika hivyo Kardinali Edoardo Martinez. Alikuwa amezaliwa tarehe 31 Machi 1927 katika kijiji cha Banos de Rio Tobìa. Mnoamo 1954 alipewa daraja la upadre kwa jimbo la Calahorra y La Calzada-Logrono, nchini Uhispania lakini katika jimbo lake, alitoa huduma yake ya kikuhani kwa miezi michache tu.  Maisha yake yote yalikuwa katika huduma ya Baba Mtakatifu, Vatican na kwa Kanisa la Ulimwengu. Katika nyadhifa mbali mbali alizopewa na kwa muda mrefu alikabidhiwa kwa imani ya Mama na kwa kumtambua kuwa ni mmoja wa roho nje ambayo ilijaa uaminifu kwa Papa na mkarimu wa kujitoa kwa ajili ya wema wa Kanisa na kwa ajili ya wokovu wa roho. Alikuwa ni mwanamme wa amani, mkarimu, mwenye akili sana na uwezo mkuu wa kutathimini mambo na alijotoa kwa Kanisa na kushirikiana na mapapa ambao aliwapenda kwa moyo wote na kuwa na muungano nao. Baada ya mafunzo ya elimu ya Kikanisa, mwaka 1956 aliingia katika nafasi ya kidiplomasia ya Vatican na kuanza huduma yake katika Ofisi ya Katibu wa Vatican katika kitengo cha lugha ya kisipanyola, ambapo alikuwa huduma na wakati huo huo kuwa na shughuli ya Profesa wa Tasisi ya Kipapa ya Mafunzo ya Kinisa kwa lugha ya kispanyola. Mwanzo wa mwaka 1970 aliteuliwa kuwa mshauri wa Mwakilishi wa Kitume Uingereza, lakini uwepo wake mbali na Roma ulidumu kwa miezi michache kwa sababu mwezi Oktoba mwaka huo aliitwa Vatican kuwa mkaguzi wa ofisi ya Katibu na wakati huo mhudumu wa moja kwa moja wa Katibu msaizidi wa Vatican, Askofu Mkuu  Giovanni Benelli.

Tarehe 12 Oktoba 1975 Papa Paulo VI alimchagua kuwa Balozi wa Kitume wa Colombia, kwa maana hiyo moja kwa moja kuwa Askofu Mkuu. Kama moto ya kiaskofu alichagua “Caritas et veritas”, maneno mawili ambayo yalimwongoza katika maisha yake yote na ambayo yalimwelekeza kazi yake ya kutenda. Mnamo maka 1979 Mtakatiuf Yohane Paulo II alitaka awe mhudumu wake wa Karibu na Kumchagua kuwa Katibu Msaidizi wa Vatican kwa miaka 9 kwa kuongozwa na matendo mema na Papa katika kutimizwa utume na mipango ya kitume. Mnamo 1992 Papa alimchagua kuwa mwakilishi wa Kongamano la Kimatafia la mama Maria huko Huelva, Hispania.  Tarehe 5 Aprili 1993, Papa Yhnae Paulo II alimakabidhi kuwa Camerlengo wa Kanisa Katoliki hasa nafasi kubwa sana ya hekima katika ambayo iko katika Katiba ya Kitume Universi Dominici Gregis.

Baada ya kutumiza miaka 85/86 nguvu zilianza kupungua na hakuweza kutoka nje ya makao yake, lakini akiwa nyumbani alikuwa akifuatilia kwa uhai wote na ushiriki wa matukio ya Kanisa. Aliweza kuendelea na maisha kama kawaida na furaha, shukrani kuu kwa huduma ya Watawa wamisionari wa Shirika la Yesu Kuhani milele na ambao kwa hakia walimsaia kila wakati, katika misa zake za kial siku asubuhi na wakati wa siku walikuwa wakisali kwa pamoja na yeye.  “Kila wakati nilipokwenda kumtembelea, nilipenda utulivu wake, utulivu na kuamini kutelekezwa kwa Mungu. Mwisho wa mazungumzo yetu mara nyingi alirudia sala ambayo alikuwa akijua: kufanya kila kitu; Najiaminisha Kwako kwa sababu unajua kila kitu; Ninajikabidhi kwako, Yesu, kwa sababu Unanipenda licha ya kila kitu ”. Na alikuwa akisisitiza kwamba "licha ya kila kitu”.

Hali yake kiafya ilikuwa inazidi kuwa mbaya kwa karibu miezi mitatu. Alilazwa hospitalini kwa takriban siku kumi huko Gemelli, na kisha akarudi nyumbani kwake Vatican, ambapo alipokea msaada na huduma zote zinazohitajika. Baba Mtakatifu Francisko alikwenda kumtembelea na kumpa faraja na baraka zake wiki moja iliyopita. Kardinali Martinez alikubali kupungua kwake polepole akiwa katika kitanda chake lakini bila kuipnga mapenzi ya Mungu, akiungwa mkono na tumaini kuu la Kikristo. Kila wakati alikuwa akitoa maneno ya shukrani kwa Masista wake na kwa wale ambao kwa ukarimu walijitahidi kumsaidia. Ushuhuda wake wa upenda kwa Kirisro na ulioynfa mzizi kwa maana ya kikanisa, Kardinali Martines ameacha urithi mkubwa wa kuhifadhi kama pia mfano kwa ibada ya bikira Maria. Karidinali Giovanni Battista Re amehitimisha akiomba kuzidi kumwombea roho yake ipumzike kwa amani.

13 August 2021, 15:43