Tafuta

2021.08.10 Kardinali  Eduardo Martínez Somalo 2021.08.10 Kardinali Eduardo Martínez Somalo 

Papa atuma salamu za rambi rambi kwa kifo cha Kard.Eduardo M.Somalo

Papa Francisko tarehe 11 Agosti ametuma salamu za rambi rambi kufuatia na kifo cha Kardinali Eduardo Martinez Somalo (94)na ambaye alikuwa amemtembelea kumwona Jumatano iliyopita.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko Jumatano tarehe 11 Agosti 2021 ametuma salamu za rambi rambi katika telegram iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin katibu wa Vatican, kufuatia na kifo cha Kardinali Eduardo Martinez Somalo kilichotokea  tarehe 10 Agosti 2021 ambaye alizaliwa huko  (Baños de Río Tobía, tarehe 31 Machi 1927) kwa maana hiyo akiwa na umri wa miaka 94  katika nyumba za kipapa Vatican. Telegram iliyotumwa kwa Monsinyo Fernando Loza Martinez katika Jumba moja Vatican, Papa anaonesha masikitiko kupokea habari za kifo cha Mjomba wake Kardinali Somalo

Papa kwa maana hiyo amependa kuelezea ukaribu wake, familia yake na wale ambao walimjua huku akiukumbuka kwa upendo na sifa  juu ya ushuhuda wa kiroho wenye matunda ya  mpendwa ndugu huyo. Kwa kufikiria kwa dhati, na mshangao wa muda mrefu na utajiri wa uzoefu alioupata, anakumbusha ushirikiano mzuri alioufanya mapapa sita ambao walimkabidhi kazi muhimu sana. Anashukuru Bwana kwa uaminifu wake na mkarimu katika utoaji wa huduma ya Kanisa na kwa Vatican.

Papa anamwomba Bwana na kwa maombezi ya mama Bikira Mtakatifu, kumpokea katika nyumba ya mbinguni ili aweze kupunzika katika heri, mwaaminifu, mhudumu wa Injili. Kwa moyo wa kina Papa amewabariki kwa baraka ya kitume wale wote ambao wanaomboleza kuondoka kwake, hasa wazo maalum limewaendea watawa wakimisionari wa Yesu Kuhani Milele ambao wamemhudumia kwa upendo mkuu.

Kardinali Eduardo akiwa na Papa Yohane Paulo II
Kardinali Eduardo akiwa na Papa Yohane Paulo II

Kardinali Somalo amezimika roho yake akiwa mjini Vatican na umri wa miaka 94, asili yake ni mhispania. Katika uhai wake aliwahi kushika nafasi mbali mbali za uongozi na miongoni mwake kuwa Rais wa Baraza la Kipapa wa Mashirika ya kitawa na Vyama vya Kitume. Vile vile anakumbukwa wakati wa wa kipindi kifo cha Papa Yohane Paulo II mnamo 2005 alichukua nafasi msingi kama ile ya kuwa camerlengo na kitovu cha ufunguo wa Vatican tangu akiwa Padre kijana.

11 August 2021, 15:44