Tafuta

Kardinali Wilfrid Fox Napier ameng'atuka kutoka madarakani na Papa Francisko amemteuwa Askofu Siegfried Mandla Jwara kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo kuu la Durban, Afrika ya Kusini. Kardinali Wilfrid Fox Napier ameng'atuka kutoka madarakani na Papa Francisko amemteuwa Askofu Siegfried Mandla Jwara kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo kuu la Durban, Afrika ya Kusini. 

Askofu mkuu Siegfried M. Jwara, Jimbo Kuu la Durban A. Kusini

Askofu mkuu Siegfried Mandla Jwara alizaliwa tarehe 1 Februari 1957. Baada ya masomo na majiundo yake ya kipadre na kitawa, kunako mwaka 1986 akaweka nadhiri zake za daima. Tarehe 14 Februari 1987 akapewa Daraja takatifu ya Upadre. Tarehe 30 Aprili 2016, akateuliwa kuwa Askofu wa Vikarieti ya Ingwavuma, Afrika ya Kusini na kuwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 25 Juni 2016.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Kardinali Wilfrid Fox Napier, O.F.M., la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo, Baba Mtakatifu amemteuwa Askofu Siegfried Mandla Jwara, C.M.M. (Congregation of Mariannhill Missionaries) kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo kuu la Durban, nchini Afrika ya Kusini. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Siegfried Mandla Jwara, C.M.M. alizaliwa tarehe 1 Februari 1957 huko St. Nivard, nchini Afrika ya Kusini. Baada ya masomo na majiundo yake ya kipadre na kitawa, kunako mwaka 1986 akaweka nadhiri zake za daima.

Tarehe 14 Februari 1987 “Siku ya Wapendanao”, akapewa Daraja takatifu ya Upadre. Tarehe 30 Aprili 2016, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu wa Vikarieti ya Ingwavuma, Afrika ya Kusini na kuwekwa wakfu kuwa Askofu hapo tarehe 25 Juni 2016. Ilipogota tarehe 9 Juni 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Durban, Afrika ya Kusini. Katika maisha yake kama Padre amewahi kuwa Mlezi wa Wanovisi, Gambera wa Seminari ya Merrivale na Mshauri wa Mkuu wa Kanda ya Shirika la Wamisionari wa Mariannhill. Na kati ya mwaka 1998 hadi mwaka 2002 alichaguliwa kuwa ni Padre Mkuu wa Kanda na kurudia tena wadhifa huu kati ya mwaka 2006 hadi mwaka 2009.

Durban Afrika ya Kusini

 

 

11 June 2021, 16:09