Tafuta

2021.04.23 Papa alitembelea watu waliokuwa wanapewa chanjo katika Ukumbi wa Paulo VI 2021.04.23 Papa alitembelea watu waliokuwa wanapewa chanjo katika Ukumbi wa Paulo VI  

Vatican:watu wengine 300 wamepewa chanjo dhidi ya Covid

Katika Ukumbi wa Paulo VI,watu wasiokuwa na makazi,wadhaifu na walio katika mazingira magumu wamepata chanjo kwa mujibu wa msemaji wa Mfuko wa Sadaka ya Kiitume.Hata hivyo kampeni ya “chanjo iliyosimamishwa",inaendelea ili kusaidia Nchi zilizoko kwenye shida ya janga kama vile India na Siria.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ombi ambalo lilikuja kwa hiari kutoka kwa watu wengi wanaoishi mitaani, ambalo lilipokelewa kwa ukarimu wa Papa ili kusaidia walio katika mazingira magumu zaidi na pia wale walio wazi zaidi kupata maambukizi ya virusi vya Corona linaendelea kutoa matunda mema. Kardinali Konrad Krajewski, Msimamizi wa Sadaka ya Kitume ya Papa ameeleza jinsi ambavyo tangu wiki mbili katika kliniki ya Mama wa Huruma, iliyoko kwenye nguzo za Mtakatifu Petro, inaendelea kwa dhati  kutoa mshikamano wa wale ambao kwa kawaida hawana uwezo wa kupata chanjo kwa haraka.

Kutokana na hilo pia Jumamosi  tarehe 8 Mei 2021 watu wengine 300 wamekaribishwa katika Ukumbi wa Paulo VI, Vatican na wapewa chanjo. Hawa ni watu ambao kwa kawaida hawasaidiwi na mashirika yanayofanya kazi katika maeneo ya jiji, kama ilivyotokea katika wiki za hivi karibuni kwa takriban ya watu maskini 1,400 waliopewa chanjo jijini  Vatican.

Toa mchango wako katika kampeni ya "chanjo iliyosimamishwa"

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Mfuko wa Sadaka ya Kitume, ameelezea vile vile hatua nyingine iliyoanzishwa ya kampeni ya Chanjo iitwayo “ Chanjo iliyosimamishwa”na ambayo imekaribishwa kwa kiasi kikubwa zaidi ya matarajio yote. Kutoa zawadi katika kipindi cha matatizo siyo kitu rahisi, kwani kinahitaji moyo  na kwa maana ni thamani msingi na neema ambayo kwa mchango mdogo unaoweza kutolewa unaweza kusaidia wale walio na mahitaji zaidi; na ni shukrani pia kwa mchango wako mdogo, unaweza kutolewa kupitia  tovuti: www.elemosineria.va ili uweze kuwa na mshikamano katika ulimwengu unaoendelea kuteseka sana na virusi.

Kwa mfano India, nchi iliyoathiriwa vibaya sana na wimbi la pili la janga  na ambalo Papa  Francisko ametoa wito wake  akionesha ukaribu wake , amepokea  dola 200,000 za kuweza kutumika katika vita dhidi ya Covid.  Kwa upande wa Sria,ambayyo pia ni nchi nyingine iliyo na mzozo usio na mwisho pia na virusi wa corona, imepokea euro elfu 350. Kwa mujibu wa msimamaizi wa Sadaka ya Kitume ameeleza kuwa michango yote inakabidhiwa katika Ubalozi wa Kitume wa Vatican mahalia ambao baadaye huwasambazia kulingana na mahitaji.

Kushiriki muujiza wa hisani

Mnamo tarehe 23 Aprili 2021 , katika fursa ya  sikukuu ya Mtakatifu George na siku ya Somo wa Papa,  Baba Mtakatifu Francisko alikuwa amewashangaza watu takriban 600 wanaohitaji ambao walipokea kipimo cha pili cha chanjo ya Pfizer-Biontech. Kiwango cha kwanza kilichukuliwa wakati wa Wiki Takatifu na hivyo kutoa tena wito wa Papa ili pasiwepo mtu aliyetengwa kwenye kampeni ya chanjo dhidi ya virusi vya corona.

08 May 2021, 16:25