Tafuta

Kardinali Parolini katika Misa kwenye Altare ya Kanisa Kuu La Mtakatifu Petro Kardinali Parolini katika Misa kwenye Altare ya Kanisa Kuu La Mtakatifu Petro 

Kard Parolin kuwakilisha Papa huko Strasburg,kwa mia 1300 tangu kifo cha Mt.Odile

Papa Francisko amemchagua Katibu wa Vatican kuwa kama mwakilishi wake katika maadhimisho ya Sherehe za Msimamizi wa Alsace zitakazofanyika katika Kanisa Kuu katika Jimbo Kuu mnamo tarehe 4 Julai ijayo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Baba MtakatifuFrancisko amemteua Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican kuwa mwakilishi wake ili kushiriki maadhimisho ya Ekaristi takatifu  ambayo itafanyika tarehe 4 Julai 2021 katika Kanisa Kuu la Strasburg,  katika fursa ya miaka 1300 tangu kifo cha Mtakatifu Odile, Msimamizi wa Alsace.

Mtakatifu  Odile, Msimamizi wa Alsace

Alizaliwa kwenye mwaka wa 660 na kifo chake mnamo mwaka 720, ambapo jina la mtakatifu Odile linamaanisha “ mwanga wa Mungu”, na alikuwa anatoka katika  familia nzuri ya Wamerovingian. Akiwa kipofu  tangu utoto wake , aliponywa kimiujiza wakati wa Ubatizo wake, alioupokea akiwa na miaka 15. Baadaye akawa mtawa na kuanzisha monasteri katika Jumba la kifalme  la Hohenbourg, lililoko kwenye mlima ambao baadaye uliitwa jina lake, Mlima wa Mtakatifu Odile na ambao kiukweli ni mahali maarufu kwa hija na utalii huko Alsace. Alitangazwa kuwa mtakatifu na Papa Leo IX katika karne ya 11, na alitangazwa kuwa msimamii wa Alsace na Papa Pius XII mnamo 1946, mwaka mmoja baada ya kumalizika kwa Vita vya pili vya Kidunia  ambavyo vilijaribu sana eneo hilo, lililounganishwa na Ujerumani wa Nazi. Kuanzia tarehe 13 Desemba 2020, Jimbo katoliki la Strasbourg limezindua Jubilei Kubwa ya maadhimisho ya miaka 1300 tangu kifo cha Mtakatifu Odile.

Umaalum wa udini  wa Alsace

Jimbo la  Strasbourg, kama vile jimbo  jirani la Metz, lina umaalum wa kutumia sheria za makubaliano ya Kinapoleon. Makuhani wanalipwa na serikali na maaskofu walioteuliwa kwa pamoja na Papa na Rais wa Jamhuri, na kuchapishwa katika Jarida la Ofisi. Majimbo haya mawili kwa makubaliano yalikuwa yametembelewa na Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo 1988. Kwa upande wake, Baba Mtakatifu Francisko alifanya ziara fupi huko Strasbourg mnamo Novemba 2014, kwa kufanya hotuba mbili katika Bunge la Ulaya na Baraza la Ulaya.

04 May 2021, 15:54