Tafuta

Wapalestina waandamana dhidi ya  mapigano ya mpaka wa Israeli na Gaza Wapalestina waandamana dhidi ya mapigano ya mpaka wa Israeli na Gaza 

Kard.Parolin:Ni udharura wa kusitisha ghasia katika mzozo Mashariki ya Kati

Katibu wa Vatican ameelezea wasi wasi wa Papa na Makao makuu Vatican kwa ujumla kutokana na kuongezeka kwa ghasia kati ya Israeli na Hamas:"Mzozo huu unaleta magofu na vifo pia nitamwalika Ursula von der Leyen aunganishe kila juhudi”.Amesema Katibu wa Vaticsn kando ya uwasilishaji wa kitabu cha kumbukumbu ya aliyekuwa mkurugenzi wa Osservatore Romano.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Ni wasi wasi mkubwa wa Papa na Makao makuu Vatican juu ya kile kinachotokea katika Ardhi Takatifu ambapo inazidi kuongezeka kwa vurugu kati ya Israeli na Hamas. Hayo yameelezwa na katibu wa Vatican, Kardinali, Pietro Parolin, kando ya uwasilishaji wa kitabu ambacho wamemkumbuka mkurugenzi wa zamani wa Osservatore Romano, Mario Agnes, kilichosainiwa na mwandishi wa habari Ignazio Ingrao, katika Jumba la Borromeo, ambacho ni  kiti cha Ubalozi wa Italia jijini Vatican. Kardinali Parolin amesisitiza udharura wa maafikiano na ameelezea juu ya wasiwasi mkubwa wa  hali hii ya ushawishi, ambayo inaendelea licha ya juhudi za jumuiya ya kimataifa  ya kutaka kuleta usitishaji wa mapigano hayo.

“Mzozo huo unaleta magofu na vile vile vifo, amesema Kardinali Parolin. Na amekumbuka maneno ya Papa Francisko mra baada  ya Sala ya Malkia wa Mbingu  siku ya Jumapili tarehe 16 Mei, wakati alipotoa umakini wa ulimwengu hasa  juu ya watoto waliokufa. “Wasiwasi wetu ni ule wa Baba Mtakatifu na kujitoa kufanya kila linalowezekana ili kumaliza mzozo huo”, amesema Katibu wa Vatican.

Kardinali Parolin akijibu maswali ya waandishi wa habari ambao waliuliza ikiwa Vatican  inaweza kufanya kama mpatanishi wa suala la Israeli na Palestina amejibu kwamba: “Nadhani kuna mtu ameambiwa kwamba hawataki kuingiliwa. Kwa maana ya kiufundi labda sio, na sidhani kama ni sawa namna hiyo. “Lakini kwa hakika lazima tuchukue hatua yoyote ambayo inaweza kusaidia kwanza kusitisha mapigano, na kumaliza mzozo huu wa muda mrefu, na kufikia azimio kulingana na suluhisho la serikali mbili”.

Kardinali Parolin anatarajia kuwa na mkutano Jumamosi ijayo  ambapo ni kati ya Papa na rais wa Tume ya Ulaya, Bi Ursula von der Leyen, ambaye pia kama Katibu wa Vativan atapata fursa ya kukutana naye. Kardinali amesema itakuwa fursa mpya kujadili mgogoro huo: “Kiukweli nitazungumza naye juu ya suala la Israeli na Palestina. Tutalazimika kuunganisha pamoja guvu ili kutafuta kumaliza mgogoro huu”.

18 May 2021, 19:17