Tafuta

Vatican News
Padre Hans Zollner Padre Hans Zollner 

Taasisi mpya katika mapambano dhidi ya manyanyaso ya watoto&watu wazima!

Rais wa Kituo cha Ulinzi wa Watoto cha Chuo Kikuu Cha Kipapa Gregoriana,Roma,Padre Hans Zollner anaelezea sababu zilizopelekea uundwaji wa Taasisi Mpya ya Atholpolojia kwamba ni katika kazi na jitihada za miaka hii kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kiakili na kupambana dhidi ya kila aina ya vurugu na unyanyasaji wa kila aina.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Rais wa Kituo kwa ajili ya Ulinzi wa watoto cha Chuo Kikuu ca Kipapa cha (CCP), Padre Hans Zollner ameelezea umuhimu wa mambo ambayo yamepelekea kuwa na mabadiliko ya kituo hicho kuwa Taasisi Mpya ya Anttholopojia, ambayo itakuwa na mafunzo ya kisayansi kuhusu hadhi ya mwanadamu na juu ya utunzaji wa watu walioathirika, (IADC).  Ni suala ambalo wapendelea wakuu wa taaluma na kuridhiwa na Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki, ambapo si katika kutazama jina tu bali ni ule ukina wake kama alivyothibitisha Padre huyo na mjumbe pia wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto. Kwa mujibu wa maelezo yake amesema kuna sababu mbili ya mabadiliko hayo. Awali ya yote, ni kwamba Kituo chao cha Ulinzi wa Watoto CCP hapo awali kisingeweza kuwa na wafanyakazi wake wa kufundisha na kutoa digrii zake za kitaaluma. Kwa sasa, kutokana na mabadiliko kuwa Taasisi ya Anthologia, itawezekana kufanya hivyo, kwa njia ambayo waalimu na maprofesa wataweza pia kukua zaidi na zaidi. Sababu ya pili ni kwamba wakati walipoanza, karibia miaka tisa iliyopita, nia ya kituo hicho (CCP), ilikua inajikita zaidi juu ya manyanyaso ya watoto, na wakati kwa miaka minne iliyopita wameona mabadiliko makubwa, maoni ya umma na katika Kanisa ambalo limejumuishwa hata watu wazima waliaathirika. Na kwa maana hii walitakiwa kubadilika na kufanya jambo muhimu zaidi la kitaaluma.

Kwa maana hiyo kama Taasisi lazima wakue na kuhamasisha  watu wenye uwezo wa kuwa profesa, watu ambao wamekwisha kufanya utaaluma hiyo katika kituo hicho (CCP). Lakini si hao tu pia hata wale ambao walikuwa wanaendeleza katika vituo vingine vya elimu kwa mantiki hiyo. Kwa sasa wanaendelea kufanya kazi katika nyanja mbali mbali zilizojitokeza hivi karibuni kama vile: unyanyasaji wa kiroho, katika muktadha wa ushauri au mwelekeo wa kiroho, unyanyasaji wa watawa katika sehemu nyingine za ulimwengu, shida kubwa iliyoshutumiwa na Baba Mtakatifu Francisko miaka mitatu iliyopita na  suala lote la uwajibikaji wa wakuu wa watawa  katika suala zima la manyanyaso. Malengo ambayo yanawekwa katika hali halisi hii, Padre Padre Hans Zollner  amethibitisha kuwa wataendelea na  hatua zao za masomo na kwa hatua zote wanazofanya kwa kushirikiana na taasisi nyingine kama vile Mabaraza  ya Maaskofu au Wakuu Mashirika ya Dini. Lakini juu ya yote, kama Taasisi ya Chuo Kikuu, wanataka kuendeleza zaidi utafiti juu ya mada maalum: kwa mfano, jinsi gani dini na taaluma mbali mbali za kielimu zinaweza kushirikiana ili kuongeza jitihada za kuzuia unyanyasaji.

Vile vile amebainisha kuhusu masomo hayo jinsi yalivyo na jinsi ambavyo yataendeshwa,  kwamba inapaswa hata hivyo kusisitizwa kuwa programu zao ni tatu kuu. Moja inajikita kwa ujifunzaji wa umbali ambao wanatoa kwa taasisi nyingi za kimataifa. Halafu kuna programu za diploma, kwa lugha ya Kiingereza na Kispanyola, ambazo zitachukua miezi sita na ambazo zinalenga watu wanaofanya kazi katika ofisi za majimbo au mashirika ya  kidini. Mwishowe, ambayo ni leseni, yaani ni shahada ya pili kwa mujibu wa mzunguko wa chuo kikuu, ambayo itashughulikiwa na wale ambao wanahudumu katika Kanisa salama kwenye Mashirika ya kitawa  na mabaraza ya  maaskofu. Kwa kuongezea, pia kuna uwezekano wa kutoa digrii ya anthropolojia ambayo itajumuisha masomo ya taaluma mbali mbali. Kimsingi Taasisi mpya ni zana muafaka zaidi na muhimu kwa ajili ya Kanisa lote na ambalo linatoa mwanzo mpya. Ni huboreshaji kielimu, na maendeleo ambayo pia yanawapatia uwezekano wa kushirikiana na mamlaka kubwa na washirika wao wa masomo. Vile vile ni muhimu kujitoa kwa ajili ya mabadiliko ya mawazo ya kiakili ili kuzui  unyanyasaji na dhuluma za aina mbalimbali  za kila wakati ambazo ziko kwenye vinasaba (DNA) vya kikanisa.

Kwa maana hii kuanzia tarehe Mosi Mei 2021, inaanza rasmi shughuli ya Taasisi Mpya ambayo hadi sasa ilikuwa imekabidhiwa Kituo cha Ulinzi wa Watoto, (Ccp) na sasa  kuwa Taasisi mpya ya Athropolojia. Muktadha wa taaluma hii itashughulika kwa kina hadhi ya binadamu na juu ya utunzaji wa watu waliothirika (Iadc). Kwa maana pana, Athropolojia ni uwanja wa maarifa ambao unashughulia sayansi nyingi za kibinadamu na asili za kila kona ya binadamu huyo. Taasisi Mpya ya Antropologia itakuwa katika Chuo Kikuu Cha Gregoriana, Roma, ambayo itapanua juhudi zake katika kazi ya ulinzi wa watoto na watu walio katika mazingira magumu na kuhamasisha mazingira salama ambayo yanazingatia heshima ya hadhi ya mwanadamu. Wakati huo huo itapanua kwa kina ukuu wa somo hili na utafiti na kwa wote wanafahamu jinsi gani ilivyo msingi kwa ajili ya kukabiliana na manyanyaso ndani na nje ya Kanisa au jamii.  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi Padre Nuno da Silva Gonçalves, anasema kwa hatua hii mpya inayoanza ni vema kumshukuru Padre Hans Zollner S.J. Mhusika wa Kituo cha Ulinzi wa Watoto na aliyehusika na Tume ya maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Ulinzi na Usalama wa watoto (ISC), vile vile ni mjumbe wa Tume ya Ulinzi wa Watoto (Ccp) kwa kazi yake tangu kuanza kwa kituo hicho mnamo 2012, na kumtakia matashi mema ya Taasisi mpya ya Anthropolojia”.

Aidha amependa kukumbuka na kuwashukuru wafadhili wote, wadau na washirika wote ambao kwa ukarimu, wamewezesha kazi iliyofanywa na Kituo cha Ulinzi wa Watoto na watu walioathiriwa kila siku kuzaa jambo hili muhimu. Shukrani inawaendee kwa kazi iliyofanyika kufikia wakati huo muhimu wa mabadiliko ambayo yanatoa mwanzo mpya wa Taasisi ya Athropolojia ya binadamu katika masuala ya ulinzi wa watoto.  Hata hivyo ikumbukwe, hivi karibuni   tarehe 15 Aprili 2021, Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki,  liliidhinisha Sheria za Taasisi hiyo mpya, ambayo inaundwa sasa na mfumo mpya wa taasisi kwa kazi iliyofanywa hadi sasa chini ya jukumu la CCP. Taasisi mpya kwa dhati itakuwa na wafanyakazi wake wa kufundisha na itatoa digrii za masomo, diploma na leseni katika Ulinzi wa Watoto na watu walioathirika, pia udaktari wa Anthropolojia.

30 April 2021, 12:49