Padre Hans Zollner Padre Hans Zollner 

Taasisi mpya katika mapambano dhidi ya manyanyaso ya watoto&watu wazima!

Rais wa Kituo cha Ulinzi wa Watoto cha Chuo Kikuu Cha Kipapa Gregoriana,Roma,Padre Hans Zollner anaelezea sababu zilizopelekea uundwaji wa Taasisi Mpya ya Antropolojia hii kuwa ni katika kazi na jitihada za miaka hii kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kiakili na kupambana dhidi ya kila aina ya vurugu na unyanyasaji wa kila aina kwa watoto na watu wazima.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Rais wa Kituo kwa ajili ya Ulinzi wa watoto cha Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana (CCP), Padre Hans Zollner ameelezea umuhimu wa mambo ambayo yamepelekea kuwa na mabadiliko ya kituo hicho kuwa Taasisi Mpya ya Anthropolojia ambayo itakuwa na mafunzo ya kisayansi kuhusu hadhi ya mwanadamu na juu ya utunzaji wa watu walioathirika, (IADC).  Ni suala ambalo wamependelea wakuu wa taaluma na kuridhiwa na Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki, ambapo si katika kutazama jina tu, bali ni ule unyeti wake kama alivyothibitisha Padre huyo na mjumbe wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto. Kwa mujibu wa maelezo yake amesema, kuna sababu mbili ya mabadiliko hayo: Awali ya yote, ni kwamba Kituo cha Ulinzi wa Watoto (CCP) hapo awali kisingeweza kuwa na wafanyakazi wake wa kufundisha na kutoa digrii zake za kitaaluma. Kwa sasa, kutokana na mabadiliko kuwa Taasisi ya Anthologia, itawezekana kufanya hivyo, kwa njia ambayo walimu na maprofesa wataweza pia kukua zaidi na zaidi. Sababu ya pili ni kwamba wakati walipoanza, karibia miaka tisa iliyopita, nia ya kituo hicho (CCP), ilikua inajikita zaidi juu ya  masuala ya manyanyaso ya watoto, na katika harakati za miaka minne iliyopita wameona maendeleo na mabadiliko makubwa, maoni ya umma na katika Kanisa ambazo zimejumuishwa hata watu wazima walioathirika. Kwa maana hiyo walitakiwa wao kubadilika na kufanya jambo ambalo ni muhimu zaidi la kitaaluma.

Kutokana na hilo, kama Taasisi lazima wakue na kuhamasisha  watu wenye uwezo wa kuwa profesa, watu ambao wamekwisha kufanya utaalam kupitia katika kituo hicho (CCP). Lakini si hao tu, pia hata wale ambao walikuwa wanaendeleza elimu katika vituo vingine vya elimu katika mantiki hiyo. Kwa sasa wanaendelea kufanya kazi katika nyanja mbali mbali zilizo jitokeza hivi karibuni kama vile: unyanyasaji wa kiroho na kwa maana hiyo  katika muktadha wa kutoa ushauri au mwelekeo wa kiroho, unyanyasaji kwa upande wa watawa katika sehemu nyingine za ulimwengu, shida kubwa ambayo ilishutumiwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa miaka mitatu iliyopita na  suala lote la uwajibikaji kwa wakuu wa mashirika ya kitwa  katika suala zima la manyanyaso ya kijinsia. Malengo yaliywekwa bayana, Padre Padre Hans Zollner  amethibitisha kuwa wataendelea na hatua zao za masomo na kwa hatua zote wanazofanya kwa kushirikiana na taasisi nyingine kama vile Mabaraza ya Maaskofu au Wakuu Mashirika ya kitawa. Lakini juu ya yote, kama Taasisi ya Chuo Kikuu, wanataka kuendeleza utafiti zaidi juu ya mada maalum: kwa mfano, jinsi gani dini na taaluma mbali mbali za kielimu zinaweza kushirikiana ili kuongeza jitihada za kuzuia unyanyasaji.

Padre Zollner vile vile amebainisha kuhusu masomo hayo jinsi yalivyo na jinsi ambavyo yataendeshwa,  kwamba inapaswa hata hivyo kusisitizwa kuwa programu zao kuu zitakuwa tat. Moja inajikita katika ujifunzaji wa umbali ambao wanatoa fursa kwa taasisi nyingi za kimataifa. Halafu kuna programu za diploma, kwa lugha ya Kiingereza na Kispanyola, ambazo zitachukua miezi sita na ambazo zinalenga watu wanaofanya kazi katika ofisi za majimbo au mashirika ya kidini. Mwishowe, ambayo ni leseni, yaani ni shahada ya pili kwa mujibu wa mzunguko wa chuo kikuu, ambayo itashughulikiwa na wale ambao wanahudumu katika Kanisa kwenye Mashirika ya kitawa na mabaraza ya maaskofu. Kwa kuongezea, pia kuna uwezekano wa kutoa digrii ya anthropolojia ambayo itajumuisha masomo ya taaluma mbali mbali. Kimsingi Taasisi mpya ni zana muafaka zaidi na muhimu kwa ajili ya Kanisa lote na ambalo linatoa mwanzo mpya. Ni huboreshaji kielimu,na maendeleo ambayo pia yanawapatia uwezekano wa kushirikiana na mamlaka kubwa na washirika wao wa masomo. Vile vile ni muhimu kujitoa kwa ajili ya mabadiliko ya mawazo ya kiakili ili kuzui  unyanyasaji na dhuluma za aina mbalimbali  za kila wakati ambazo ziko kwenye vinasaba (DNA) vya kikanisa.

Kwa maana hii kuanzia tarehe Mosi Mei 2021, inaanza rasmi shughuli ya Taasisi Mpya ambayo hadi sasa ilikuwa imekabidhiwa kwa  Kituo cha Ulinzi wa Watoto, (Ccp) na sasa  inakuwa Taasisi mpya ya Athropolojia. Muktadha wa taaluma hii itashughulikia kwa kina hadhi ya binadamu na juu ya utunzaji wa watu waliothirika (Iadc). Kwa maana pana, Athropolojia ni uwanja wa maarifa ambao unashughulia sayansi nyingi za kibinadamu na asili za kila kona ya binadamu huyo. Taasisi Mpya ya Antropologia itakuwa  Chuo Kikuu Cha Gregoriana, Roma, ambayo itapanua juhudi zake katika kazi ya ulinzi wa watoto na watu wazima walio katika mazingira magumu na kuhamasisha mazingira salama ambayo yanazingatia heshima ya hadhi ya mwanadamu. Wakati huo huo itapanua kwa kina ukuu wa somo hili na utafiti na kwa wote wanafahamu jinsi gani ilivyo msingi kwa ajili ya kukabiliana na manyanyaso ndani na nje ya Kanisa au jamii.  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi Padre Nuno da Silva Gonçalves, anasema kuwa hatua hii mpya inayoanza ni vema kumshukuru Padre Hans Zollner S.J. Mhusika wa Kituo cha Ulinzi wa Watoto na aliyehusika na Tume ya maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Ulinzi na Usalama wa watoto (ISC), vile vile ni mjumbe wa Tume ya Ulinzi wa Watoto (Ccp) kwa kazi yake tangu kuanza kwa kituo hicho mnamo 2012, na kumtakia matashi mema ya Taasisi mpya ya Anthropolojia”. https://childprotection.unigre.it/

https://childprotection.unigre.it/education-formation/

Kwa kuhitimisha amependa kukumbuka na kuwashukuru wafadhili wote, wadau na washirika wote ambao kwa ukarimu, wamewezesha kazi iliyofanywa katika Kituo cha Ulinzi wa Watoto na watu walioathiriwa kila siku kuweza kuzaa jambo hili msingi kabisa. Shukrani inawaendee kwa kazi iliyofanyika kufikia wakati huo muhimu wa mabadiliko ambayo yanatoa mwanzo mpya wa Taasisi ya Athropolojia ya binadamu katika masuala ya ulinzi wa watoto.  Hata hivyo ikumbukwe, hivi karibuni  tarehe 15 Aprili 2021, Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki,  liliidhinisha Sheria za Taasisi hiyo mpya, ambayo inaundwa sasa na mfumo mpya wa taasisi kwa kazi iliyofanywa hadi sasa chini ya jukumu la CCP. Taasisi mpya kwa dhati itakuwa na wafanyakazi wake wa kufundisha na itatoa digrii za masomo, diploma na leseni katika Ulinzi wa Watoto na watu walioathirika, pia udaktari wa Anthropolojia. Ka maelezo zaidi unaweza kusoma kwenye link hii: https://www.unigre.it/en/events-and-communication/communication/news-and-press-releases/

30 April 2021, 12:49