Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko ameongoza Misa Takatifu ya Pasaka, Jumapili asubuhi tarehe 4 Aprili 2021, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mahali ambapo mara baada ya Injili ametoa muda wa ukimya wa tafakari ya kina. Na baada ya misa Takatifu Papa Francisko ametoa ujumbe wa Pasaka wa “Urbi et Orbi” kwa ajili ya mji na ulimwengu mzima huku akisisitiza jinsi ambavyo leo hii tunasherehekea tukio ambalolinatupatia tumaini ambalo halitukatishi tamaa. “Yesu aliyesulubiwa amefufuka”. Video fupi inaonesha tukio lililokuwa linatendeka leo hii katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, licha ya vizuizi vilivyopo vya janga la sasa la ulimwengu.