Hija ya kitume ya Papa Francisko nchini Iraq:Mosul,udugu un nguvu mauaji
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Ikiwa ni siku ya tatu ya Papa Francisko nchini Iraq, Jumapili tarehe 7 Machi amejikita kusali kwa ajili ya waathirikwa wa vita huko Mosul. Video fupi inaonesha moja ya wakati muhimu sana na wenye mawazo makuu ya Papa Francisko nchini Iraq, ambayo imeona maombi kwa ajili ya watu walioathirika katika vita huko Mosul.
Ni mji ulioharibiwa na ghadhabu ya ISIL lakini ambao umeanza hatua kwa hatua za ujenzi mpya hata na uzoefu wa ushirikiano kati ya Wakristo na Waislamu. Papa Francisko katika kuelezea kilichotendeka wakati huo amesema ulikuwa ni ukatili ambaoi uliikumba na dhoruba kama hiyo isiyo ya kibinadamu. Kwa njia hiyo Papa amewakabidhi waathiriwa wote na marehemu kwa Bwana na wakati huo huo anawaombea pia watesi watubu.