Tafuta

Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro 

Mkutano mjini Vatican kuhusu itikadi kali za kidini

Umefanyika mkutano kwa njia mtandao kati ya mabaraza ya kipapa kwa siku mbili tarehe 26 na 27 Januari,ambao umeunganisha watalaam wa masuala ya kikiristo na kiislamu ili kukabiliana na majibu yatokanayo na imani hizo mbili kutokana na kuzuka kwa matukio kama hayo yanayohitaji suluhisho zinazoongozwa na udugu.

VATICAN NEWS

Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mazungumzo ya kidini tarehe 26 na 27 Januari wamekuwa na mkutano kwa njia ya mtandao na siyo kwa umma kwa kuongozwa na mada: “Itikadi kali za kidini. tafsiri na Majibu ya wakristo na waislamu. Katika mkutano huo walishiriki wataalam na viongozi wa masuala ya dini za kikristo na za kiislamu.

Katika mchakato wa mkutano huo wametathimini matukio  mbali mbali ya itikadi kali za kidini na vurugu, kusoma mizizi yake, njia za kueneza, pamoja na juhudi na mipango iliyopitishwa ili kukomesha na kuzuia mchakato huu. Mkutano unajikita katika kazi ya kudumu ya baadhi ya Ofisi za Vatican kwa ajili ya kuelewa hali hii ya kushangaza na kushirikiana katika kuhamasisha na kukuza utamaduni wa mazungumzo na udugu.

Katika maandalizi hayo wamchangia Ofisi ya Katibu wa Vatican, Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki, Baraza la Kipapa la Kahamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu na Taasisi ya Kipapa ya Mafunzo ya Kiarabu na Kiislamu.

28 January 2021, 15:40