Tafuta

2018.02.14 Papa wakati  anapakwa majivu katika Kanisa la Mtakatifu Sabina Aventino,Roma 2018.02.14 Papa wakati anapakwa majivu katika Kanisa la Mtakatifu Sabina Aventino,Roma 

Kutokana na Covid,inabadilisha ibada ya majivu

Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti imechapisha maandishi ambayo yanafafanua njia ambazo makuhani watatakiwa kufuata wakati wa maadhimisho ya kufungua Kwaresima:Itatakiwa kuvaa barakoa na kusoma kanuni ya kupaka majivu mara moja tu.

Na Sr. Angela Rwezaula, - VATICAN NEWS

Hali halisi ya kiafya inayosababishwa na ugonjwa wa virusi vya corona unaendelea kuhitaji mfululizo wa tahadhari ambazo pia zinaoneshwa katika muktadha wa liturujia. Kwa kuzingatia hayo katika mwanzo wa Kwaresima mwaka huu, Baraza la Kipapa la Ibada na nidhamu ya Sakramenti imejulisha kupitia Tovuti yake maelekezo ambayo yanatakiwa washereheshaji wazingatie katika ibada ya kuweka majivu ambayo itakuwa ni Jumatano tarehe 17 Februari 2021.

Baada ya kubariki majivu na kuyanyunyizia kwa maji matakatifu, kwa mijibu wa taarifa hiyo, kuhani atawageukia washiriki waliopo huku akisoma mara moja maandiko yote kama ilivyo katika Misale ya Roma: “Badilika na kuamini Injili”, au “Kumbuka, mwanadamu, wewe ni mavumbi na utarudi mavumbini”.

Katika taarifa hiyo aidha inabainisha kuwa “kuhani atasafisha mikono yake na atavaa barakoa ili kulinda pua na mdomo wake, baadaye anawapaka majivu wale watakao mkaribia au, ikiwa inafaa, yeye mwenyewe atakwenda kwa wale wote ambao watakuwa wamesimama katika nafasi zao”. Kuhani, atahitimisha kwa kuchukua majivu na kuwapaka kichwa, bila kusema chochote.

12 January 2021, 17:24