Tafuta

Siku ya Vijana duniani:Papa Francisko akiwa na dìbaadhi ya vijana huko Poland. Siku ya Vijana duniani:Papa Francisko akiwa na dìbaadhi ya vijana huko Poland. 

Uchumi kwa mujibu wa Papa Francisko-pendekezo la changamotisha dunia!

Kuanzia Alhamisi tarehe 19 hadi 21 Novemba 2020 utafunguliwa mkutano wa siku tatu wa “Economy of Francesco”,yaani uchumi wa Francisko,uliozinduliwa na Papa kwa ajili ya vijana wanauchumi na wajasiriamali ili kuhamaisha mchakato wa mabadiliko ya ulimwengu katika masuala mazima ya kiuchumi.

Na Sr. Angela Rwazaula- Vatican.

Mtindo mpya wa kuelewa uchumi kwa mujibu wa roho ya Mtakatifu Francisko wa Assisi na Waraka wa Laudato si, kuunda harakati ya vijana wanauchumi kwa ajili ya kutafisri pamoja katika mtandao wa kila siku wa waraka wa 'Fratelli tutti', yaani 'wote ni Ndugu'. Haya ni malengo ya “Economy of Francesco”, ya Mkutano na vijana wanauchumi kwa matashi ya Papa Francisko, unaotazamiwa kuanza tarehe 19 hadi 21 Novemba 2020. Kitovu cha tukio hili la kimataifa litajikita kuchambua mada za nguvu ambazo zinahusu kazi, fedha, elimu na akili bandia. Kutokana na janga ambalo linaendelea kutishia ulimwengu la Covid- 19 mkutano huo utaendeshwa kwa njia ya mtandao na imethibitishwa ushiriki wa Papa Francisko.

Miongoni mwa watoa nada katika mazungumzo ya Jumuiya hii maalum na kubwa atakuwa ni Muhammad Yunus, mwanauchumi na mwenye tuzo ya Nobel ya amani 2006, Vabdana Shiva, Mjumbe wa Jukwaa la kimataifa kuhusu utandawazi na Stefano Zamagni, Mwenyekiti wa Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya sayansi Jamii. Hata hivyo mkutano huu utafuatwa mwingine unaotarajiwa kufanyika majiria ya baridi mwaka 2021, huko Assisi, mahali ambapo Mtakatifu Francisko wa Assisi alivua kila kitu na hasa mambo ya kidunia na kumchagua Mungu peke yake awe nyota angavu katika maisha yake.

Katika mahojiano na Vatican News na Domenico Rossignoli, mtafiti wa Chuo Kikuu katoliki amesema “msingi wa uchumi ulio bora ni udugu”. Vijana, wanauchumi, wajasiriamali na wanaharakati kutoka ulimwenguni kote wanaalikwa kutafakari pamoja  na kutia saini makubaliano ya vizazi vingi vyenye lengo la kubadilisha uchumi wa sasa na kutoa roho moja ambayo iwe ni ya kesho, yenye haki zaidi, inayojumuisha na endelevu. Kama vile Papa Francisko anavyosisitiza mara kwa mara kwamba, “kila kitu kimeunganishwa kwa karibu na ulinzi wa mazingira hauwezi kutengwa na haki kwa maskini, kutoka suluhisho la shida za muundo wa uchumi wa ulimwengu”.

Katika barua aliyowaandikia vijana Papa alisisiza kuwa ni muhimu kurekebisha mifano ya ukuaji ambayo haimheshimu mwanadamu, mazingira na hadhi ya mtu na ili uchumi uwe jumuishi na endelevu. Akiendelea amesema katika barua hiyo kwa wanauchumi vijana, wajasiriamali wa ulimwenguni wa wakati wa “Uchumi wa Francisko”, anaonesha njia ya mtindo wa kujenga uchumi ambao ni uchumi tofauti, ni wa pamoja na kujumuisha kila mtu na haumbagui bali unamweka binadamu katikati na wala haudhalilishi, bali hutunza kazi ya uumbaji wote. Mfano mpya wa uchumi, kwa maana hiyo ni tunda la utamaduni wa kushirikishana kwa msingi wa udugu na usawa. Suala hilo hasa ni vijana wanaopaswa kuwa mafundi wa siku za mbeleni, na wao ambao wameitwa kusuka uchumi wa Francis.

16 November 2020, 13:48