Tafuta

Assisi, Economy of Francesco Assisi, Economy of Francesco 

Tukio la Uchumi wa Francesco umethibitishwa tarehe 19-21 Novemba

Maandalizi ya tukio la Economy of Francesco 2020,toleo la kimtandao litaruhusu vijana wote waliojiandikisha kushiriki mkutano katika hali hiyo hiyo,kwa kushirikishana uzoefu wa kuishi,kazi,mapendekezo na tafakari ya kukomaa katika miezi hii.

Mkutano wa Uchumi wa Francisko na vijana wanauchumi kwa utashi wa Baba Mtakatifu Francisko umethibitishwa kuanzia tarehe 19-21 Novemba 2020. Kufuatana na dharura ya Covid-19 , kamati ya maandilizi imeamua tukio hili la kimataifa kufanyika kwa washiriki wote waliojiandisha na watoa mada kwa njia ya mtandao.Umethibitishwa hata ushiriki wa Papa Francisko kwa njia ya mtandao.  Badaye mkutano huo untarajia kufanyika huko Assisi kunako kipindi  cha baridi mwaka 2021 ikiwa hali halisi ya kiafya itaruhusu usalama wa washiriki wote kuwapo.

Maandalizi ya tukio la Economy of Francesco 2020, toleo la kimtandao litaruhusu vijana wote waliojiandikisha kushiriki mkutano katika hali hiyo hiyo, kwa kushirikishana uzoefu wa kuishi, kazi, mapendekezo, na tafakari ya kukomaa katika miezi  hii kwenye vijiji 12.  Kamati iko kazini ili kuekeleza mpango wa ubunifu, ushiriki na ulimwengu ambao unahifadhi mambo msingi ya Uchumi wa Francisko kama vile: Kazi ya makundi, mikutano ya mwaka, maono ya wazungumzaji, tasaufi ya kifransiskani, tamasha ya kisanii na maonesho, kwa kutajirishwa na fursa na lugha ambazo kwa mtindo wa kidigitali wa tukio hilo linavyotoa.

Economy of Francesco ni harakati ya vijana na sura zao binafsi, mawazo ambayo yanadadisi, na kuenea  ulimwengu mzima kwa ajili ya uchumi wa haki, jumuishi na endelevu, na kwa ajili ya kutoa mtindo mmoja wa uchumi wa kesho. Dunia inahitaji ubunifu na upendo wa washiriki ambao kama wahunzi wa wakati ujao wakiwa wanazingatia Uchumi wa Francisko. Amefafanua hayo Padre Enzo Fortunato Mkurugenzi muhisika wa mawazoliano ya Economy of Francesco. Kwa maelezo zaidi fungua tovuti hii:www.francescoeconomy.org

06 November 2020, 16:06