Tafuta

Vatican News
2018.12.07  ufisadi kimataifa 2018.12.07 ufisadi kimataifa  

Vatican:Ufisadi ni hatari kwa amani na usalama!

Katika mkutano wa Osce,Askofu Mkuu Balvo anaonya hatari ya ufisadi na usafirishaji haramu ambao pia umezungukia kwa karibu hata pesa zilizotengwa kwa ajili ya Covid-19.Wito wa nguvu ni kufanya kazi kwa ajili ya wema wa wote bila kuwatenga waliodhaifu zaidi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mapambano dhidi ya ufisadi ndiyo ilikuwa mada msingi katika hotuba ya Mwakilishi wa Vatican katika Mkutano wa Jukwa la Kiuchumi na Mazingira wa Shirika la Usalama na Ushirikiano wa Ulaya (OSCE) katika jiji la Praga. Hotuba iliyokabidhiwa tarehe 10 Septemba 2020 ya Askofu Mkuu Charles Balvo, Balozi wa Kitume katika Jamhuri ya Ceca na Mkuu wa uwakilishi wa Vatican katika mkutano huo, inasema ufisadi ni hali halisi hatari kwa ajili ya amani na usalama. Katika hotuba hiyo bado wasiwasi ni mkubwa kutokana na kwamba fedha nyingi zilizotolewa kwa ajili ya kukabiliana na janga la Covid-19, tayari zimekwisha vutiwana kuwindwa  katika shughuli za kihalifu na kusababisha hatari kwa wale ambao ni wenye kuhitaji zaidi ya fedha hizo na wanabaki bila msaada unaohitajika. Ni lazima kuwa waaminifu, Vatican inasisitiza kwa kuwa na   utambuzi kuwa ufisadi unaweza kudhibitiwa kwa viwango vyovyote katika kila nchi mwanachama wa OSCE, na kwa maana ya kutambua uwepo wa jeraha kubwa kama hili ni wazi wa kuwa na  uwezo wa kupambana nao.

Suluhisho inayolenga faida ya wote

Kutokana na hoja hiyo ni mwaliko  kutoka Vatican wa kutafuta suluhisho jipya na bunifu  katika muktadha wa sasa wa janga la corona au suluhishi ambazo hazina mgawanyiko, kisiasa au kuwanyika sehemu, lakini ambalo hutafuta kwa dhati  kwa ajili ya  faida ya wote na maendeleo fungamani ya  wanadamu. Kwa kuzingatia hayo Vatican  inakumbusha kuwa,  kunako tarehe  1 Juni 2020, Papa Francisko alitangaza Hati yake ya  ‘Motu poprio’  kuhusu sheria juu ya uwazi, udhibiti na ushindani katika taratibu za utoaji wa mikataba ya umma ya Vatican  na Serikali ya  Jiji la Vatican, kwa lengo la  kupunguza  kwa kiasi kikubwa hatari ya ufisadi wa wale ambao wameitwa kutawala na kusimamia vyombo vya Vatican. Kwa mujibu wa maandishi ya Askofu Mkuu Balvo  aansema “Uamuzi huu wa Baba Mtakatifu, unapeleka kutambua kuwa   jeraha la ufisadi, ambalo ni ukweli kwamba wakati wafanyakazi wa umma wanaiba au wanafuja fedha za umma, yote haya yanaathiri jamuiya wanazozihudumia ”.

Uwazi katika usimamizi wa mambo ya umma

Ikiwa kwa hakika usimamzi wa mambo ya umma yanakuwa wazi na uwajibikaji, maendeleo ya uchumi thabiti na wa kudumu na usalama, kwa dhati haviwezi kuwa mashakani, au hata ubatiri. Kwa maana hiyo  Askofu Mkuu   Balvo anatoa ushauri wa kupingana na ufisadi kwa njia ya utamaduni, elimu, mafunzo, ushiriki wa dhati  wa kizalendo, kwa sababu anasema sheria ni za lazima,  lakini hazitoshi. Kinachohitajika ni kutenda kwa ujasiri ili kukung’utua dhamiri nafsi, ili sintofahamu zilizoelezwa,  ziweze kupitia na  kufikia ushiriki  kamili wa kutatua   hali ngumu ya matukio haya kwa namna ya kupambana nayo.

11 September 2020, 15:16