Tafuta

Papa Mstaafu akiwa na Kaka yake Georg Ratzinger aliyefariki Mosi Julai 2020 akiwa na umri wa miaka 96 Papa Mstaafu akiwa na Kaka yake Georg Ratzinger aliyefariki Mosi Julai 2020 akiwa na umri wa miaka 96 

Pd.Georg Ratzinger,kaka yake Papa mstaafu amefariki huko Regensburg

Kuhani mzee wa Bavaria alikuwa amelazwa hospitalini huko Regensburg nchini Ujerumani,mahali alikokuwa anaishi na mahali ambapo alitembelewa kwa ziara ya mwisho na kaka yake Papa Mstaafu.Hawa ni ndugu wawili waliopata daraja la upadre kwa siku moja.

VATICAN

Georg Ratzinger kaka yake mkubwa  wa  Papa,mstaafu amefariki  siku ya  Jumatano asubuhi, Mosi Julai  2020 akiwa na  umri wa miaka 96. Alilazwa hospitalini huko Regensburg, mji ambao aliishi sehemu kubwa ya maisha yake marefu. Pamoja na kifo chake, Joseph Ratzinger, yaani Papa Mstaafu kabla yake alitamani na kusafiri kwa ndege kumwona kaka yake kwa mara ya mwisho na ambaye alikuwa ndugu peke aliyekuwa  bado hai. Ndugu hao wawili  mmoja alikuwa mwanamuziki na mwimbishaji wa kwaya maarufu, na mwingine kwanza mtaalimungu  na badaye kuwa  Askofu, Kardinali na  mwishowe akawa Papa. Wote wawili walibahatika kuwekwa wakfu wa kikuhani siku moja na mara zote walikuwa na umoja.

Alizaliwa huko Pleiskirchen, Bavaria, kunako  tarehe 15 Januari 1924, na alianza kucheza kinanda kanisani wakati alikuwa na miaka 11. Mnamo mwaka wa 1935 aliingia katika seminari ndogo huko Traunstein, lakini kunako 1942 aliandikishwa kwenye Reichsarbeitsdienst yaani (Huduma ya Wafanya kazi wa Reich), na baadaye huko Wehrmacht, ambayo pia alipigana nchini Italia. Alitekwa na washiriki kunako mwezi Machi 1945, na alibaki mfungwa huko Napoli  kwa miezi kadhaa kabla ya kuachiliwa na kuruhusiwa kurudi katika familia yake.

Mnamo 1947, pamoja na kaka yake Joseph, aliingia seminari ya Herzogliches Georgianum huko Munich. Mnamo tarehe 29 Juni 1951, ndugu wote wawili, pamoja na wenzao wengine wapatao arobaini, waliwekwa wakfu wa kikuhani katika Kanisa Kuu la Freising na Kardinali Michael von Faulhaber. Baada ya kuongoza kwaya huko Traunstein kwa miaka thelathini, tangu mwaka w1964 hadi 1994, alikuwa Msimamizi wa Kwaya ya Kanisa Kuu ya makanisa ya Regensburg, “Regensburger Domspatzen”. Aligusa ulimwengu  huko akifanya matamasha mengi, na akaelekeza rekodi nyingi za kijerumani kama Deutsche Grammophon, Ars Musici na nyimbo nyingine muhimu za kumbukumbu, na uzalishaji uliowekwa kwa watunzi maarufu kama Bach, Mozart, Mendelssohn na watunzi wengine.

Kunako  tarehe 22 Agosti 2008, akimshukuru meya wa Castel Gandolfo kwa kumpa uraia wa heshima ya Georg, Papa Mstaafu Benedikto XVI alizungumzia  juu ya kaka yake kuwa  “tangu mwanzo wa maisha yangu,  kaka yangu daima amekuwa sio rafiki yangu tu, bali pia kiongozi  wa kuaminika. Kwangu yeye amekuwa kiongozi, mwelekeo na kumbukumbu kwa uwazi na uamuzi na maamuzi yake. Amewahi kunionyesha na kuniongoza njia ya kuchukua, hata katika hali ngumu”.

Georg Ratzinger katika mahojiano miaka kumi na moja iliyopita alisema, “kaka yangu na mimi," wote wawili tulikuwa wavulana wa madhabahu.Sisi sote  wawili tulihudumia Misa. Ilikuwa wazi kwetu, kwanza kwangu na kwake, ya kwamba maisha yetu yangekuwa huko huko  katika huduma ya Kanisa. Na alishirikisha kumbukumbu za utoto wao pia kwamba :“Huko Tittmoning, Joseph alikuwa amepokea uthibitisho kutoka kwa Kardinali Michael Faulhaber, Askofu Mkuu wa Munich. Alikuwa amevutiwa na akasema kwamba yeye pia anataka kuwa kardinali. Lakini ni siku chache tu baada ya kukutana na kumuona mchoraji aliyechora kuta za nyumba yetu, alisema kwamba wakati atakapokuwa mtu mzima, atakuwa mchoraji( ...)".

01 July 2020, 15:00