Tafuta

Vatican News
2013-02-24 Papa Benedikto XVI 2013-02-24 Papa Benedikto XVI 

Papa Mstaafu amerudi jijini Vatican!

Papa Mstaafu Benedikto XVI amerudi katika makao yake mara baada ya siku kadhaa kumtembelea kaka yake mgonjwa nchini Ujerumani.

VATICAN 

Papa Mstaafu ameacha Seminari ya Regensburg nchini Ujerumani karibia saa 4.00 asubuhi majira ya Ulaya, alikokuwa amekaribishwa katika siku hizi na kwenda katika uwanja wa ndege wa Monaco ya Baviera ambapo baadaye amewasiri jijini Roma. Majira ya saa saba na  dakika 45 amerudia kwa gari katika Monasteri ya Mater Ecclesiae mjini Vatican. Kwa maana hiyo Papa Mstaafu amehitimisha  ziara ya siku zake nchini Ujerumani kwa ajili ya kukaa karibu na kaka yake Georg mwenye umri wa miaka 96 ambaye ni mgonjwa.

Papa msaafu Benedikto XVI alifika Monaco ya Baviera siku ya Alhamisi iliyopita na kupokelewa na Askofu Rudolf Voderholzer ambaye alimsindikiza hadi Regensburg. Katika siku za kukaa huko Papa Mstaafu ameweza kumtembelea mara nyingi kaka yake lakini pia hata kuona maeneo mengine ya  wapendwa wa familia yake kwa namna ya pekee  katika makaburi ya Ziegetsdorf, mahali ambapo wanapumzika wazazi wake na dada yake mkubwa pia nyumba yake huko Pentling, pembeni kidogo mwa mji wa Regensburg mahali ambapo alikaa wakati yeye ni Profesa wa Chuo Kikuu cha eneo hilo na sasa ni Makao makuu ya Taasisi ambayo wameipa jina lake.

Kati ya mikutano ya siku hizi ni pamoja na ule wa Balozi wa Kitume nchini Ujerumani aliyewasiri kutoka Berlin, Askofu Mkuu Nikola Eterović na ambaye wakati wa huduma yake ya Kipapa, Papa mstaafu alikuwa amemteua katika shughuli ya ukatibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu.

22 June 2020, 16:06