Papa Francisko awatembelea watoto katika michezo ya kiangazi mjini Vatican!
Na Sr. Angela Rwezaula- Vtivan
Watoto wengi walikuwa bado hawajaamini kumwona Papa anatokeza ambao kila aasubuhi wanakusanyika pamoja katika kituo cha kiangazi kilichopendelewa na Papa mwenyewe mjini Vatican kwa ajili ya kuwasaidia wazazi ambao wanafanya kazi mjini Vatican. Kiukweli ilikuwa ni baada ya saa tatu hivi, Papa Francisko amewatembelea watoto na vijana ambao walikuwa wanafungua kinywa katika uwanja wa Jengo la Papa Paulo VI.
Kwa mujibu wa msemamji Mkuu wa vyombo vya habari Vatican, Dkt. Matteo Bruni amesema “Mara baada ya kupitia kwenye meza zao, Papa ametembelea hata sehemu zote na maeneo yaliyotengeneza kwenye Ukumbi wa Papa Paulo VI kwa ajili ya tukio hilo na kukaa katikati na washiriki hao baadaye amerudi katika Makao yake ya Mtakatifu Marta saa nne na kuwashukuru kila mmoja wa wahudumu hao kwa kazi yao wanayotenda”. Wakati wa ziara yake hiyo fupi Papa Francisko amekaa katikati ya watoto na kuwatia moyo ili watengeneze marafiki wapya. “watu ambao hutaka kujifurahisha peke yao, mara nyingi ni wabinafsi, kwa maana ni lazima kukaa pamoja na marafiki”, Papa amebainisha.
Padre Fontana aeleza furaha na mshangao wa watoto
Akiwasalimia watoto, Papa amepitia katika meza zao kuanzia zile za watoto wadogo, za shule za msingi na sekondari. Amependa kuulizia hata maswali wanafanya nini kwa siku nzima na kama walikuwa na furaha, kwa mujibu wa Mratibu wa “Kiangazi kwa vijana”, Padre Franco Fontana, ambaye ni msimamizi wa Kikanisa cha Vikosi vya Ulinzi na Majumba ya Makumbusho. Kwa mshangao mkubwa vijana walibaki kimya kabisa na baadaye walimzungusha kwenye Ukumbi na kuendelea na shughuli zao za michezo ya kila siku.
Papa amejibu maswali yote kwa urahisi
Hata hivyo Papa Francisko amependa iwe hivyo. Watoto watatu wamemuuliza maswali ambayo yalikuwa yamekwisha andaliwa kwani ndiyo ilikuwa nia ya kumwandikia barua. Papa ameyajibu yote kwa urahisi tu na mwisho amesalimia na kuwashukuru watu 22 wanaowasaidia watoto na vijana hao. Kabla ya kuondoka wamepiga hata picha ya pamoja. Jambo ambalo limemshangaza Padre Franco ni kwa namna gani watoto wamempokea Papa kama kifamilia, urahisi na ubaba ambao wameishi kwa kipindi kifupi hicho.
Shughuli za michezo wakati wa kiangazi
Kituo hiki cha kiangaza kimefunguliwa kwa utashi wa Mamlaka ya Vatican ili kuwasaidia kidogo wazazi ambao wanafanya kazi Mjini Vatican. Kimefunguliwa mwezi huu wa Julai 2020 katika shughuli za elimu, michezo na katika kutembelea Bustani ndani ya Vatican. Shughuli za michezo zinafanyika katika Ukumbi wa Papa Paulo VI, ambapo ni mamia ya watoto karibu ambao wanafika kia siku asubuhi, lakini pia kwa kufuata protokali za kuzuia maambukizi ya covid-19. Kituo kinaendeshwa na shirika la Mtakatifu Dono Bosco pamoja na chama kiitwacho “Yote ni siku kuu”. Kila siku shughuli pia ni katika bwawa la kuogelea, michezo ya mpira wa tenis, wa miguu na kikapu, na michezo mingine kama pic nic katika Bustan za Vatican.