Tafuta

We run toghether ni kauli mbiu inayoongoza mashindano ya Mshikamano kwa ajili ya kufadhili hospitali za Bergamo na Brescia nchini Italia We run toghether ni kauli mbiu inayoongoza mashindano ya Mshikamano kwa ajili ya kufadhili hospitali za Bergamo na Brescia nchini Italia 

Kamba zinakatwa kuanza mnada wa mashindano ya mshikamano!

Mnada wa michezo kwa ajili ya ufadhili "WE RUN TOGETHER", ulioanzishwa na Papa Francisko umeanza tarehe 8 Juni 2020.Haya ni mashindano kwa njia ya mnada wa mshikamano ili kuweza kufadhili hospitali za Brescia na Bergamo nchini Italia,walio mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya janga la corona.Mashindano hayo yanafanyika kupitia mtandaoni.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Mtu anaweza kujiuliza hivi kweli ni mchezo kwa mujibu Papa Francis? Ndiyo, inawezekana. Ni hakika, kwa njia nyingine tayari ni ukweli kwa sababu ni  mchezo ambao unafanya utamaduni wa kukutana na watu  kwa kushinda na kuweka pembeni kinzani, vurugu na biashara isiyosimamishwa.  Wanasema hayo  hasa kwa mabingwa wengi ambao wanaitikia mwaliko wa Papa wa kukimbia kwa moyo kupitia mnada wa mshikamano  uliopewa kauli mbiu  “Tunakimbia pamoja” “We Run Together”. Fursa hiyo imeanza tarehe 8 Juni 2020 kupitia mtandao katika  tovuti ya www.charitystars.com ambapo inawezekana kushiriki katika ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya kufadhili wahudumu wa hospitali za Bergamo na Brescia, nchini Italia  walio  mstari wa mbele katika mapambano ya  virusi vya corona

Ni zaidi ya mipango mingine maana ni ushuhuda

Hata hivyo “We Run Together”  au tunakimbia pamoja ni zaidi ya mpango muhimu wa hisani kwa maana ni ushuhuda kwamba inawezekana kuishi  uzoefu wa mchezo kwa mujibu wa Papa Francisko kwa maana ya kwamba mchezo ni kama daraja la amani ambalo huwaunganisha wanawake na wanaume wa dini na tamaduni tofauti, hukuza ujumuishaji na kuhamasisha urafiki, mshikamano, na elimu.  Ni maneno ya Papa Francisko aliyochagua kunako tarehe 20 Mei iliyopita wakati wa kukutana na wanariadha wa Vatican ili kuzindua mnada huo, ulioandaliwa na ushirikiano wa  vyama vya wanamichezo waitwao “Fiamme Gialle, Cortile del Nations na Fidal Lazio”.

Mabingwa wa mshikamano

Jibu ambalo ulimwengu wa michezo kimataifa unatoa katika ujumbe wa Papa ni ishara thabiti ya matumaini, hasa katika wakati huu wa janga. Na hivyo ulikuwa mwaliko wa Papa  Francisko kwa wanariadha, wakati  huo wa  mkutano wa Mei 20, aliwahimiza  wawe ‘wabeba uzuri’ na kujua jinsi ya kwenda “kwa kasi kwa  wanyonge”. Na kwa dhati ndiyo maneno ambayo yamethibitishwa na Alex Zanardi  kwamba ni ya kina ya shauku yake.  Kwa mujibu wake Zanardi  amesema, maneno hayo yanapaswa yatumike kwa kila mtu na siyo tu kwa wanariadha, amesisitiza bingwa ambaye ameweka mnadani shati lake alilokuwa amevaa wakati wa shindano la ‘Paralympics’ huko Rio del Janeiro, Brazil mwaka 2016. Mtindo  huo pia amefafanua ni kama  walionao  waendesha baisikeli ambao hulazimika kungojea wenzi wao, kwa mfano ambao wanaanguka au kupunguza mwendo baada ya mwingine taili la baiskeli kupasuka hivyo kuweza kumsindikiza hadi anarudi katika kundi kuendelea na mbio. Kwa roho hiyo, ulimwengu wa wanamichezo ‘Paralympic’ wamejiunga kwa wingi katika  kaulimbi hiyo ya “Tunakimbia pamoja”/ “We run together”  ili kupeleka ubingwa wao kwa wale ambao wanahitaji zaidi kwa kutoa mshikamano wao!

08 June 2020, 12:00