Kamba zinakatwa kuanza mnada wa mashindano ya mshikamano!
Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican
Mtu anaweza kujiuliza hivi kweli ni mchezo kwa mujibu Papa Francis? Ndiyo, inawezekana. Ni hakika, kwa njia nyingine tayari ni ukweli kwa sababu ni mchezo ambao unafanya utamaduni wa kukutana na watu kwa kushinda na kuweka pembeni kinzani, vurugu na biashara isiyosimamishwa. Wanasema hayo hasa kwa mabingwa wengi ambao wanaitikia mwaliko wa Papa wa kukimbia kwa moyo kupitia mnada wa mshikamano uliopewa kauli mbiu “Tunakimbia pamoja” “We Run Together”. Fursa hiyo imeanza tarehe 8 Juni 2020 kupitia mtandao katika tovuti ya www.charitystars.com ambapo inawezekana kushiriki katika ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya kufadhili wahudumu wa hospitali za Bergamo na Brescia, nchini Italia walio mstari wa mbele katika mapambano ya virusi vya corona
Ni zaidi ya mipango mingine maana ni ushuhuda
Hata hivyo “We Run Together” au tunakimbia pamoja ni zaidi ya mpango muhimu wa hisani kwa maana ni ushuhuda kwamba inawezekana kuishi uzoefu wa mchezo kwa mujibu wa Papa Francisko kwa maana ya kwamba mchezo ni kama daraja la amani ambalo huwaunganisha wanawake na wanaume wa dini na tamaduni tofauti, hukuza ujumuishaji na kuhamasisha urafiki, mshikamano, na elimu. Ni maneno ya Papa Francisko aliyochagua kunako tarehe 20 Mei iliyopita wakati wa kukutana na wanariadha wa Vatican ili kuzindua mnada huo, ulioandaliwa na ushirikiano wa vyama vya wanamichezo waitwao “Fiamme Gialle, Cortile del Nations na Fidal Lazio”.
Mabingwa wa mshikamano
Jibu ambalo ulimwengu wa michezo kimataifa unatoa katika ujumbe wa Papa ni ishara thabiti ya matumaini, hasa katika wakati huu wa janga. Na hivyo ulikuwa mwaliko wa Papa Francisko kwa wanariadha, wakati huo wa mkutano wa Mei 20, aliwahimiza wawe ‘wabeba uzuri’ na kujua jinsi ya kwenda “kwa kasi kwa wanyonge”. Na kwa dhati ndiyo maneno ambayo yamethibitishwa na Alex Zanardi kwamba ni ya kina ya shauku yake. Kwa mujibu wake Zanardi amesema, maneno hayo yanapaswa yatumike kwa kila mtu na siyo tu kwa wanariadha, amesisitiza bingwa ambaye ameweka mnadani shati lake alilokuwa amevaa wakati wa shindano la ‘Paralympics’ huko Rio del Janeiro, Brazil mwaka 2016. Mtindo huo pia amefafanua ni kama walionao waendesha baisikeli ambao hulazimika kungojea wenzi wao, kwa mfano ambao wanaanguka au kupunguza mwendo baada ya mwingine taili la baiskeli kupasuka hivyo kuweza kumsindikiza hadi anarudi katika kundi kuendelea na mbio. Kwa roho hiyo, ulimwengu wa wanamichezo ‘Paralympic’ wamejiunga kwa wingi katika kaulimbi hiyo ya “Tunakimbia pamoja”/ “We run together” ili kupeleka ubingwa wao kwa wale ambao wanahitaji zaidi kwa kutoa mshikamano wao!