Tafuta

Vatican News
Misa ya Papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican itaendelea kwa njia mubashara hata kwa wiki ijayo ikiwa pmoja na Katekesi. Misa ya Papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican itaendelea kwa njia mubashara hata kwa wiki ijayo ikiwa pmoja na Katekesi. 

Misa mubashara katika Kanisa la Mtakatifu Marta inaendelea!

Kwa mujibu wa Msemaji mkuu wa vyombo vya habari Vatican amebainisha kuwa maadhimisho ya misa takatifu za kila siku asubuhi katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican zitaendelea kutolewa mubashara na ndivyo itakavyo kuwa hata kwa katekesi ijayo tarehe 18 Machi 2020.

Kulingana na hali halisi ambayo inaendelea kujionesha kutokana na COVID-19, Baba Mtakatifu Francisko ametoa uamuzi wa kuendelea na misa kila siku asubuhi saa 1.00 kamili majira ya Ulaya hata kwa wiki ijayo katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican kwa mubashara, hata Jumapili tarehe 15 Machi 2020 na kwa wiki nzima ijayo.

Kwa kuzingatia sheria zilizowekwa na marufuku ya kuwa na mikusanyiko katika harakati hizi za kuzuia kuenea kwa virusi (COVID-19), sala ya Malaika wa Bwana, tarehe 15 Machi 2020 na Katekesi ijayo ya  Jumatano tarehe 18 Machi vitakuwapo mubashara. Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican pia anabainisha kuwa katika tovuti ya Vatican News picha zitasambazwa pia  Vatican itawawawezesha Vyombo vya Habari vitakavyoomba ili kufanikisha kuwafikia waamini ulimwenguni kote waweze kushiriki kwa hali yoyote.

14 March 2020, 13:33