Tafuta

Vatican News
Papa Francisko tarehe 6 Februari amekutana na waziri Mkuu wa Croazia Bwana Andrej Plenković Papa Francisko tarehe 6 Februari amekutana na waziri Mkuu wa Croazia Bwana Andrej Plenković  (ANSA)

Papa Francisko amekutana na waziri Mkuu wa Kroatia Andrej Plenković

Tarehe 6 Februari 2020 Papa amekutana na Waziri Mkuu wa Andrej Plenković,wa Jamhuri ya nchi ya Croatia,na baada ya mkatano huo amekutana pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher,Katibu wa mahusiano na ushirikiano wa nchi za Nje.

VATICAN 

Papa Francisko tarehe 6 Februari 2020 amekutana na Waziri Mkuu Bwana Andrej Plenković, wa Jamhuri ya nchi ya Croatia na baada ya mkatano huo amekutana pia  na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akiambatana na Askofu Mkuu  Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Ushirikiano na chi za Nje. Katika mazungumzo na Katibu wa Vatican, wameonesha uwepo wa  mahusiano mema  kati ya sehemu zote mbili, na nia ya kuendeleza ushirikiano katika sekta husika.

Katika  mazungumzo yao pia, wamesisitizia juu ya msingi wa jitihada  za miaka 3 ya nchi ya Kroazia wa jukumu la  uwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Ulaya  na kwa namna ya pekee katika kutazama changamoto ambazo zinajikita katika wakati endelevu wa Ulaya. Hatimaye wamezungumzia mantiki zinazotazama kimataifa na kikanda, ikiwa ni pamoja na hali halisi ya watu wa Kroatia walioko Bosnia -Erzegovina, uhamiaji, amani na usalama.

 

06 February 2020, 14:43