Tafuta

Vatican News
Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican ametuma barua yake katika Mkutano wa 70 wa Wiki ya Liturujia Kitaifa inayofanyika huko Messina Italia.Anahimiza tafakari la kina katika liturujia kwa ajili ya huduma Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican ametuma barua yake katika Mkutano wa 70 wa Wiki ya Liturujia Kitaifa inayofanyika huko Messina Italia.Anahimiza tafakari la kina katika liturujia kwa ajili ya huduma 

Kard.Parolin:Kutafakari kwa kina katika liturujia kunawezesha kupenda ndugu!

Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican ametuma barua kwa ajili ya Mkutano wa 70 wa Wiki ya Liturujia Kitaifa nchini Italia.Katika barua hiyo anatoa salam kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko na kuwashauri wapokee daima kwa ukarimu maana na lugha za ishara kwenye liturujia,ikijumuishwa na sanaa,nyimbo,muziki na ukimya.Kutakari kwa kina katika litutujia inawezesha upendo na huduma kwa jirani

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuendelea mafunzo ya kiliturujia ili kuweza kuwasaidia watu wa Mungu na kupenda liturujia kama uzoefu wa kukutana na Bwana na ndugu, unaojikita katika oungofu wa kutufanya tuwe na uwezo wa kupenda na kuhudumia wengine kama alivyo fanya Kristo, ndiyo maneno yaliyomo katika barua ambayo ni kama utume wa Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akiwatia moyo washiriki wa Mkutano wa 70 wa Liturujia Kitaifa ambao wameunganika huko Messina kuwanzia tarehe 26 Agosti hadi Alhamish ijayo. Ni mkutamo ya watu ambao kila mwaka wanakutana katika moja ya majimbo katoliki nchini Italia. Mwaka huu wanaongozwa na tema isemayo: “Liturujia; wito kwa wote katika utakatifu wa ubatizo”

Kugundua kwa upya mambo yaliyomo ndani ya liturujia na kuhifadhi katika ibada

Katika barua yake aliyoelekeza kwa Askofu Claudio Maniago wa Jimbo la Kastellaneta na Rais wa Kituo cha Matendo ya Kiliturujia, Italia na ambaye ameandaa tukio hili, anaomba kusaidia jumuiya ili wajikite kwa kina katika sala ya Kanisa, kwa  kugundua kwa upya mambo yaliyomo na kuyahifadhi katika ibada. Liturujia itakuwa ya kweli na  yenye uwezo wa kuunda na kubadili wale ambao wanashiriki, anabainisha Kardinali Parolin, iwapo wachungaji na wlei wataendelea kuelewa vema na kupokea kwa ukarimu maana yake ya  lugha za ishara, ambazo zinajumuishwa na sanaa, nyimbo na muziki katika huduma ya maadhimisho ya fumbo na  kutambua kwa dhati ukimya wake.

Lengo la kuanzishwa kwa wiki ya liturujia

Lengo la kuanzisha kwa Wiki ya Liturujia Kitaifa ina umuhimu  hata wa kutafakari kwa kina juu ya upyaisho wa liturujia, ulioombwa na Mtaguso wa II wa Vatican. Kardinali Parolin anafafanua uhusiano kati ya utakatifu na liturujia huku akiwataka kwa namna ya pekee kutazama Mtaguso Mkuu (Sacrosanctum Concilium) kuhusu hati ya  Liturujia Takatifu. Amesema, Mababa wa Mtaguso wanasisitiza kwamba liturujia wakati inapoadhimisha utakatifu, inatakatifuza waamini katika Liturujia. Na  ibada halisi za hadharani huadhimishwa kwa Mwili wa Fumbo la Kristo Yesu, yaani Kanisa. Hili ni tendo takatifu katika maisha na utume wa Kanisa na hata kama Baba Mtakatifu Francisko analivyo kumbusha kwamba “liturujia ni maisha kwa ajili ya watu wote wa Kanisa.” Katika Liturujia, upo uwezekano wa utakatifu wa Mungu kwa hakika ambao unaoesha inaonesha Kristo na uso wa uhuruma, wa upendo wa bure na wakati huo huo  Liturujia inaruhusu waamini waishi maisha yake wenyewe. Baba Mtakatifu kwa namna hiyo ni matashi yake kuwa, kutokana na Wiki hii ya Lirurujia, inawezekana kukomaa utambuzi ya kuwa liturujia  ni mahali mwafaka ambamo utakatifu wenyewe wa Mungu unavutia.

Kutoka Liturujia hadi uongofu kwa ajili ya kuwa na mwenendo kama Bwana

Katika Ekaristi, Roho Mtakatifu anawafanya kuishi maisha ya Mungu, ambaye anabadili kila kitu, na  kama watu wanaokufana kufanya kuwa na uwezo wa kupenda kama alivyofanya Yesu, kwa kutoa maisha yake binafsi kwa ajili ya huduma ya ndugu. Liturujia kwa hakika ni uzoefu ambao unaelekeza uongofu wa maisha kwa njia ya kubadilika namna ya kufikiri, namna ya mwenendo wa Bwana, anabainisha, Kardinali Parolin, huku akikumbusha tena maneno ya Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake mwezi Februari kwenye Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa.

Katika hotuba ya Baba Mtakatifu kwa washiriki haoaliwakumbusha kuwa,liturujia siyo kambi ya jitengenezee mwenyewe na huwezi kuipunguza kwa walio na haki au kuweka orodha na matukio,bali  lituturujia inapaswa kupokelewe kwa ukarimu na kuhamasishwa kwa upendo, katika sala na ishara zilizo ndani mwetu  au na mimi, yaani katika jumuiya ya kweli. Aidha Baba Mtakatifu alikazia juu ya kupenda liturujia, ambao ni uzoefu wa kukutana na Bwana na ndugu kama njia ya wokovu wa maisha. Na kutokana na hilo aliweka angalisho la uongofu dhidi ya  mawazo potofu yasiyo zaa matunda kwani liturujia ya jumuiya ya Kanisa isiweze kuwa na tabia ya kufikiria yaliyopita au kulazimisha mapya ambayo yanaleta hatari ya kuwa na umimi kwa watu wa Mungu. Na kinyume chake ni kutambua liturujia takatifu kama tunu hai ambayo haiwezi kupunguzwa kamwe kwa kuhalisha haki au usasa, badala yeke ni kupokelewa kwa ukarimu na kuhamasisha upendo. https://www.vaticannews.va/sw/pope/news/2019-02/papa-sakramenti-ibada-nidhamu-baraza.html

27 August 2019, 13:02