Tafuta

Wawakilishi wa Mkutano wa mwaka wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti wamekutana na Papa tarehe 14 Februari 2019 Vatican Wawakilishi wa Mkutano wa mwaka wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti wamekutana na Papa tarehe 14 Februari 2019 Vatican 

Papa amekutana na wawakilishi wa Mkutano wa Baraza la Ibada na nidhamu ya sakramenti

Katika Ukumbi mdogo wa Paulo VI mjini Vatican,tarehe 14 Februari 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti ambapo amekazia umuhimu wa mafunzo ya kiliturujia kwa mujibu wa mada inayoongoza mkutano wao

Na Sr.Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 14 Februari 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti. Katika wito wake karibia kwa washiriki 80 katika ukumbi mdogo wa Paulo VI mjini Vatican  amewahimiza wafanya kazi kwa ajili ya watu wa Mungu ili wapate kugundua uzuri wa kukutana na Bwaa katika Liturujia na ili waweze kuwa na maisha kwa jina lake

Angalisho la kuwa na uongofu

Baba Mtakatifu anashukuru Kardinali  Robert Sarah kwa maneno yake na kuwasalimia wajumbe, waandaaji na wahudumu Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti. Anasema Mkutano wa mwaka unafikia wakati mwafaka. Imetimia miaka 50 tangu tarehe 8 Januari 1969 ambapo Mtakatifu Paulo VI alianzisha Baraza hilo kwa lengo la kutoa muunod wa upyaisho uliopendekezwa na Vatican. Hii ilikuwa inatakiwa kutangaza vitabu vya kiliturujia katika mantiki zake na maamuzi ya mababa wa mtaguso kwa kwa kuwwazesha watu wa Mungu wapate ushiriki  na utambuzi ulio wazi wa mafumbo ya Kristo (Rej Cost. Sacrosanctum Concilium, 48).Utamaduni wa kusali wa Kanisa ulikuwa inahitaji vielelezo vya upyaisho bila kupoteza lolote katika  milenia ya utajiri wake na badala yake kugundua kwa upya zile tunu za asili. Katika miezi ya kwanza kwa  mwaka huo, ndipo ilichanua mtindo mpya wa Makao ya Kitume kwa ajili ya faida ya Watu wa Mungu. Katika tarehe  14 Februari 1969 kwa Motu Proprio wa Mysterii paschalis ilitolewa kalenda ya kirumi na mwaka wa Kiliturujia. Kwa maana hiyo umuhimu wa Katiba ya kitume yaani Misale ya Roma ikatangazwa na Baba Mtakatifu kunako tarehe 3 Aprili 1969. Mwaka huo huo ikaonekana tena mwanga mpya wa vitabu vya ibada za misa (ordo misae) na nyingine, kati yazo ni ya Ubatizo wa watoto, ya ndoa pia na mazishi. Ilikuwa ni hatua za mwanzo wa safari ya kufuata kwa hekima thabiti. Baba Mtakatifu anasema, haitoshi kuwa na  vitabu vya kiliturujia ili kuboresha liturujia, kwa sababu maisha ya kweli ya kusifu na kumpendeza Mungu yanahitaji mabadiliko ya moyo. Uongofu huo umeelekeza na maadhimisho ya kikristo ambayo ni kukutana na Mungu aliye hai (Mt 22,32).

Liturujia takatifu kama tunu hai na ambayo isipunguzwe thamani yake

Baba Mtakatifu  amekazia juu ya kupenda liturujia, uzoefu wa kukutana na Bwana na ndugu kama njia ya wokovu wa maisha. Na kutokana na hilo anaweka angalisho la uongofu na mawazo potofu yasiyo zaa matunda kwani liturujia ya jumuiya ya Kanisa isiweze kuwa na tabia ya kufikiria yaliyopita au kulazimisha mapya ambayo yanahatarisha umimi kwa watu wa Mungu. Kinyume chake ni kutambua liturujia takatifu kama tunu hai ambayo haiwezi kupunguzwa kamwe kwa kuhalisha haki au usasa, badala yeke ni kupokelewa kwa ukarimu na kuhamasisha upendo. Aidha Baba Mtakatifu anasema Vatican kwa dhati haiondoi nafasi ya maaskofu duniani, badala yale inashirikiana na wote ili kuhudumia katika utajiri wa tamaduni za lugha nyingi, wito wa sala katika Kanisa la ulimwengu. Sambamba na hilo anasema kuna Motu proprio ya Magnum principium (tarehe 3 septemba 2017), wenye  lengo la kusaidia ulazima wa kuendeleza ushirikiano daima na kamili katika matumaini ya pamoja, kulinda na ubunifu kati ya Mabaraza ya Maaskofu na Baraza la Baraza la Kipapa linalijikta katika zoezi hili la kuhamasisha liturujia takatifu. Ni matashi mema ya Baba Mtakatifu wa kuendelea na mchakato huo wa ushirikiano kwa utambuzi wa uwajibikaji na muungano wa Kanisa wa kupanua umoja na wingi wake.

Ni tatizo la umoja

Baba Mtakatifu Francisko amekazia mada msingi kwamba lazima kukumbuka kuwa liturujia ni maisha ambayo yanaunda na siyo mawazo ya kujifunza. Ni bora kukumbuka kuwa hali halisi ni muhimu zaidi ya mawazo. Na wema wa liturujia kama ilivyo kwa mantiki nyingine za maisha ya Kanisa isisishie kuwa tasa. Na ndipo amekazia juu ya mafunzo kama moja ya mada ya mkutano wao. (cfr Esort. ap. Evangelii gaudium, 231-233). Na ili maisha yawe kweli sifa inayompendeza Mungu lazima kwa dhati kubadili moyo, Uongofu huo unaelekezwa katika maadhimisho ya kikristo ambayo ni mkutano na maisha ya Mungu aliye hai. Kwa maana hiyo kazi yao leo hii ni sawa na kumsaidia Baba Mtakatifu ili aweze kuendelea na utume wake kwa wema wa Kanisa katika sala inayaoendelea katika dunia nzima. Kuungana kikanisa kwa njia ya kuwa na Makao makuu ya kitume na Mabaraza ya Maaskofu katika Roho ya ushirikiano, mazungumzo na mkutano wa pamoja. Liturujia siyo kambi ya jiandalie binafsi, badala yake ni maonesho ya muungano wa Kanisa. Kwa maana hiyo sala na ishara zake zinapaswa kuwa za pamoja na siyo binafsi na ili kuweza kuzuia itikadi za muungano na mizizi ya malimwengu ya kitasaufi.

Kusaidia watu wa Mungu ili wasali vema kwa kina

Ni tunu kwa maana ya mada ya mkutano wao ambayo inasema “ mafunzo ya liturujia ya watu wa Mungu. Kanisa inyawasubiri wasubiri Baba Mtakatifu anasema kwa dhati ni ile ya kueneza kwa watu wa Mungu mwanga wa fumbo la Bwana ambaye anajionesha katika liturujia. Kuzungumzam juu ya liturujia kwa watu wa Mungu ina maana ya utambuzi wa dhamiri ya nafasi ambay hawezi kuondolewa na ambayo liturijia inavaa katika Kanisa na kwa ajili ya Kanisa. Pia kuna suala la kusaifia kwa dhati watu wa Mungu waweze kujikita kwa kina sala vema katika Kanisa na kuipenda kama uzoefu wa kukutana na  Bwana na ndugu , katika mwanga na ambao ni kugundua kwa upya mambo yote yaliyomo na kuhifadhi ibada. Kwa kuwa liruturujia ni uzoefu wa uongofu kwa njia ya kujifananisha kwa namna ya kufikiria na mwenendo wa Bwana , mafunzo ya liturjuia haiwezi kuishia katika utoaji wa  mafunzo ya utambuzi , hiyo ni makono japokuwa ni muhimu karibia vitabu vya kiliturujia na hata kulinda kutimiza nidhamu za ibada. Na ili liturujia iweze kutendeka vuma kama maman a mwalimu, wachungaji na wale laimia waanzishe kuipokea maana na lugha za ushala, ikiwa ni pamoja na sanaa, wimbo  na muziki kwa ajili ya hduma ya fumbo la maadhimisho na hata ukimya. Hata Katekisimu ya Kanisa Katoliki ilichukua njia hi ina kuonesha katuka liturujia, kuthamanisha sala na ishala. Mafunzo ni njia mojawapo kwa ajili ya kuingia katika fumbo la liturujia, katika makutano hai na Bwana msulibiwa na mfufuka. Mafunzo maana yake ni kugunfa maisha mapya ambayo watu wa Mungu walipokea kwa njia ya Sakrameni na kuendelea kugunda uzuri wake pia kuupyaisha.

Wao wanawajibika ili watu wa Mungu wagundue uzuri wa kukutana na Bwana katika mafumbo ya liturujia

Kuhusiana na hatua za mafunzo, Baba Mtakatifu amesema, uzoefu unaonesha kwamba, zaidi ya mafunzo ya mwanzo, ni lazima pia  kukuza mafunzo ya kudumu kwa makleri na walei hasa wanaojikita katika fumbo la huduma ya liturujia. Mafunzo siyo ya mara moja tu bali ya kudumu.Kwa wale wenye kutiwa wakfu maalum hata kwa mtazamo wa maadhimisho, inahitaji kukumbuka hata maneno ya mtaguso: "ni lazima kutoa nafasi ya kwanza katika mafunzo ya kiliturujia kwa makleri” (Cost. Sacrosanctum Concilium, 14). Uwajibikaji wa mafunzo ni wa kushirikisha japokuwa unahitaji kila jimbo mahaliawafanye zoezi hili kwa hatua. Shughuli yao amesisitiza Baba Mtakatifu, itawasadia Baraza hilo kukomaa katika mpangilio na maelekezo ya kutoa, katika roho ya huduma katika  Mabaraza ya Maaskofu, Majimbo na taasisi za mafunzo, na wakati huo huo hata magazeti yanawajibika kulinda na kusindikiza mafunzo ya liturujia kwa watu wa Mungu. Amehitimishwa akisema kwamba, wote waaalikwa kujikita kwa undani zaidi katika mafunzo, kupyaisha mafunzo ya liturujia. Liturujia kwa hakika ni njia mwalimu na  ambayo ni  maisha ya kikristo kwa kila hatua ya kukua. Mbele yao wao wanalo zoezi kubwa na zuri. Kufanya kazi ili watu wa Mungu waweze kugundua uzuri wa kukutana na Bwana katika maadhimisho ya mafumbo yake na kukutana naye, kuwa na maisha tele kwa jina lake. Amewashukuru kwa jitihada za ona kuwabariki.

14 February 2019, 15:54