Tafuta

Vatican News
Tuzo kutolewa katika tamasha la waandishi wa mediterranea Tuzo kutolewa katika tamasha la waandishi wa mediterranea 

Zawadi ya toleo la Tamasha la 10 kwa Waandishi wa Habari wa Mediterrania!

Katika tamasha la Fukweni kwa Mashujaa wa Otranto, tarehe 16 Septemba 2018 wamefanya maadhimisho ya kutoa zawadi ya Toleo la 10 kwa Waandishi wa habari wa Mediterrania, ambapo hata Vatican News ni mojawapo wa kupokea zawadi!

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Waliokuwa bora  katika utoaji taarifa za kitaifa na kimataifa kwa kile kinachotokea katika Mediterrania na historia ambazo zinasaidia, si tu kubaki tofauti bali, ni  kujua vema kila ambacho kinatukia katika dunia hata kutoa nafasi ya kufakari kwa dhati. Na  ndiyo zawadi inayotolewa kwa karibu ya miaka 10 mfululizo wa Mashindano ya Tamasha wa Waandishi wa Habari wa Mediterranea wa Otranto, ambao kwa mwaka 2018 imekwenda sambamba na Kipeo kikubwa ambacho kinaikumba Bahari ya Mediterranea: kwa mfano wa vita vya Siria,Yemen, Libia Iraq, tishio la kigaidi kimataif, majanga ya wahamiaji na mambo mengi yaliyo karibu na sisi, kwa mujibu wa Lino Patruno , mhusikia Mkuu wa habari katika kujenga amani.

Nafasi ya habari

Kutokana na hili, nafasi ya habari imepata fursa ya kufanya mjadala katika tamasha ambalo limehitimishwa; Katika viwanja na fukwe za Otranto, wamezungumzia kwa kina juu ya mfumo wa habari za kugusi ( fake news); hata za kutoa habari mbaya, na uchakachuaji wa habari, pamoja  na nafasi ya vyombo vya habari vya kijamii. “Waandishi wa habari hawatoi suluhisho la matatizo yaliyopo, lakini wanao uwajibu mkubwa”, amesisitiza Bwana Stefano Pilli Kaimu Mkurugenzi wa Gazeti la Ansa ambapo katika Mashindanuo amepokea naye tuzo kutokana na kuandaa mpango wa Habari za wahamiaji, yaani  (Infomigrants) ambalo ni huduma inayotolewa  katika lugha mbalimba kwa ajili ya wahamiaji zinazotolewa na Gazeti la Ansa , kwa ushirikiano wa Vyombo vya habari vya Ufaransa na Deutsche Welle (DW) pia hata Paolo Messa mwanzilishi wa Portale “Fomiche”.

Washindi katika sekta tatu za mashindano

Washindiwamegawanyika katika sekta tatu inayohusu mada ya amani na wahamiaji; Sehemu nyingine inayohusu  Mediterranea na haki ambazo hazitambuliki; na Sehemu ya tatu inahusu Ugaidi wa kimataifa.

Ubunifu wa teknolojia wa Vatican News

Hata hivyo kuna aina nyingine ya zawadi iliyotolewa nje ya mashindano ambaye imekwenda kwa Vatican News kutokana na ubunifu wa kiteknolojia, kwa ajili ya video zilizoonesha wakati wa kutoa zawadi, ambazo mwezi Desemba mwaka jana walionesha juu ya kazi ya mageuzi ambayo vyombo vya habari Vatican vilikuwa vikiendelea kujikita na mchakato huo kwa kusindikizwa na baadhi ya mabaraza ya kipapa.  Aliye onesha na kupokea zawadi hiyo na Massimiliano Menichetti mratibu wa Habari kwa lugha nyingi Vatican akiongozana na kikundi cha wanahabari wa Vatican  na waandishi wengine, kwa upande wa Video Benedetta Capelli, Cecilia Seppia, Emanuela Campanile,pamoja  na wahaudumu wa Papa, Cesare Cuppone.

Na katika sababu zilizosukuma ubunifu wa lazima leo hii  kusimulia matendo ambayo yanaendelea kwa ajili ya vyo vya habari Vatican ni ile ya  kuwa makini zaidi kwa masuala yanayo husi abinadamu, katika haki, na mada nyingi zinzohusu amani na mazungumzo

 

17 September 2018, 14:38