Tafuta

Vita kati ya Israeli na Palestina unaendelea. Vita kati ya Israeli na Palestina unaendelea.  (AFP or licensors)

Mazungumzo ya simu kati ya Papa Francisko na rais wa Iran,Raisi

Mazungumzo ya viongozi hawa yalifanyika Dominika alasiri tarehe 5 Novemba 2023 kama ilivyothibitishwa na Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican kwa waandishi wa habari.

Vatican News

Papa Francisko alizungumza kwa simu Dominika alasiri tarehe 5 Novemba 2023 na rais wa  Jamhuri ya Iran,  Ibrahim Raisi. Hayo yalithibitishwa na Msemaji wa Vyombo vya Habari Vatican, Dk. Matteo Bruni, akithibitisha juu ya mazungumzo hayo kwamba yalifanyika kwa maombi kutoka kwa Mkuu wa Serikali ya nchi hiyo ya Iran.

Hata hivyo katika Tovuti ya Rais wa Iran inabainisha kuwa Mkuu wa Nchi hiyo, Raisi alipongeza miito mingi ya Papa kuhusu kusitisha moto huko Gaza. Wito wa Papa Francisko ambao ulirudiwa tena mnamo Dominika tarehe 5 Novemba 2023 kwamba: “Ninaendelea kufikiria juu ya hali mbaya ya Palestina na Israel, ambapo watu wengi wamepoteza maisha. Tafadhali acha, kwa jina la Mungu: sitisha moto! Ninatumaini kwamba njia zote zitafuatwa ili mzozo huo uweze kuepukwa kabisa, waliojeruhiwa wasaidiwe na misaada iweze kuwafikia wakazi wa Gaza, ambako hali ya kibinadamu ni mbaya sana. Waachilie mateka mara moja. Miongoni mwao pia kuna watoto wengi, warudi kwenye familia zao! Ndiyo, hebu tufikirie kuhusu watoto, watoto wote waliohusika katika vita hivi, pamoja na Ukraine na migogoro mingine: hivi ndivyo maisha yao ya baadaye yanavyouawa. Tuombe nguvu ya kusema “inatosha,” alisisitiza Papa kwa masikitiko.


Mnamo tarehe 30 Oktoba 2023, mazungumzo ya simu yalifanyika kati ya Askofu Mkuu Paul R. Gallagher, Katibu wa Vatican wa uhusiano na Mataifa na Mashirika ya kimataifa, na Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, pia katika kesi hiyo kwa ombi la Iran. Katika mazungumzo hayo, Dk. Matteo Bruni aliripoti kuwa, Askofu Mkuu Gallagher alielezea "wasiwasi mkubwa wa Vatican kwa kile kinachotokea kati ya Israel na Palestina, akisisitiza juu ya hitaji kamili la kuzuia kupanua mzozo na kufikia suluhisho la serikali mbili kwa utulivu wa amani ya kudumu katika Mashariki ya Kati”.

Hata hivyo katika siku za hivi karibuni, mazungumzo mengine ya simu ya Papa yamejulikana kwa mfano: mnamo tarehe 2 Novemba 2023, Baba Mtakatifu  rancisko alizungumza na  Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, mnamo Oktoba 26 na Rais wa Uturuki, Bwana Recep Tayyip Erdoğan na Oktoba 22 na Rais wa Marekani Bwana Joe Biden. Papa Francisko  pamoja na mambo mengine, amekuwa akionesha mara kwa mara haja ya kutafuta njia za amani na matumaini ya kuweza kufikia suluhisho la serikali mbili na hadhi maalum kwa Yerusalemu.

Mazungumzo ya Simu kati ya Papa na Rais wa Iran, Bwana Raisi
06 November 2023, 09:36