Tafuta

2023.06.07 Dakika moja kwa ajili ya amani 2023: Ukraine, Nchi Takatifu na ulimwengu mzima. 2023.06.07 Dakika moja kwa ajili ya amani 2023: Ukraine, Nchi Takatifu na ulimwengu mzima. 

Papa:Tarehe 8 Juni ni dakika moja ya kuomba kukomesha vita duniani!

Mwishoni mwa katekesi yake,Papa aliwataka waamini wa madhdhebu yote na dini mbalimbali kujiunga na mpango wa“Dakika kwa ajili ya amani”wa Chama cha matendo Kikatoliki kimataifa kilichopendekeza kusimama kidogo tarehe 8 Juni saa 7.00 ili kuomba amani kwa ajili ya mabara matano hasa kwa ajili ya Ukraine.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Amani nchini Ukraine, Zuppi alitumwa na Papa huko Kyiv mnamo 5 na 6 Juni 2023 kwa Mwaliko mpya wa kuombea amani duniani.  Papa Fransisko alihutubia kabla ya kuhitimisha katekesi yake katika  Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican huko , akiomba kila mtu kuomba maelewano kati ya watu. Papa ameomba kwa hiyo sala hasa kwa ajili ya Ukraine, ambapo ujumbe wa Kardinali Matteo Zuppi ulihitimishwa tarehe 6 Juni  uliotumwa kusikiliza kwa kina mamlaka ya Ukraine juu ya njia zinazowezekana za kufikia amani ya haki na kuunga mkono ishara za kibinadamu zinazochangia kupunguza mvutano”, kama ilivyoelezwa katika taarifa kutoka mjini Vatican.

Katekesi ya Papa
Katekesi ya Papa

Baba Mtakatifu Francisko kwa maana hiyo ameonesha mawazo yake kwa nchi ya Ulaya Mashariki kwa zaidi ya mwaka mmoja iliyojaribiwa na vita pia kwa maneno aliyolekezwa kwa waamini wanaozungumza Kipoland, ambao alipendekeza, kwa mara nyingine tena, kudumu katika upendo wa Kikristo na kuunga mkono Waukraine  na kuhitimishwa kwa , salamu yake kwa mahujaji wa Italia, akiwaomba waamini wa imani mbalimbali na madhehebu ya  kidini, kujiunga, Alhamisi tarehe 8  Juni katika  mpango wa Chama cha matendo KatolikiKimataifa kwa Dakika ya Amani kwa Ukraine, Nchi Takatifu na dunia nzima. Kwa hiyo saa saba kamili Mtanadao wa Kimataifa wa matendo kikatoliki inapendekeza kwamba wamini wa maungamo na dini mbalimbali wakusanyike katika sala, wakitoa muda wa daskika moja. Tunakaribisha mwaliko huu, tukiombea mwisho wa vita duniani na hasa kwa Ukraine mpendwa na anayeteswa”.

Kusali kwa ajili ya amani duniani
Kusali kwa ajili ya amani duniani

Ni mpango rahisi" kwa mujibu wa msemaji wa  Jukwaa la Kimataifa la Matendo ya Kikatoliki, likipendekeza kwamba kila mtu aeneze ndani ya familia, kati ya marafiki, katika vyama, mahali pa kusoma na kazini. Pendekezo ni kusimama kwa dakika moja ili kuomba au kutoa  mawazo kwa ajili ya amani”, tarehe 8 Juni saa saba  katika nchi na mahali  popote walipo. “A minute for peace” ilizinduliwa kwa mara ya kwanza tarehe 6 Juni, 2014, kwa kuunga mkono “Ombi la Amani”lililohamaishwa na Papa Francisko, ambayo ingefanyika siku mbili baadaye katika Bustani ya Vatikani pamoja na rais wa Israeli wa wakati huo Simon Peres na rais wa Mamlaka ya Palestina Maḥmūd ʿAbbas, na ambapo patriki Konstantinople Bartholomew I alikuwapo. Ili kukuza mpango wa maombi, Jukwaa la Kimataifa la Matendo ya Kikatoliki lilizindua hashtag #unminutoporlapaz kwenye mitandao ya kijamii na kufanya kupatikana kwenye tovuti yake mfululizo wa nyenzo na mwongozo mdogo wa kukusanyika na kusali na tarehe 10 Juni inaalika mkutano mfupi wa maombi mtandaoni na baadhi ya marafiki kutoka nchi zenye migogoro.

Baada ya Ketekesi Papa ameomba kusali Juni 8 kwa ajili ya amani Ukraine, Nchi Takatifu na ulimwengu mzima
07 June 2023, 16:52